Nimeshindwa namna ya kumshauri...

Nimeshindwa namna ya kumshauri...

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Kuna msg imeingia kwenye simu ya mke wangu ikitoka kwa wifi yake (mke wa mdogo wake) . Clearly ni ya mapenzi akisema wataonana na bla bla zingine; na leo kweli ameamka anasafiri kwenda mjini? Msg ilikuja kwa bahati mbaya maana alikuwa anaongea na mke wangu muda huo huo, hivyo alituma kwa namba ya mke wangu instead ya mwanaume.

Tatizo: Mke wangu anataka kuiforward kwa mdogo wake. Nimekataa maana itavunja ndoa. Mke wangu anasema atakuja kuwaulia ndugu yao kwa ukimwi maana it seems siyo mwaminifu! Nimemwambia anipe muda nitafakari how to handle this situation. Concern ya mke wangu ni ndugu yao kupata magonjwa hasa UKIMWI.

Nimpe ushauri gani?
 
Kwa mtazamo wangu, Ikiwezekana mkeo ampigie simu wifi yake kwa upole kabisa na busara kwamba kwa bahati mbaya ile sms aliyokua anatuma sehemu nyingine imekuja kwake na amuombe tu anachofanya sio kizuri Kama mwanamke mwenzake, angeweza kumwambia mumewe lakini hajapenda kufanya hivyo akiamini kwamba ilo litaharibu ndoa yao hivyo ameamua kumwambia mwenyewe ili abadilike na haache hayo mambo Kama ataamua kuendelea na kuto badilika basi itabidi aseme.

Nadhani ilo litamtesa kwa kumpa hukumu ndani ya nafsi yake kwa mstaarabu ataomba msamaha ila kwa aliye vurugwa ataonekana tu kwa mwitikio wake na apo Sasa anaweza enda kumwambia ndugu yake.
 
Ushauri wangu ni kumuita huyo wifi wa mkeo muongee naye kwa kina. Awape namba na jina la huyo mwanaume wake mumpigie na kumuonya aache upuuzi wake wa kutaka kuvuruga ndoa ya watu. Na huyo wifi wa mkeo mumpe onyo kali sana.
 
Asante. Mke wangu ali propose hiyo njia nikasema inaweza ikaleta confrontation kati yao maana alikasirika sana ! Fine ngoja apoe kwanza aweze kumwambia kwa upole as you proposed. Ngoja tulitafakari
 
Amueleze tu Ndugu yake acha kumzuia zuia Asipokuwa makini na kukusikiliza wewe ipo siku kaka yao atakuja kubambikiwa mtoto ambaye sio wake na atamlea

Ndoa ya Aina hiyo ndoa gani sasa hiyo !??

Hiyo ndoa au kikundi cha VICOBA!?
 
Amweke wazi tu mdogo wake. Kuna mambo ya kuyakalia kimya ila sio masuala ya kukosa uaminifu kwenye ndoa.
Nakubaliana na wewe, ila reaction ya mwanaume inaweza ikawa ya kuvunja ndoa.... kukosa amani nyumbani maana hata akitoka kwenda kulima.. amekwenda kwa wanaume etc etc
 
Ushauri wangu ni kumuita huyo wifi wa mkeo muongee naye kwa kina. Awape namba na jina la huyo mwanaume wake mumpigie na kumuonya aache upuuzi wake wa kutaka kuvuruga ndoa ya watu. Na huyo wifi wa mkeo mumpe onyo kali sana.
asante ngoja tulitafakari
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
mkuu nahisi hiyo txt ulikua unatumiwa wewe ndio maana hutaki mkeo afanye anachotaka kifanya.

comment tayari.
Nipe ushauri. Mimi sikuwepo , nilikuja ananionyesha, kama ilikuwa yangu yanini anionyeshe?
 
mkuu Mimi navyofaham ni kwamba nyama ya mtu ni tamu na ukianza Kula ni ngumu kuacha......

labda kama tayari Wana watoto, tofauti na hapo mnachokilea hapo majibu yake mtayapata siku moja.

uaminifu ukikosekana hakuna ndoa tena hapo ...ni kumuachia kila mmoja akafaidi anakoona ni kutamu zaidi... yanini mtu aje aanguke presha kama c kutangulia mbele ya haki kisa mwenza...

yapo yanayoweza kusuluhushika ila haya yanayovunja uaminifu katika ndoa huwa ni disrespectful act na ni kama nyama ya mtu mmoja akianza kula ujue ataendelea kula Tu.....
 
mwambie mkeo aongee na mdogo wake,kipi wifi yake anakikosa kwake?? wanawake sisi ni baadhi yetu tu ndio huwa tunachiti wengi ni wavumilivu ndoani,LOL...we always want to feel SEXY,LOVED AND WANTED...hii ni CONSTANTLY ..sasa kuna kitu kinamiss hapo...mwambie mkeo aongee na mdogo wake..LOL
 
Rebeca uache kulalia upande wa mwanamke mwenzio najinyonga kwa mlenda 😂
 
mwambie mkeo aongee na mdogo wake,kipi wifi yake anakikosa kwake?? wanawake sisi ni baadhi yetu tu ndio huwa tunachiti wengi ni wavumilivu ndoani,LOL...we always want to feel SEXY,LOVED AND WANTED...hii ni CONSTANTLY ..sasa kuna kitu kinamiss hapo...mwambie mkeo aongee na mdogo wake..LOL
Yaani mtu achepuke halafu uende kuuliza upamde wa pili kuwa umepungukiwa na nini? Kweli kabisa? Aisee hapana. Issue adeal na mchepukaji tu. Hii ni kuhamisha tatizo kwa asiyehusika!
 
adili na huyo wifi ake tu kiutulivu lakin ajue shida ya yeye kutoka nje ni nini??
 
Back
Top Bottom