Mweleze kuwa umemsanehe, na kweli umsamehe. Kusamehe sio kurudiana ila ni kumwachilia moyoni na usiwe na kinyongo wala hasira naye, tena hata mkionana. Kama huwezi, Mungu anaweza kukusaidia.
Kusamehe ni faida yako wewe wala si yake tu. Usiposamehe sio tu Mungu hatakusamehe, bali hali hiyo ya uchungu inaweza ikaendelea kukusumbua kwa mahusiano mengine.
Tafuta muda ikiwezekana mweleze msimamo wako. Kuogopa kutoonana sio suluhisho, kwa kuwa siku moja mnaweza kukutana. Dawa ni msamaha unaotoka moyoni, kwa Mungu yote yawezekana.