KING ASSENGA
JF-Expert Member
- Oct 8, 2016
- 928
- 1,478
Ndugu zangu, jihadharini sana na marafiki wa karibu hasa kwenye maswala yanayohusu hela. Nimekutwa na utapeli wa aina ambayo yeyote mwenye rafiki anayemwamini hawezi kutoboa kwenye utapeli huo.
Huyu rafiki nilimkuta mwaka 2021 huko Iringa kwenye mazingira ya kilimo cha nyanya. Alikuwa muungwana kabisa, tena church boy kweli kweli. Tulikaa sehemu moja geto, tulikuwa watu watatu mpaka nilipohama Iringa, na sikuwahi kuona tabia yake mbovu yoyote.
Baada ya mwaka 2021, mimi niliondoka na kuendelea na harakati zangu Dar es Salaam mpaka leo hii. Baada ya muda mfupi, alidai alipoteza simu na hivyo kupoteza namba zangu, na mimi pia nilipoteza namba zake. Niliporudia namba zangu nilizokuwa natumia kabla ya kuikimbia Dar kwa ajili ya kukwepa depression na anguko zaidi la kibiashara, basi tulikutana tena Dar kwenye mwezi wa Januari, tarehe 4.
Aliniona kwenye biashara yangu ya magodoro na electronics mitaa ya wilaya ya Ubungo. Ilikuwa kama surprise. Baada ya kama wiki mbili, tukiwa karibu sana, aliniambia kuna fursa ya hela kama ningekuwa na mtaji wa milioni tano au zaidi anishirikishe hiyo fursa. Nikamjibu kwamba kwa sasa nipo vibaya sana, huwezi kuamini sina hata milioni moja kwenye akaunti ya benki ya nje ya biashara nilizonazo.
Basi akaniambia tarehe 21 nitafute milioni mbili na nusu tu ya kuanzia anishirikishe dili lenyewe. Nikamjibu sawa kwa alivyokuwa mpambanaji, niliamini kabisa itakuwa fursa maana uvaaji wake na kuwa na gari juu ndani ya miaka mitatu tu tuliyopotezana, bila shaka itakuwa ishu ya maana. Basi siku hiyo akaja na gari fresh, nikazama ndani. Walikuwa wawili, yeye na jamaa mmoja bonge kinoma, na akaenda hewani. Basi tukawa tunapiga stori, tukitoka nilipokuwa kufika mahali, rafiki yangu akaniambia umebeba hela hiyo milioni mbili na nusu. Nikamjibu ndio, basi akaanza kuongelea fursa yenyewe.
Wanaita utakatishaji fedha. Wanaambatanisha noti za elfu kumi original na karatasi flani nyeusi wanaita "nega" au "black money" ambazo wanadai hela hazitolewi nje zikiwa kamili. Zinakuja kama hayo makaratasi meusi na yanakuwa ni hela ila hayana baadhi ya nembo, na ukiziambatanisha hizo karatasi na noti ya elfu kumi na kumwagia chemical, zote zinakuwa nyeusi. Ukisafisha na chemical tofauti, zote zinakuwa noti kamili za elfu 10. Sijawahi kukutana na utapeli wa namna hii, ila nilipinga baada ya kuelezwa na kuoneshwa mfano.
Basi, baada ya kuweka msimamo sana, rafiki yangu ananijua vizuri nikishapinga jambo, basi akasimamisha gari sehemu flani. Alibaki kwenye gari akawa anapiga simu. Tayari hisia zangu zilinipeleka kuwa nipo kwenye hatari. Basi rafiki yangu akaniambia, "Unajua nini hapa? Ushajua siri ya kundi hatari na hawawezi kukuacha salama. Wewe toa hizo milioni mbili zifanyiwe utakatishaji upate hela zako nao wapate chao, alafu utaangalia namna ya kuja kujitoa bila tatizo zaidi. Unaona gari ya nyuma Alphard? Wapo watu watano na silaha, hivyo upo hatarini." Muda uleule kuna Alphard iliingia, plate namba ilifunikwa.
Nakuja kutuweka kati, basi nikaingia kwenye gari tukaenda hotel flani, wakafanya yao. Mwisho wakasingizia chemical imeganda, wakaniacha na yale makaratasi meusi, wakatoweka, na mimi sikukaa, nikatoweka zangu pia. Nikiwa na maumivu ya milioni mbili, lakini niliendelea kuwapigia simu kujifanya sijashtuka nishatapeliwa. Waliendelea kusema watarudi, ila hawakurudi na hawakujua nishatoka pale.
Basi baada ya kuendelea kumtafuta rafiki yangu, akanijulisha chemical ya kusafishia mzigo chini ya milioni 10 umekwisha, hivyo nijitahidi nipate 4M naye atafute 4M ili mzigo usafishwe. Basi nikawa mkali sana kwa kujifanya kwanini wamemwagia chemical kama kuwa hawana uhakika wa chemical ya kusafishia hela zingine. Wakijua sijashtuka, walichoniachia ni makaratasi meusi. Basi niliwatamanisha kupata hiyo 4M na wakaingia mkenge kwa akili sana. Nikamkamatisha rafiki yangu kwa polisi, akakaa ndani, wenzie walikimbia.
Alikuja kudhaminiwa baada ya wiki moja na kujaribu kuomba alipe ili kesi isiende mahakamani. Alidai hana uwezo kwani fedha zilibebwa na kundi, hivyo anaomba nimpe muda wa mwezi na atatoa ushirikiano wa kuwakamata wengine. Basi nikaacha kama lilivyo, nasubiri kulipwa au akishindwa, kesi iende mahakamani japokuwa sina uzoefu wa huko.
Mnalipi la kunishauri ili nipate fedha zangu? Na sina uzoefu na mambo ya sheria, hata polisi sina nako mazoea.