Nimetapeliwa hela na rafiki wa karibu

Nimetapeliwa hela na rafiki wa karibu

Walikufanyka black mail, hela anazo chukua gari lake si umesema ana gari
 
Ukipiga picha ya object yoyote kwa ajili ya kwenda public ondoa vidole.
 
Duh pole sana mkuu. Watu wanasema ukipotezana na mtu kwa zaidi ya miaka miwili ukija kukutana nae anakuwa sio Yule uliekuwa unamjua
Najutia sana kumwamini ni muda machache Kawa jambazi
 
Ndugu zangu, jihadharini sana na marafiki wa karibu hasa kwenye maswala yanayohusu hela. Nimekutwa na utapeli wa aina ambayo yeyote mwenye rafiki anayemwamini hawezi kutoboa kwenye utapeli huo.

Huyu rafiki nilimkuta mwaka 2021 huko Iringa kwenye mazingira ya kilimo cha nyanya. Alikuwa muungwana kabisa, tena church boy kweli kweli. Tulikaa sehemu moja geto, tulikuwa watu watatu mpaka nilipohama Iringa, na sikuwahi kuona tabia yake mbovu yoyote.

Baada ya mwaka 2021, mimi niliondoka na kuendelea na harakati zangu Dar es Salaam mpaka leo hii. Baada ya muda mfupi, alidai alipoteza simu na hivyo kupoteza namba zangu, na mimi pia nilipoteza namba zake. Niliporudia namba zangu nilizokuwa natumia kabla ya kuikimbia Dar kwa ajili ya kukwepa depression na anguko zaidi la kibiashara, basi tulikutana tena Dar kwenye mwezi wa Januari, tarehe 4.

Aliniona kwenye biashara yangu ya magodoro na electronics mitaa ya wilaya ya Ubungo. Ilikuwa kama surprise. Baada ya kama wiki mbili, tukiwa karibu sana, aliniambia kuna fursa ya hela kama ningekuwa na mtaji wa milioni tano au zaidi anishirikishe hiyo fursa. Nikamjibu kwamba kwa sasa nipo vibaya sana, huwezi kuamini sina hata milioni moja kwenye akaunti ya benki ya nje ya biashara nilizonazo.

Basi akaniambia tarehe 21 nitafute milioni mbili na nusu tu ya kuanzia anishirikishe dili lenyewe. Nikamjibu sawa kwa alivyokuwa mpambanaji, niliamini kabisa itakuwa fursa maana uvaaji wake na kuwa na gari juu ndani ya miaka mitatu tu tuliyopotezana, bila shaka itakuwa ishu ya maana. Basi siku hiyo akaja na gari fresh, nikazama ndani. Walikuwa wawili, yeye na jamaa mmoja bonge kinoma, na akaenda hewani. Basi tukawa tunapiga stori, tukitoka nilipokuwa kufika mahali, rafiki yangu akaniambia umebeba hela hiyo milioni mbili na nusu. Nikamjibu ndio, basi akaanza kuongelea fursa yenyewe.

Wanaita utakatishaji fedha. Wanaambatanisha noti za elfu kumi original na karatasi flani nyeusi wanaita "nega" au "black money" ambazo wanadai hela hazitolewi nje zikiwa kamili. Zinakuja kama hayo makaratasi meusi na yanakuwa ni hela ila hayana baadhi ya nembo, na ukiziambatanisha hizo karatasi na noti ya elfu kumi na kumwagia chemical, zote zinakuwa nyeusi. Ukisafisha na chemical tofauti, zote zinakuwa noti kamili za elfu 10. Sijawahi kukutana na utapeli wa namna hii, ila nilipinga baada ya kuelezwa na kuoneshwa mfano.

Basi, baada ya kuweka msimamo sana, rafiki yangu ananijua vizuri nikishapinga jambo, basi akasimamisha gari sehemu flani. Alibaki kwenye gari akawa anapiga simu. Tayari hisia zangu zilinipeleka kuwa nipo kwenye hatari. Basi rafiki yangu akaniambia, "Unajua nini hapa? Ushajua siri ya kundi hatari na hawawezi kukuacha salama. Wewe toa hizo milioni mbili zifanyiwe utakatishaji upate hela zako nao wapate chao, alafu utaangalia namna ya kuja kujitoa bila tatizo zaidi. Unaona gari ya nyuma Alphard? Wapo watu watano na silaha, hivyo upo hatarini." Muda uleule kuna Alphard iliingia, plate namba ilifunikwa.

Nakuja kutuweka kati, basi nikaingia kwenye gari tukaenda hotel flani, wakafanya yao. Mwisho wakasingizia chemical imeganda, wakaniacha na yale makaratasi meusi, wakatoweka, na mimi sikukaa, nikatoweka zangu pia. Nikiwa na maumivu ya milioni mbili, lakini niliendelea kuwapigia simu kujifanya sijashtuka nishatapeliwa. Waliendelea kusema watarudi, ila hawakurudi na hawakujua nishatoka pale.

Basi baada ya kuendelea kumtafuta rafiki yangu, akanijulisha chemical ya kusafishia mzigo chini ya milioni 10 umekwisha, hivyo nijitahidi nipate 4M naye atafute 4M ili mzigo usafishwe. Basi nikawa mkali sana kwa kujifanya kwanini wamemwagia chemical kama kuwa hawana uhakika wa chemical ya kusafishia hela zingine. Wakijua sijashtuka, walichoniachia ni makaratasi meusi. Basi niliwatamanisha kupata hiyo 4M na wakaingia mkenge kwa akili sana. Nikamkamatisha rafiki yangu kwa polisi, akakaa ndani, wenzie walikimbia.

Alikuja kudhaminiwa baada ya wiki moja na kujaribu kuomba alipe ili kesi isiende mahakamani. Alidai hana uwezo kwani fedha zilibebwa na kundi, hivyo anaomba nimpe muda wa mwezi na atatoa ushirikiano wa kuwakamata wengine. Basi nikaacha kama lilivyo, nasubiri kulipwa au akishindwa, kesi iende mahakamani japokuwa sina uzoefu wa huko.

Mnalipi la kunishauri ili nipate fedha zangu? Na sina uzoefu na mambo ya sheria, hata polisi sina nako mazoea.
mwaka juzi kuna mtu mmoja tumekuwa pamoja kwani nyumba yao utotoni inafuata kutoka ya kwetu, na tumekuwa watu wazima. alinikopa pesa akiahidi atairudisha ndani ya siku 10 kwa sababu alikuwa ameishiwa hela ya pango la duka lake na mwenye nyumba anataka ampe mtu mwingine kama hatalipa. kwa huruma nilimpa hela akalipa. huu ni mwaka wa 3 hata simu huwa hapigi. nilisubiri sikiu 10 nikasema ningoje mwezi, ukaisha, miezi 2, mara mi3 mara mwaka napiga simu hapokei (of course anakaa mkoa tofauti na mimi) nikanyamaza. hata salamu za chrismass wala mwakampya hajawahi kuniwish tangu achukue pesa zangu, hadi leo hii naongea amekata hadi mawasiliano. hivi ungekuwa wewe ungefanyaje? nilichofanya, nimekata mawasiliano naye pia kwa sababu sijamwelewa.

kwa sababu zamani na mimi nilikuwa na mambo ya kienyeji kwanza awali wazo lilinijia au alichukua ile hela yangu kwa lengo la kuipeleka kwa mganga apore baraka zangu, au aliambiwa nini na waganga achukue pesa kwangu ili azifanyie mazingara, au nini? na uzuri mimi silogeki, nina Yesu, nikajiuliza au alipeleka pesa zangu kwa mganga madawa yake yakaungua kwa sababu amekutana na Nguvu za Mungu aliye juu yangu? Imekuwaje hata simu hapigi, amekata mawasiliano yote miaka 3 sasa hata nikimtafuta hataki simu yangu kupokea? amekutana na nini? imebaki kitendawili hadi leo.

wazoefu wa haya mambo ya kukopesha hebu niambieni atakuwa na shida gani? ni mtoto wa mamangu mdogo hivyo nilishaamua kumsamehe hata pesa nikiamini labda alikuwa na shida, au hata kama aliamua kunidhulumu haina shida mbona Mungu anaendelea kunibariki napanda tu viwango kiuchumi sirudi nyuma? sasa kwa nini kakata mawasiliano?sijui.
 
Ogopa Sana fursa ambayo haikupi Nafasi ya kukaa kutafakari, Kufunyia uchunguzi na mwishowe Kufanya maamuzi.

We unafikilia huyo ange google kuhusu huo mchongo mtandaoni, angetapeliwa? Na Fursa yoyote kabla haijaingia Jitahidi wakati Wa kupata Elimu na kuielewa zaidi husiende ama Kutembea na Mtaji.
 
Hiyo mzee inaitwa WASH WASH, michezo hiyo ilifanyika sana Nigeria enzi hizo.

Unapewa makaratasi meusi, ukiyaosha kwa chemicals ule weusi unatoka inabaki noti kamili.

Michezo wanayofanya, wanazipaka noti chache za elfu kumi huo weusi, kisha mengine yanakua makaratasi tupu nayo wanayapaka rangi nyeusi, hivyo unakua mzigo mzigo mwingiiii kumbe unaeza kukuta hela halali haizidi elfu 50.

Ukija wewe wanachukua karatasi moja kwenye mfuko (ambayo ni noti halali,) wanamwagia chemicals ule weusi unatoka unaliona teni halisi.

Kisha wanakuonyesha mfuko uliojaa makaratasi na kukwambia zote ni noti, unachotakiwa kuwa nacho ni chemicals tu, kwa hiyo unajikuta unatoa hela wanakuuzia chemicals kisha haoooo.

Wewe sasa unajifungia ndani kuanza kuosha, unakuta umeachiwa shangazi kaja limejaa makaratasi basi unapagawa unajiona milionea tayari ukiosha unashangaa noti halali ni chache, mengine ni makaratasi tu

View: https://youtu.be/n7_jlp1_MLg?si=HvFTZNRhQyWoaDvY

Utapeli wa hivi kuna mjamaa aliufanya kwenye meli miaka ya nyuma huko, alitengeneza kimashine kinatoa hela, akawadanganya watu, hiyo mashine ina uwezo wa ku print hela kila baada ya lisaa inaprint noti moja ya dola mia.

Watu walivyoona wakapagawa, akawauzia kimashine, mpaka meli inatia nanga bado kina print

Mwisho ikawaje
 
mwaka juzi kuna mtu mmoja tumekuwa pamoja kwani nyumba yao utotoni inafuata kutoka ya kwetu, na tumekuwa watu wazima. alinikopa pesa akiahidi atairudisha ndani ya siku 10 kwa sababu alikuwa ameishiwa hela ya pango la duka lake na mwenye nyumba anataka ampe mtu mwingine kama hatalipa. kwa huruma nilimpa hela akalipa. huu ni mwaka wa 3 hata simu huwa hapigi. nilisubiri sikiu 10 nikasema ningoje mwezi, ukaisha, miezi 2, mara mi3 mara mwaka napiga simu hapokei (of course anakaa mkoa tofauti na mimi) nikanyamaza. hata salamu za chrismass wala mwakampya hajawahi kuniwish tangu achukue pesa zangu, hadi leo hii naongea amekata hadi mawasiliano. hivi ungekuwa wewe ungefanyaje? nilichofanya, nimekata mawasiliano naye pia kwa sababu sijamwelewa.

kwa sababu zamani na mimi nilikuwa na mambo ya kienyeji kwanza awali wazo lilinijia au alichukua ile hela yangu kwa lengo la kuipeleka kwa mganga apore baraka zangu, au aliambiwa nini na waganga achukue pesa kwangu ili azifanyie mazingara, au nini? na uzuri mimi silogeki, nina Yesu, nikajiuliza au alipeleka pesa zangu kwa mganga madawa yake yakaungua kwa sababu amekutana na Nguvu za Mungu aliye juu yangu? Imekuwaje hata simu hapigi, amekata mawasiliano yote miaka 3 sasa hata nikimtafuta hataki simu yangu kupokea? amekutana na nini? imebaki kitendawili hadi leo.

wazoefu wa haya mambo ya kukopesha hebu niambieni atakuwa na shida gani? ni mtoto wa mamangu mdogo hivyo nilishaamua kumsamehe hata pesa nikiamini labda alikuwa na shida, au hata kama aliamua kunidhulumu haina shida mbona Mungu anaendelea kunibariki napanda tu viwango kiuchumi sirudi nyuma? sasa kwa nini kakata mawasiliano?sijui.
🤣🤣🤣🤣🤣watu kama nyie mnatapeliwa kirahisi sana..
Kanywa biaa hela yote..
 
Pole Sana Ila umetapeliwa kijinga Sana .

Pia hiyo kesi uongea na polisi awake vitu vyake rehani mgawane hasara
 
Back
Top Bottom