Nimeshitushwa sana na kauli ya CCM ikionyesha kuwa South Africa au Namibia wasingekuwa huru hadi leo, tungeanzisha uhusiano wa kibalozi na Makaburu!

unajua ni watanzania wangapi wamefariki kwa ajili ya kukomboa hizo nchi, unajua familia zao zina hali gani sasa kila mtu apambane na hali yake diplomasia ya uchumi ndiyo inatakiwa kwa sasa ugomvi wa wapalestina na isarael hautusaidii chochote si tuangalie ni maslahi gani tutapata toka kwao
 

kwani hao Palestina na Polisario kuna walichokipata huko UN? mbona munajifanya munawa support?
 
Ebu msikilize Lubinga hakuna aliposema hayo! Huyo mleta hoja ameweka tafsili yake na nyinyi ndiyo mnayoijadili. Msikilizeni Kanali mwenyewe maana mahojiano yameambatanishwa. Sasa nyinyi mnatoa maoni yenu kwa wrong information mliyopewa. Sikiliza mahojiano kwanza ndipo ujadili, maana uliyotafuniwa na mleta hoja siyo. Ukweli! Ameumeza ukweli wewe akakulisha makapi aliyopaswa kutema!
 
Ndugu kwa sasa watanzania hawatanii wameshalijua zimwi likujualo mfano wakina lisu hawajapona kwa bahati mbaya ni swala la mda tu KUWA SEHEMU YA MABADILIKO NA MABADILIKO YANAANZA NA WEWE CCM is an old lion
 
Siku hizi hata majuha wanaingia JF...mkuu huu Ni uwezo wa chini kabisa wa kujenga hoja,
.Kama umetumwa unawaangusha walio kutuma ,Kama ndio akili zako...pole Sana!
 

UPO SAHIHI MKUU!
 
Hivi una akili wewe? Soma kichwa cha thread vizuri na jifunze kufanya inference. Ndio maana kuna w=viwango tofauti vya shule. Unajua maana ya foreign policy, au unafikiri Tanzania itakuambia foreign policy kwa ajili ya kila nchi?
 
Siku ukipatwa na janga nyumbani kwako na familia yako na majirani wako wakakupuuza bila msaada ndio utaelewa maana ya unachosema. Kwani jirani zako wanapokusaidia wanapata faida gani, haiwasaidii chochote wanapaswa kuangalia maslahi yao. Ukivamiwa na majambazi kuja kutoa msaada wanaweza kufa bure. Sasa skeli ya jirani ndiyo hiyo inakua hadi kuwa skeli ya taifa. Lakini huwezi kuelewa kwa kuwa una roho ya shetani wewe, nikijua wewe jirani yangu nahama hiyo sehemu.
 
Dunia imebadirika afrika kusini wangekuwa wema tuliowatendea wangekuwa wanatuheshimu Sana watu hujifunza kutokana na makosa wale tuliokuwa tunaona ni maadui Sasa hv ndio wanaongoza kutusaidia mfano Korea kusini
 
Dunia imebadirika afrika kusini wangekuwa wema tuliowatendea wangekuwa wanatuheshimu Sana watu hujifunza kutokana na makosa wale tuliokuwa tunaona ni maadui Sasa hv ndio wanaongoza kutusaidia mfano Korea kusini
Nimeuliza hapo juu, kwamba hivi ilikuwa sera yetu kuzisaidia hizi nchi kujikomboa ili tuje tufaidike nazo? La hasha kabisa. Sisi tuliwasaidia kutokana na kuwa watu wenye utu, sio kwa kutegemea kulipwa fadhira sijui watu wetu wakienda kwao kinyume cha utaratibu wasipigwe. Na kama kuna watu katika nchi hizi wameamua kuwa walevi tu na wapumbavu wa kufanya xenophobia, hicho si kitu cha kutufanya sisi tubadilishe msimamo wetu katika watu wnye utu na kusimamima usawa wa binadamu. Unamwona mpumbavu anakula kinyesi na wewe unaamua kunywa mkojo, akili gani hiyo?
 
Labda nikusaidie maana tutabisha bila kufika mwisho nchi inaendeshwa kwa Sera za chama kinachotawala wakati ule Sera yetu ya Mambo ya nje ililenga ukombozi kusini mwa afrika lakini kwa dad's Sera yetu ya nje ni diplomasia ya uchumi
 
Labda nikusaidie maana tutabisha bila kufika mwisho nchi inaendeshwa kwa Sera za chama kinachotawala wakati ule Sera yetu ya Mambo ya nje ililenga ukombozi kusini mwa afrika lakini kwa dad's Sera yetu ya nje ni diplomasia ya uchumi
Ewaaa! Ndio maana nikasema, kwa hiyo dad's Sera yetu ya nje ya diplomasia ya uchumi, leo Afrika Kusini na Namibia wasingekuwa huru tungewaalika Makaburu kufungua ubalozi Tanzania huku tukidai tunawasidia Afrika Kusini na Namibia kupigania uhuru.

Sasa umenielewa Mkuu
 
Mkuu, ukilinganisha kipindi Kolimba alipotoa hiyo kauli na sasa, basi nadhani hata Kolimba is turning is his grave! Kama alidhani hali ilikuwa mbaya wakati huo, imagine sasa hivi!

Ndugu yangu, sikio la kufa Halina dawa. Hata akija Yesu leo na kufanya miujiza, CCM haiwezi kupata pumzi. Najua nia ipo, lakini uwezekano haupo.

Tatizo ni kwamba hata ukatumbua watendaji woteeeee, bado tatizo liko pale pale. Hali halisi huko ndani ni mbaya kuliko sisi tunavyoelewa.

Hali ni mbaya ndugu yangu. Kubwa zaidi hakuna aliyetayari kuungama mbele ya wananchi na kuisema, sisi ndio wahusika wa matatizo yaliyopo ndugu watanzania- Tunawaomba radhi kwa niaba ya chama chetu. Ikitimia siku hiyo ndio kaburi la Kolimba litazungumza!!!!!!!!! kwani naye atakuwa ameombwa Radhi.
 
Hivi una akili wewe? Soma kichwa cha thread vizuri na jifunze kufanya inference. Ndio maana kuna w=viwango tofauti vya shule. Unajua maana ya foreign policy, au unafikiri Tanzania itakuambia foreign policy kwa ajili ya kila nchi?
Ila kiwango cha shule changu hukifikii na nimesimiliza hayo mahojiano toka mwanzo mpaka mwisho, na kulinganisha na kichwa cha habari- pia na contents zake. Jamaa ana infer mambo ambayo kanali Lubinga hakusema!
Usibishe tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…