TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
1. Bila kupepesa maneno, nikuambie tu kwamba wewe ni mhanga wa suala ambalo niliwahi kulileta humu kupitia uzi huu;Ni kweli sikupata muda wa kumchunguza,kwani baba yake ni mchungaji, niliamini Kwa Hilo!😭
Mtego wa kuoa/kuolewa na mtu wa dini yako unavyoweza kukucost maishani
Kuna baadhi ya madhehebu ya dini yameweka msimamo kwamba muumini haruhusiwi kuoa/olewa na mtu wa dhehebu lingine. Binafsi nimeona watu wakipata matatizo yafuatayo kutokana na msimamo huo; 1. Baadhi ya madhehebu hayo unakuta vijana (hasa wanaume) ni wachache. Kwahiyo linapokuja suala la kuolewa...
Mara nyingi watu hua mnajiaminisha kwamba kwavile huyu ni mkristo mwenzangu, tena mtoto wa mchungaji, basi huyu ni MALAIKA sina haja ya kumchunguza. Tena si ajabu ulikua na options zingine ukazikataa kisa sio "washarika" wenzio.
Big Mistake..!
2. Wanawake wengi mnaoolewa mkiwa MABIKIRA huwa mna matatizo. Moja, wengi mnadhani kwamba bikira ni kitu cha maana sana kwamba mwanaume akikukuta nacho baasi we umemaliza kila kitu. Ukweli ni kwamba bikra ni kitu kinatolewa ndani ya sekunde na kinasahaulika. Je, zaidi ya hiyo bikra, una nini? Bikra imeshatoka, haya una kipi sasa cha kumfanya huyo mwanaume aendelee kuwa na wewe? Unajua mapenzi? Una akili? Una kauli nzuri? Una heshima? Unajua kum-handle mwanaume? Kama vyote hivyo huna, si ajabu sasa kuona mwanaume anarudi kwa baby mama wake mwenye watoto wawili anakuacha hapo na bikra yako.
3. Kama ulivyosema, hapo upo kwenye mtego. Manake najua kabisa kutoka kwenye ndoa huthubutu unaogopa utaonekanaje na wakristo wenzio, kulipekela suala kanisani huthubutu manake unataka ndoa yenu iendelee kuonekana ya mfano. Huu unafki wakristo wengi sana unatutesa kutaka kuonekana ndoa yenu "imesimama" kumbe ndani hamna kitu!
Cha kukushauri hapo;
1. Usiongeze watoto! Huyo mwanaume anaweza kukuacha mda wowote, so hakikisha ukiachwa angalau uwe na mzigo mwepesi
2. Anza kujijenga wewe mwenyewe maana we ni singo maza mtarajiwa. Tafuta channel zako za kupata hela ili uweze kujitegemea
3. Anza kupunguza ukaribu na watu wa kanisani kwenu ikiwezekana hata kanisani usiende mara kwa mara. Au hama kanisa. Hii itakusaidia hata ukiachika usisengenywe sana. Watu wa kanisani wengi ni wanafki, wambea, wasengenyaji wakubwa!
4. Usiombe ushauri kwa watu wako wa karibu au wa kanisani. Wengi hamna cha maana watakachokushauri zaidi ya kukucheka na kukutangaza. Pambana kimya kimya