Nimeshitakiwa kwa kosa la kutishia maisha,wanasheria msipite hapa kimya tafadhali!

Nimeshitakiwa kwa kosa la kutishia maisha,wanasheria msipite hapa kimya tafadhali!

The GT

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2015
Posts
461
Reaction score
529
HESHIMA NA IWE KWENU WAKUU.
Miezi mitatu imepita sasa tangu watu wasiojulikana kuvamia kibanda changu cha biashara mara 2 ndani ya mwezi mmoja na kufanikiwa kuiba mali zenye thamani kubwa hali iliyopelekea nifikiri mbali sana baada ya kushirikiana na uongozi wa kijiji na kushindwa kuwapata wahalifu hao niliamua nijiingize kwenye imani zetu zile ndipo nilipoenda kwa mganga wa jadi aliyepo kijijini hapahapa ambapo nilipofika kwa huyo mganga kwa utaalamu wake aliniambia kuwa mwizi huyo ni workmate wangu aliyemtaja kwa jina na sasa huyo workmate ni ndugu kabisa na huyo mganga(Huyo workmate wangu ni mzawa wa kijiji hiki ninachofanyia kazi).Mganga akadai kuwa haijalishi kuwa ana undugu na huyo mtu yeye hafugi ubovu hivyo atanisaidia,ambapo aliniagiza nipeleke baadhi ya vitu ili zoezi lifanyike si la kuua bali kumwita huyo mwenzangu ili tukayamalize.Kumbe baada ya zoezi hilo kufanyika,mganga alinisaliti na kwenda kumueleza huyo ndugu yake yaliyoyojiri na sasa nimeshitakiwa hivyo.
KISHERIA NAPONAJE HAPA MWENZENU?
 
Kosa la kwanza kulifanya kwenda kwa mganga, Na kosa la pili kukuambia kama mdogo wake na wewe ukakubali kuendelea na mchakato wa kishirikina. Kwasababu damu nzito kuliko hela uliotaka kumlipa mganga.

Kuhusu sheria. Jee umefunguliwa kesi mahakamani? Au ulikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi? Vipi Ulitoa kauli ya kumtishia maisha Workmate wako au Mganga au mtu yeyote yule?
 
Ahsante sana ndugu tozi25 .Binafsi nakiri kukosea huko maana nilizidiwa na jaziba,sasa ningependa nikujibu maswali uliyoniuliza hapo juu kwani nimejaribu kuqoute imeshindikana.
1.Nimeshitakiwa ofisi ya serikali ya kijiji ambapo nimekanusha madai hayo na uongozi wa kijiji umekosa sheria ya kutumia kunikuta na hatia ila nje ya mazungumzo ya kisheria,limezungumzwa sana hadi mshitaki kufikia kutaka kulipwa laki 3 mazungumzo ambayo yalijikita kuangalia mahusiano yetu tu ya kijamii na kikazi.
2.Sikuwahi mtamkia neno lolote baya la kumtishia huko huyo workmate mwenzangu au mganga mwenyewe ila hoja hiyo ameianzisha yeye mwenyewe baada ya kuambiwa na huyo m ganga.
 
Endelea kukana mpaka mwisho,huyo mganga ushahidi wake ni hafifu,na mganga na yeye mkane kua hujawahi kwenda kwake

ploudly ngosha [emoji243][emoji243][emoji243]
 
Kwenye wekundu hapo ndio jibu lote kuwa hujakutwa na hatia kwahio wewe hauna kosa ulilo tenda.
Na hapo kwenye blue mazungumzo nje ya sheria ina maana hii ni kupatanishwa tu kwa hitilafu iliotokea au?
Mwisho hii kwenye kijani mahusiano ya kijamii na kikazi hapa kwa nilivyo fahamu kuwa wewe na huyo aliepeleka madai anataka haki yake ya mshahara wake wa kufanya kazi kwako sijui nipo sawa? Kama nipo sawa hapo sheria itakuhusu kumlipa mshahara wake.
 
Ahsante sana tozi25 kwa mwangaza wako,suala la laki 3 sio kuwa nimlipe mganga kwa kazi aliyoifanya,ila ni huyu workmate wangu ambaye alipoambiwa na mganga basi wameunda hoja ya uongo kuwa moja kwa moja nilifika kwa huyo mganga kwa kutaja jina lake na kumuomba mganga amshughulikie huyo bwana kitu ambacho si kweli na ndipo msingi wake wa mashitaka kuwa nilitaka kumdhuru.Hivyo hiyo laki 3 ni kama fidia kwa kosa la kutishia maisha hitimisho ambalo limezingatia vielelezo tu vya kijamii na mahusiano na si hitimisho la kisheria.
 
Maelezo yako hayajitoshelezi. Lakini kama ndivyo mambo yalivyo namna maneno yako yalivyodhihirisha, basi ondoa shaka.

Ili kupata msaada wa kisheria, sharti umweleze wakili habari sahihi ya mambo yaliotokea hata kama yanaoneka kukutia hatiani. Unapoficha chochote unamfanya wakili ashindwe kukutetea mara yale ambayo hukumweleza yanapojitokeza mahakamani.

Sent from iPhone 9
 
hivi suala hili la kumueleza wakili ukweli hawezi kukusaliti
 
Endelea kukana mpaka mwisho,huyo mganga ushahidi wake ni hafifu,na mganga na yeye mkane kua hujawahi kwenda kwake

ploudly ngosha [emoji243][emoji243][emoji243]
dah! Kmmae mganga wa watu mnatenga kiasi hicho hahaha, waganga anzeni kufunga cctv.
 
Bado naendelea kupata mawazo yenu,nashukuru kwa mnaothubutu kuchangia.
 
ukikana mashtaka mpaka mwisho hiyo kesi unashinda pia unaweza kwenda mahakamani na kumfungulia mashtaka huyo kijana na mganga wake kwa kukuchafua ili akulipe fidia na uzuri wake ulishakana toka mwanzoni
 
Back
Top Bottom