Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kuna msemo kwamba mtu anaweza kutenda au kufanya kitu ambacho kitamfanya hadi mtu aliyekufa na kuzikwa kaburini ageuke. Ndivyo nilivyohisi Nyerere akifanya kufuatia kauli ya Kanali Ngemela Lubinga juu ya msimamo wa sasa wa CCM katika suala zima la uchumi wa kidiplomasia.
Akihojiwa na mwandishi Khalifa Said, Kanali Lubinga alitamka bila kupepesa macho kwamba Tanzania bado ina msimamo wa kusaidia nchi zinazotawaliwa kimabavu na kunyanyaswa na mataifa mengine, kama vile Palestina dhidi ya Israel na Polisario dhidi ya Morocco. Hata hivyo msimamo wa sasa wa CCM na serikali yake ni kwamba tunabadilika na wakati, kwamba tutaendelea kupinga utawala wa mabavu dhidi ya Polisario na Palestina, lakini hilo halitatuzuia kuanzisha uhusiano wa kibalozi na nchi zinazowakandamiza, kwa kuwa kwanza kuna maslahi ya kiuchumi. na pili kuna faida ya kuwa karibu na adui yako.
Kwa mtazamo huu wa CCM, ni sawa na kuitangazia dunia nzima, pamoja na nchi kama Afrika Kusini na Namibia, kwamba kama wasingekuwa wamefanikiwa kuuangusha utawala wa kimabavu na kibaguzi wa Makakaburu, leo hii Tanzania ingeanzisha uhusian wa kibalazi na makaburu na kuwakaribisha kufungua ofisi ya ubalazoi nchini, huku bado tukiendelea kuwasaidia Afrika Kusini na Namibia kupigania uhuru!
Kanali Ngumbalu alienda mbali ya hapo. Alipoulizwa kuhusu Tanzania kuunga mkono na kushiriki kushangilia Marekani kuhamishia ubalozi wake toka Tel Aviv kwenda Jerusalaem kinyume na azimio la Umoja wa Mataifa, pale ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo Dr. Mahiga aliposhiriki na Trump katika sherehe hiyo, Kanali Lubinga alitoa msimamo kwamba Tanzania ina sera zake (ambazo wakati mwingine zitapingana na maazimio ya Umoja wa Mataifa), sawa na hili suala la kuiunga mkono Marekani kinyume na Azimio la Umoja wa Mataifa katika suala la Jerusalem!
Nimeshituka sana na msimamo huu wa serikali ya awamu ya tano chini ya CCM. Kwa mara nyingine nimeshukuru kwamba Nyerere alikufa kabla ya kuona aibu kama hiii, maana sijui angeficha wapi uso wake. Ni aibu ambaye ingeweza kumuua Nyerere kwa mshituko. Na kama waswahili wanavyosema, Nyerere must be turning in his grave kwa ajili ya vitu kama hivi toka chama cha siasa alichokiasisi!
Ningetamani sana kusikiliza haya mahojiano na Prof Kabudi, na niwe na swali moja tu kwake; really, we can stoop so low on foreign policy?
Source: