Nimesikiliza mahojiano ya Prof. Assad na Kikeke, huyu Prof. ana ujuaji mwingi. Unafukuzaje mfanyakazi akikataa kufanya majukumu ambayo sio yake?

Kupanga mafile kuna shida gani?, Mimi nimefanya kazi na madriver wenye elimu ya uhasibu 2. Siku ambayo hatuendi field walikuwa wanamsaidia mhasibu kazi za kihasibu, baada ya kuona utayari wao tuliwapandishia mishara.
Umeshasema Wana elimu ya uhasibu
Records and archive management ni taaluma na huyo driver alifanya akaona ugumu ndio maana akaona Bora kuacha Wala hakupaswa kupigiwa mfano kana kwamba ni mvivu na asiefaa ni mtu aliyekataa kufanya kitu kilicho nje ya uelewa wake
Hakuna hata sehem inaonesha prof alitoa ushauri wa huyo mtu kupewa short course ya hiyo kazi mpya ili asiwe jobless kama kweli alikuwa jobless
Kwenye hili Prof ameonesha upande wake wa pili kuwa yeye na Magu sawa sawa
 
Magufuli alijidhalilisha sana kumfukuza kazi kinyume na katiba huyu profesa. Kwanini alikua anaogopa kufanya kazi na watu waadilifu alikua anaficha nini?
 
Mie nimemsikiliza juzi...jamaa ni genius...its a rare gem in Africa...! ndo maana sisytem ikamtema
Mleta uzi anamatatizo ya kuwaelewa ma-genius, hivyo usimlaumu. Bado ana mengi ya kujifunza toka kwa Prof Assad.
 
Samahani ndg!
Je unaweza kuonyesha kifungu chochote kwenye Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma zinazomtaka mtumishi ambaye hatathibitishwa kazini kuishi kama mkibarua?
Standing orders ni kwa ajili ya watumishi wa umma ambao ni pensionable. Kwa vile Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro ni private basi standing orders haziwahusu. Na kwa vile dereva wa ngazi yake sio pensionable hahusiki na standing orders.

Probation period inatoa haki kwa pande zote kuvunja mkataba bila penalties. Ukiacha kazi wakati wa probation period hauadhibiwi ila ukiacha kazi baada ya probation period unatakiwa ufuate hatua kadhaa ( notisi ya muda fulani) ndio usiadhibiwe. Vile vile ukifukuzwa wakati huo bila kufuata utaratibu unakuwa na haki ya kudai fidia.
Wakati wa probation ni wakati wa kujipendekeza. Huyu dereva angekuwa makini angeomba mwenyewe asaidie kupanga mafaili baada ya kuona anashinda siku nzima bila kufanya kazi yeyote.
Kwenye hili hamumtendei haki dereva hasa kwa vile dereva alifukuzwa kwa sababu ya utoro kazini na sio kukataa kupanga mafaili.

Amandla...
 
Kupanga mafile kuna shida gani?, Mimi nimefanya kazi na madriver wenye elimu ya uhasibu 2. Siku ambayo hatuendi field walikuwa wanamsaidia mhasibu kazi za kihasibu, baada ya kuona utayari wao tuliwapandishia mishara.
Dereva kilaza asiyeweza kupanga files sijui hata walimuokata wapi,
 



Huwezi kumuelewa na utamaduni wa uvivu wa kupindukia Tanzania. Yaani unaajiri Dereva ambaye ambaye anashinda kwenye gari kwa masaa nane anamsubiri Boss bila kufanya lolote na tunaona ni sawa!. Si ajabu umasikini umetawala
 
Amekuwa na kazi ya kulalamika tu mda wote.
Ukiwa unafahamu kuwa boti unalosafiria linakwenda kuzama, hutaacha kulalamika kila dakika ili pengine Kapteni atastuka na kuponya mtumbwi.

Ni mwendawazimu tu (ashakum si matusi) ambaye atakaa kimya nyakati kama hizo na badala yake atachekelea na kumpongeza kapteni.
 
Wewe upo hapa kubishana kumbe.
Unaelewa maana ya taaluma kwanza?? Ukienda kuajiriwa kama daktari mahali ukapewa gari la kuendesha mwenyewe kwenda kazini ukiulizwa una taaluma gani utasema una taaluma ya udaktari na udereva??
 
Kwa KAZI yake ya kuwa Auditor Mkuu, anaruhusiwa kuwa Mwenyekit WA Bodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…