Nimesikiliza mahojiano ya Prof. Assad na Kikeke, huyu Prof. ana ujuaji mwingi. Unafukuzaje mfanyakazi akikataa kufanya majukumu ambayo sio yake?

Nani alikuwa anampigia kuzungumza naye siri za kiofisi kwenye simu yake binafsi??
Kwa kazi ya CAG hakuna siri muhimu na ya haraka anayotakiwa kuishugulikia akiwa nyumbani kwake, pia kama ipo inatakiwa atumie channel rasmi za serikali kama email na katika chombo rasmi cha mawasiliano kilichotolewa na serikali.

Wa kwanza kukamatwa alitakiwa huyo aliyempigia kuzungumza siri za serikali katika unsecured network.
 
Inawezekana alishauriwa na mkewe afukuze huyo dereva.
 

Private ipi accountant anakuwa vyote hivyo hapo? Akifanya makosa katika kazi ambayo hajasomea anachukuliwa hatua ama inafagiwa chini ya zulia? Na ukaguzi wa utendaji unawapa hati safi kuwa mhasibu kafanya multitasking?
 
Angeshamove on na mambo mengine, kulalama miaka nenda maana yake sio kichwa kama unavyomnadi hapa.
Wenye akili wanamfuata kutaka kusikia mengi kutoka kwake .unataka awakimbie? Hii nchi wajinga mpo wengi sana .
Hili ni somo kwa viongozi wasiofuata sheria na katiba kama alivokua magufuli.
 
Mambo sio rahisi hivyo, kama huna majukumu ya kufanya kazini unatakiwa uondolewe, huwezi kulipwa wakati huzalishi chochote.
Ww ndio haujui kabisa sheria za Kaz, wanaita, labour laws. Inaangaliwa contract ya ajira kwanza ndugu. Hivyo ni vitu sensitive sana na MACEO wengi wenye kiherere cha kufukuza watu wanasababisha hasara kubwa kwa makampuni na wafanyakaz wanarudishwa kazini.
 
Kama umeajiriwa na imefikia mahali majukumu yako hayapo tena hapo kazini unatakiwa uondolewe hapa kazini au ufanye kazi nyingine,
Unataka ulipwe bure tu wakati hufanyi kazi yoyote??
 
Lazima uhuni wa yule marehemu uanikwe ikibidi kaburi lake likatandikwe viboko. Anawakomesha safi sana mi namkubali sana prof.
Badala ya kwenda mahakamani wangemshauri kwenda mirembe ndiko mahali sahihi kwake kwa wakati huu.
 
Muulize kuna degree au diploma ya driving?. Professional inaanzia bachelor degree na kuendelea, yeye anathani certificate in driving ni taaluma. Nchi hii imejaa wajinga wengi sana.
Kwa hiyo uhunzi na ufinyanzi ama ususi sio profession, ama uchezaji mpira sio profession wala dancing sio profession, wewe kweli unahitaji elimu, madreva wa f1 hawana profession kisa hakuna degree ya udereva?
 
Mie nimemsikiliza juzi...jamaa ni genius...its a rare gem in Africa...! ndo maana sisytem ikamtema

Anchopigania ni nini tofauti na dereva wake? Sababu yeye na Zitto wamefungua kesi ya kutenguliwa kwake haukufuata sheria, mkataba wa kazi aliyopewa alipoajiriwa. Ni miaka minne sasa anapambana mahakamani japo yupo 64/65 umri wa kustaafu ulishapita. Wakati huo Ansema fukuza huyo bila kuzingatia haki zake sababu ni dereva.
 
Private ipi accountant anakuwa vyote hivyo hapo? Akifanya makosa katika kazi ambayo hajasomea anachukuliwa hatua ama inafagiwa chini ya zulia? Na ukaguzi wa utendaji unawapa hati safi kuwa mhasibu kafanya multitasking?
Mhasibu hasomei manunuzi, hr na uhasibu?. Zote hizi ni sehemu ya kozi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…