Nimeshuhudia aisee Kilimo kinalipa sana

Shughuri za kilimo na kiuchumi za kusimuliwa siku zote Huwa za mafanikio tu,utasikia kilimo Cha matikiti kinalipa,maesabu ya vikokotozi na cm,siku zote ni mazuri,
Reality ni kitu tofauti,unataka kujua shughuri fulani inalipa,ingia field,Hz story za mitandaoni,achana nqzo
 
Tangu lini kijijini kukawa na maisha mazuri? Acha blaa blaa..

Watakuwa wamejenga shelter sio nyumba
 
Wakuu kuna fursa hapa,zinahitajika tani 100 za ufuta mweupe na kwa bei nzuri utanunuliwa.DM iko wazi kwa wahusika.

ANGALIZO:UWE SERIOUS NA BIASHARA.
 
Imewachukua miaka mingapi kuwafikia hapo walipo nadhani hukuwauliza. Wanalima nini na kwa mfumo gani wa umwagiliaji?, kutegemea mvua au kuna chanzo cha maji visima, mito n.k.
Hizo bidhaa soko lake lipo wapi ambapo hupeleka?.
Mbali na kilimo wanajishughulisha na nini vingine kama vyanzo vya mapato? nadhani ndiyo maswali ya muhimu na uchunguzi wako ungelenga huko kwakuwa unaweza ukakuta yupo kwenye kilimo lkn anauza duka la jumla au ananunua ndizi au nazi kwa wakulima kulangua kisha anapeleka mjini ndiyo iliyompa mafanikio lkn kwakuwa humuona shambani pia ukadhani kilimo cha alizeti ekari tatu ndio kimemtoa kwa kujenga na kununua hadi Noah.
Jifunze kama unataka kulima anza na wewe kulima kidogo kama mara tatu usije na matokeo yako kichwani tikiti ekari moja unapata milioni 24 unaweza ukachezea za uso hata laki usipate.
 
Kalime mkuu huta jura lakini sio Mahindi ya ugali hayo faida kiduuuchu
 
Kalime mkuu huta jura lakini sio Mahindi ya ugali hayo faida kiduuuchu
Kama ni mahindi napo kulima ni mahindi gobwa gobwa maarufu ya kuchoma. Uzuri yanasoko na hayatumii gharama kubwa sana katika kuhudumia kama mazao mengine ya nyanya, tikiti, hoho n.k
 
Ulichokiona ni kweli na hakika... Usisite jitose
 
Wapi huko??kama si wavivu?
 
Wakuu kuna fursa hapa,zinahitajika tani 100 za ufuta mweupe na kwa bei nzuri utanunuliwa.DM iko wazi kwa wahusika.

ANGALIZO:UWE SERIOUS NA BIASHARA.
Hizi biashara za Tani kadhaa za ufuta sijui tani 10 za zao gani huwa miyeyusho! Hizo Tani utazitoa wapi katika hali ya kawaida?
 
Hii ni nzuri.
 
Tangu lini kijijini kukawa na maisha mazuri? Acha blaa blaa..

Watakuwa wamejenga shelter sio nyumba
Mkuu, ukishafika vijijini?

Siyo kila kijiji kina maisha mazuri kama ambavyo si maeneo yote ya mijini Yanaaisha mazuri.

Ukitembelea baadhi ya maeneo katika baadhi ya mikoa Tanzania, mfano Machame, Marangu, Meru, Kagera, n.k., utaamini kuwa kuna vijiji vina maendeleo makubwa sana na hivyo maisha yake kuwa ya "kuvutia".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…