Nimesikiliza mahojiano ya Prof. Assad na Kikeke, huyu Prof. ana ujuaji mwingi. Unafukuzaje mfanyakazi akikataa kufanya majukumu ambayo sio yake?

Nimesikiliza mahojiano ya Prof. Assad na Kikeke, huyu Prof. ana ujuaji mwingi. Unafukuzaje mfanyakazi akikataa kufanya majukumu ambayo sio yake?

Job description inasema hvyo ntapangiwa kazi zingine if elrctrical job hakuna na supervusor wangu

Kumbuka unaweza kuumia wewe ama kuumiza wenzako. ukiumia wewe ukaamua kusamehe kwa kutafsiri hivyo huo ni ubwege wako, ila ukiumiza wafanyakazi wenzako watachukua hatua wataenda mahakamani kumdai mwajiri wako fidia. Huwezi jitafsiria kadri upendavyo hiyo phrase. Mahakamani unanyooshwa vizuri tu ukishitakiwa na tafsiri sahihi ya hicho ulichosema utapewa.hicho sio kichaka cha kujifichia
 
Wakati akihojiwa na Salim Kikeke,

Aliyewahi kuwa CAG na kuondolewa kwa aibu kuu Prof. Assad anadai kuna mtumishi huko Morogoro aliajiriwa kama Dereva.

Lakini kwakuwa hakuwa na mtu wa kumuendesha basi wakaamua wawe wanampa kazi ya kupanga mafaili.

Jamaa baada ya kuona anafanya kazi ambazo sio zake akaamua kuandika barua akidai alipwe kwa kufanya kazi ambazo sio zake.

Huyu Prof msomi na mshika dini akamuamuru HR amfukuze kazi huyo dereva.

Hapa tunasikiliza mahojiano ya Prof. Akilalamika kufutwa kazi bila utaratibu lakini wakati huo huo anatueleza bila aibu kitendo chake cha kinyama cha kumfuta mtumishi kazi kwa kudai haki zake.

Soma Pia: Prof. Mussa Assad: Taarifa ya utenguzi wangu nilipewa siku moja kabla

Kwa elimu yake hiyo anaona ni sahihi kwa dereva kufanya kazi za kupanga file badala ya kuendesha gari kulingana na mkataba wa ajira yake??

Je yeye huyo Prof. Angeambiwa akadeki korido pale UDSm badala ya kufundisha wanafunzi kukariri madesa angefanya hivyo.

Ama kweli binadamu ni wasahaulifu sana na wanafiki mno.

Huyu keshasahau namna alivyomtenda mwenzake anaona ni haki yake kuonea wengine kwa kuwa kasoma sana ila wenzake hawana haki ya kumfuta yeye kazi.

Such an arrogant and a very useless academician.


View: https://youtu.be/eE2JoDEd43Q?si=vgPL1ihKxMpsLtel

Karma is real. Prof akae kwa kutulia. Cheo alishavuliwa.
 
Kazi ya udereva ishehimiwe kama kama kazi nyingine Doctor,CAG , nurse. Angemtafutia kazi ya udereva kwingine. Asingeweza kufanya hivyo ulaya anapokusifia sana.
Hakukuwa na kazi kwingine. Kumsaidia akampa kazi ya kupanga mafile. Ilikuwa apange mafile au arudi nyumbani. Mjinga kachagua kurudi home.
 
JINGA SANA HUYU MZEE. ANA KAKIBURI FLANI HIVI KA KUDHANI YEYE NI BORA KULIKO WENGINE
Dunia huwa ina namna ya kuwanyenyekeza watu, ukifikiria kuwa wewe ndio kila kitu basi unakuja kutana na jambo litakalokufanya ubadili mtazamo.
 
Asad huwa anaamini hakuna mwenye akili kama yeye!

Hii lilitokana na Sifa alizopewa baada ya kutimuliwa na jiwe!
Zile ndio zikamlevya
 
Dunia huwa ina namna ya kuwanyenyekeza watu, ukifikiria kuwa wewe ndio kila kitu basi unakuja kutana na jambo litakalokufanya ubadili mtazamo.

Sasa analalamika yeye kuvuliwa u CAG ila kumbe naye alimtendea Dereva vivyo hivyo. What goes around comes around.
 
Back
Top Bottom