Nimesimamishwa kazi Serikalini, naomba msaada wa kisheria

Nimesimamishwa kazi Serikalini, naomba msaada wa kisheria

NGOSWE.120

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2011
Posts
219
Reaction score
233
Wapendwa wana JF,

Mimi na wenzangu kumi na moja (11) ambao ni Walimu kwa taaluma - tumesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazotukabili za kuto-mtii mwajiri wetu mahala pa kazi (msimamizi) wa kituo. Aidha kutokana na mashtaka hayo dhidi yetu, tume iliundwa kwa maagizo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ili tuhojiwe ili kubaini ukweli wa hizo tuhuma dhidi yetu.

Kwa pamoja, tulitoa ushirikiano wa kutosha tu kwa tume iliyoundwa ili haki iweze kutendeka. Tulihojiwa mtu mmoja mmoja sisi sote watuhumiwa 11, pia na mkuu wa kituo (mwajiri-msimamizi mahala pa kazi) naye alihojiwa.

Toka tume imemaliza kazi ya kutuhoji imepita miezi minne sasa, na mbaya zaidi kwa sasa tunalipwa nusu mashahara hadi hapo hukumu itakapotoka kulingana na ukweli utakaobainika.

Msaada wenu:-

1. Naomba mnisaidie kunielewesha - kisheria mtu akisimamishwa kazi na kuundiwa tume, ni muda gani yampasa asubiri hiyo hukumu? I mean uvumilivu wake unapaswa uwe wa muda gani?

2. Je kuna hatua gani stahiki naweza kuzichukua kisheria dhidi ya mshtaki (mwajiri) endapo kutakuwa na delay ya muda mrefu - lets' say ukapita mwaka without any feedback?

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu kwa ushauri mtakao utoa ili utusaidie kutetea haki zetu.

Ni Mimi mtoto wa Kabwela,

NGOSWE.120.
 
Kama kuna wanasheria wamsaidie. Hakuna profession isiyokuwa na consultation fee. Inategemeana mmeonana wapi. Bar. Jamiiforums. Ofisini. N.k
Uko sahihi mkuu. Halafu ni vyema kumpa hata muongozo tu then kama kuna mahitaji zaidi wawasiane
 
Wapendwa wana JF,

Mimi na wenzangu kumi na moja (11) ambao ni Walimu kwa taaluma - tumesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazotukabili za kuto-mtii mwajiri wetu mahala pa kazi (msimamizi) wa kituo. Aidha kutokana na mashtaka hayo dhidi yetu, tume iliundwa kwa maagizo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ili tuhojiwe ili kubaini ukweli wa hizo tuhuma dhidi yetu.

Kwa pamoja, tulitoa ushirikiano wa kutosha tu kwa tume iliyoundwa ili haki iweze kutendeka. Tulihojiwa mtu mmoja mmoja sisi sote watuhumiwa 11, pia na mkuu wa kituo (mwajiri-msimamizi mahala pa kazi) naye alihojiwa.

Toka tume imemaliza kazi ya kutuhoji imepita miezi minne sasa, na mbaya zaidi kwa sasa tunalipwa nusu mashahara hadi hapo hukumu itakapotoka kulingana na ukweli utakaobainika.

Msaada wenu:-

1. Naomba mnisaidie kunielewesha - kisheria mtu akisimamishwa kazi na kuundiwa tume, ni muda gani yampasa asubiri hiyo hukumu? I mean uvumilivu wake unapaswa uwe wa muda gani?

2. Je kuna hatua gani stahiki naweza kuzichukua kisheria dhidi ya mshtaki (mwajiri) endapo kutakuwa na delay ya muda mrefu - lets' say ukapita mwaka without any feedback?

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu kwa ushauri mtakao utoa ili utusaidie kutetea haki zetu.

Ni Mimi mtoto wa Kabwela,

NGOSWE.120.
Mkuu kabwela hukuwa wazi,,,,,,,,maagizo yapi hukutii je ulipewa barua mara ngapi hata hivyo wanasheria watashindwa kukushauri vema kwani uko ki-ujumla zaidi manaana unatakiwa kutoa maelezo ya kina ili kupata facts of case,,,,,,,
 
Ushauri wa kisheria una gharama mkuu

Ndio uroho wa wanasheria/mawakili ni money mongers kupita utu -shyster lawyers-. Ndio maana wanashindwa kwenda mahakamani kupinga kuendelea kwa bunge la katiba kwa vile wako preoccupied na hela, hela, hela, hela.........
 
Nenda idara ya kazi ukalalamike. Utapewa mwongozo nini cha kufanya.

Nilidhani mtu akiwa kwenye uchunguzi ama na kesi mahakamani bado anapata mshahara in full?
 
Pole mwl bila shaka yatakuwa mambo ya ubaya songea ttc nawashauri jichangechange mtafuta mwanasheria awasaidie!
 
Ngoswe, Mazoea yuko wapi? On a serious note, sheria ya sasa mtu ukisimamishwa kazi unalipwa full salary. Nenda mahakama ya usuluhishi (CMA) utapewa maelekezo stahiki. Pole jamaa yetu.
 
Pole sana mkuu,bila shaka watakuja.

Kwa sheria ya sasa hairuhusiwi kumpa mtu nusu mshahara
waliomsimamisha wamefanya hivyo kwa kutumia mazoea.

Mashauri ya kazi huwa yanapaswa kumalizwa mapema ili mhusika ajue hatima yake na kumwondolea msongo wa mawazo.
 
Naona umeridhika na nusu mshahara wakati unatakiwa ulipwe wote! Kuhusu muda wa kusimamishwa kazi, ukisoma sheria zote utagundua kuna mkanganyiko hivyo hakuna muda maalumu wa uchunguzi inategemea na nature ya kosa. Kuhusu hatua za kumchukulia mwajiri nadhani so long as utakuwa unapata full salary haina haja ya kumshtaki.
 
kwa mwajiriwa wa serikali miongozo yenu kuhusu ajira ipo Kwenye STANDING ORDERS huko ndiko walikopitia mpaka wakakusimamisha kazi kifupi hata huo muda umeandikwa huko......nahitaji consultation fee ili niendelee
 
nenda ofisi za CWT omba sheria za utumishi na standard order yake, kila kitu kimeelezwa humo.
 
kwa mwajiriwa wa serikali miongozo yenu kuhusu ajira ipo Kwenye STANDING ORDERS huko ndiko walikopitia mpaka wakakusimamisha kazi kifupi hata huo muda umeandikwa huko......nahitaji consultation fee ili niendelee

hahahahaha....!! you made my evening wonderful loh!
 
Nenda idara ya kazi ukalalamike. Utapewa mwongozo nini cha kufanya.

Nilidhani mtu akiwa kwenye uchunguzi ama na kesi mahakamani bado anapata mshahara in full?

Hapati full hata Zombe alikuwa anakula nusu akiwa mahabusu
 
mm navyo jua ,mtumishi wa uma akisimamishwa kazi atandelea kulipwa mshahara kamili...pia chama cha walimu kinachosimamia haki za wanachama wake,inabidi watafute wakili kwa gharam za chama kuwatetea ktk kesi yenu.ndivyo nijuavyo...ngoja tusubili wataalamu zaidi wachangie
 
Tulia tu watakuja kuwalipa pesa kubwa sana za malimbikizo yenu!!! Hakuna siku hata moja seerikali ya Magamba ilishinda kesi
 
Back
Top Bottom