NGOSWE.120
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 219
- 233
Wapendwa wana JF,
Mimi na wenzangu kumi na moja (11) ambao ni Walimu kwa taaluma - tumesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazotukabili za kuto-mtii mwajiri wetu mahala pa kazi (msimamizi) wa kituo. Aidha kutokana na mashtaka hayo dhidi yetu, tume iliundwa kwa maagizo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ili tuhojiwe ili kubaini ukweli wa hizo tuhuma dhidi yetu.
Kwa pamoja, tulitoa ushirikiano wa kutosha tu kwa tume iliyoundwa ili haki iweze kutendeka. Tulihojiwa mtu mmoja mmoja sisi sote watuhumiwa 11, pia na mkuu wa kituo (mwajiri-msimamizi mahala pa kazi) naye alihojiwa.
Toka tume imemaliza kazi ya kutuhoji imepita miezi minne sasa, na mbaya zaidi kwa sasa tunalipwa nusu mashahara hadi hapo hukumu itakapotoka kulingana na ukweli utakaobainika.
Msaada wenu:-
1. Naomba mnisaidie kunielewesha - kisheria mtu akisimamishwa kazi na kuundiwa tume, ni muda gani yampasa asubiri hiyo hukumu? I mean uvumilivu wake unapaswa uwe wa muda gani?
2. Je kuna hatua gani stahiki naweza kuzichukua kisheria dhidi ya mshtaki (mwajiri) endapo kutakuwa na delay ya muda mrefu - lets' say ukapita mwaka without any feedback?
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu kwa ushauri mtakao utoa ili utusaidie kutetea haki zetu.
Ni Mimi mtoto wa Kabwela,
NGOSWE.120.