Kimsingi binafsi nilisimamia uchaguzi, jioni msimamizi ngazi ya kata akanipigia simu akauliza nipe matokeo, nikampa, akauliza mbona yako hivi nikamwambia wewe ulitakaje? Akasema mbona matokeo yako hivi nikamuuliza ulitaka ya namna gani, akasema kwani kwenye semina hukuwepo nikamwambia nilikuepo na nilielewa.
Kwa kweli yale mafundisho yaliyokuwa yanatolewa kwenye semina na mashinikizo ya wakurugenzi! Nilifika hatua nikakereka mno.
Baadae msimamizi akaniuliza na mawakala umewapa nakala ya haya matokeo, nikamwambia kila mmoja amepata, akaniambia jaza fomu za matokeo upya nikamwambia hapa nasubiri malipo tu ukiona hayafai endelea, kimsingi niliondoka tulipokuwa. Kiufupi haukuwa uchaguzi.