Nimeshuhudia baadhi ya wachaga na wakinga wanaacha ajira nzuri wanaingia mazima biashara ambazo zina hatari ya hasara, huu ujasiri wanautoa wapi?

Nimeona mchaga marehemu Mengi akiwa mhasibu wa kwanza kutambulika hapa nchini akiacha ajira nono.
Hujui historia ya Mengi. Uliza kwanza! Mengi ndio watanzania wa kwanza kupata CPA (or kitu kama hicho kwenye mambo ya biashara from UK). Katika Africanisation, Nyerere alipenda kuona waafrika wanakuwa kama wahindi kushiriki secotr binafsi katika kukuza uchumi wa nchi. So akaamrisha BOT iwape mitaji mikubwa. Wakapewa and thanks God Mengi managed to make headway in his bussiness!
 
kila mtu ana malengo yake,wengine malengo yao yanatimia kwa mshahara wa laki 3,so akipata ajira ya salary 500k ni neema.viceversa wengine malengo yanahitaji 800k per month,huyu ataona hawez kutimiza akiwa kwenye ajira ya salary 500k atatafuta nje.

lakin wengine wanaachwa bila option baada ya kufukuzwa.too bad hawezi sema amefukuzwa bali "nimeacha hela ndogo"...So ijue vita yako(malengo) then fanya sawa sawa na malengo yako.Maisha hayana formula kila mtu anamtihani wake sio swala la kikabila[emoji2][emoji2]am i clear?[emoji1787][emoji1787]

nje ya topic
watu husema ajira hazimfanyi mtu kuwa tajiri
"jibu ni kuwa,hata kama siwez kuwa tajiri kwenye ajira,sitaki kusimuliwa,niilate kwanza afu ntaamua mwenyewe" alisikika mlevi mmoja
 
Kuna makabila yenye wasomi kama wahaya, wasukuma, wangoni, wanyakyusa, hawa wakilamba kazi shughuli imeisha, mshahara wa uhakika kwao upo sasa kwenda kwenye bishara ambako kuna hatari za hasara kuna maana gani ??
Hakuna biashara isiyo na risk, na wafanya biashara wote waliofanikiwa walichukua risk. Kwa hiyo ukifanya risk, kuna uwezekano wa mara nyingi wa 50:50 kufanikiwa au kutofanikiwa.

Risk zipo katika kila kitu unachofanya maishani. Hata unapopanda gari yako au daladala kwenda kazini ni risk. Kupanda basi kwenda mikoani ni risk. Kupanda ndege ni risk. Watu wanakufa kila siku kwa kufanya hayo, lanini je, utaacha kupanda daladala au basi au gari yako au ndege kwa kuwa kuna risk? No risk no gain.
 
Mwambie huyo
Usisahau mwigulu ni waziri,hajaacha uwaziri sasa hv anamiriki mabasi ya bilioni kadhaa,usimsahau shabiby Mbunge wa gairo,ni Mbunge,na ni mfanyabishara mkubwa tu,wa hotel,mafuta,mabasi,
Kupanga ni kuchagua,hakuna Cha ajabu Wala upekee
 
Passion ,Kazi zina fitina na majungu Sana Bora biashara ina nafuu..

Higher risk higher return
 
Waige uione.

Mkinga tangu akiwa ana miaka 16 anakuwa ameshapanda miti yake ya mbao ya kutosha.

Anapokuja kuvuna tayali kijana mkubwa ndio hao matajiri wa kariokoo.
porojo.....hizo story ndio kichaka cha wakinga wengi....huzitumia ili kuwahadaa baadhi ya watu wanaohoji chanzo cha biashara zao.

kama unadhani kupanda miti ndio kunawatajirisha wakinga, na wewe kijijini kwenu anza kumpandia miti mwanao wa miaka 5 ili akiwa mtu mzima aanzenayo kama mtaji wa biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…