Nimesikitika sana kwa hiki nilichoona hospitalini

Bila kuitaja hiyo hospitali ni majungu
 
Huyo unapiga shaba afe yeye atangulie kwanza
 

Pole, ni hospitali gani hiyo tafadhali, maana umetoa taarifa lakini umeogopa au umeficha jina la hiyo hospitali. Itaje tu na huyo daktaripia mtaje maana analipwa kwa hizi kodi za wananchi.
 
Mama anaupiga mwingi.

Wana wasiwasi gani wakijua kuwa ikifika saa 10 wanaanza kutibia wagonjwa privately hapo hapo kwenye majengo ya serikali.
Kwahiyo dawa ni kwenda hospitali jioni? Ila wanatakiwa kutoa huduma siku nzima, kila siku, na asiwe mmoja, hapa kuna mushkeli.
 
Taja jina la hospital sio jina la mtu/dr

Ila isijekuwa alikuwa amekesha na ndo aloko tuu hapo
Inawezekana kabisa, pengine hiyo saa 4 anatoka kuwaangalia waliolazwa. Ila kuwatetea wakati mwingine ni ngumu!
 
Mkuu, hiyo kawaida sana kwa hospitali za serikali, wale wenye bima za afya wana unafuu wa kwenda private hospitals. Kiufupi huduma za afya bado ni changamoto sana, ingawa kuna majengo yanayovutia ila huduma zinasikitisha sana.
 
Na k
Na kinachokushinda kuitaja hospital na jina lake na idara anayofanyia kazi ni nn?! Tena ukiwa na fake IDs na unakua na uwoga kwny nshu km hii inayohitaji kuwa exposed ili kuongeza uwajibikaji wa watumishi wa umma?!
Ila baadhi ya wabongo bhn,kuandamana barabaran hamuez na hata huku nako mnashindwa?!

Mkuu umerogwa ama hauko sawa?!!
 
Pale siasa inapoongoza taaluma na uchumi, matokeo yake ndio hayo.

Mbunge wa kuchaguliwa analipwa 11m per month, anakopeshwa ndinga kali ya 200+m, ana marupurupu mengine na ufisadi mwingi, hana cha maana anachofanya zaidi ya kupiga makofi bungeni na anasubiri pension ya 250+m baada ya miaka mitano.

Daktari au engineer analipwa 2+m hana bonuses zozote, hana mianya ya kupiga, anasubiri pension ya 150+m baada ya miaka 30+ ya utumishi.

Unataka uwajibikaji kweli?
 
Pole alikuhudumia??
 
Juzi kati nilikuwa na jambo langu BAKITA, mkongwe mmoja pale akaweka wazi kabisa kuwa anaanza kunywa chai kwanza ndipo ahudumie wateja maana hajanywa chai asubuhi. !! 😲
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…