Nimesikitishwa Taifa Stars Kutembeza Bakuli

Nimesikitishwa Taifa Stars Kutembeza Bakuli

Ndio ndio

Mgonjwa ndio unatakiwa achangiwe..tena baada ya kujiridhisha kuwa kuna uwezekano wakupona au la
Kabisa kabisa tuchangie wagonjwa tu full stop hawa wengine wapambane na hali zao
 
Ongezea :-
Kanisani, msikitini n.k
Mara ya mwisho kwenda kanisani ilikua 2003...nakumbuka nilitoa michango 6 siku hiyo,yqn nilisimama mara sita kwenye seat kwenda kutoa hiyo michango inayoitwa sadaka
 
Hata mimi nimeshangaa sana! Yaani timu ya Taifa imefuzu mashindano ya Afrika halafu serikali inashindwa hata kujenga ushawishi kwa makampuni na mashirika ya umma! badala yake inatupia mzigo kwa wananchi!

Mbona mabilioni ya kuchezea kugharamia uchaguzi wa marudio wakati ule kwa wale wachumia tumbo walio unga mkono juhudi hawakuomba popote?
Nitaichangia Yanga, ila siyo Taifa Stars.
 
Wananchi kuichangia taifa star ni upuuzi mkubwa, ni aibu, ni foolishness kabisa. Hata kuichangia timu kubwa kama yanga ni aibu tena mtu anathubutu kusema eti kiongozi anatakiwa kupenda timu zote, mambo ya kipuuzi kabisa. Haya matimu yanatakiwa yamilikiwe na watu binafsi sisi tuyalime kodi tu. Timu ya wananchi!! Upuuzi wa 1920. Dunia imeshaenda mbali sana kisoka sisi tuko pale pale na tunashangilia.
 
kuna kitu nyuma ya pazia hapa.... CAF wanatoa hela, juzi kati FIFA walitoa dollors za kutosha sana, leo CCm wanakuja kutuletea mambo mseto.

HAPO NIMEGUA WANAANZA VIJISABABU WANAPOKUJA KUFUNGWA Senegal 6-1, Kenya 4-0, Algeria 7-0 jumla inakuwa 17-1 waseme timu haikuwa na hela.

ccm acheni kutuonea hivi.
 
Kweli hatuko serious kama nchi
Dhahabu ipo
Tanzanite ipo
Gesi ipo
Kilimanjaro ipo
Almasi ipo
Ngorongoro ipo
Mikumi ipo
Bandari iPo....
Na Burundi nao wapo afcon wao wasemeje?
 
Hii nchi kila siku michango tu

Harusi
Send-off
Birthday za wadada
Yanga
Taifa stars

Daaaa huchomoki
.
FB_IMG_1560757179883.jpeg
 
Si wamejua kumbe watu mna hela,acha waendelee kutembeza bakuli
 
Back
Top Bottom