Nimetapeliwa kwenye ndoa ya Kikristo tena na mkristo mwenzangu

Kwa kujiangalia ww na uyo past participle tense wake nani mzuri?
 
Ok kwanza pole,pili ulikosea kwa nia njema ya kutomchunguza kwanza,anyway hiyo usijali,sasa ni qazi wewe peke yako hutaweza kupata suluhu na mumeo,nenda kwenye kanisa mlilofunga ndoa hiyo watawasaidia kutatua shida yenu
 
Expectation Vs Reality= Reality win sababu ndo uhalisia wa binadamu muda wote ameubwa kubadilika hautakiwi kuwa na expectation yoyote ile kwa mwanadamu, kingine badili FIKRA zako wala sio vitendo vya mme wako ndo vinavyokuumiza bali ni FIKRA unazotengeneza mwenyewe ndo zinazalisha hisia za maumivu una uchaguzi wa kuumia au kutokuumia kwa kubadilisha FIKRA zako, tatu kila tatizo linalotokea kwenye maisha lina maana nzuri ila hisia tunazoweka kwenye tatizo zinatufunga macho tusione mafunzo yaliyopo kwenye tatizo, sasa weka hisia pembeni alafu angalia kwenye tatizo ili umejifunza nini utaona kuna shule nzuri ipo nyuma ya tatizo, msisitizo weka hisia pembeni ndo utajifunza.
 
Nilinusurika kuingia katika ulaghai huo [emoji3][emoji3][emoji3], nikiwa Nina miaka 18 boss kamtuma mfanyakazi wa chini yake (msichana) kaniita kwake naingia nikamkuta yule baba akaniambia naomba ongea naye, nimeshaingia nikamwamkia akaitikia akaanza kumwaga sera anataka kunioa maana umri wake unamruhusu pia wazazi wanamsumbua sana, nikamuuliza dini vipi? Akajibu atabadili kunifuata nikamwambia sawa peleka barua haina shida, ikawa kila jioni naitwa Hana la maana zaidi ya kuwa anataka ndoa ifungwe haraka. Sikumwambia mtu yoyote maana Mimi huwa siamini mtu haraka ki hivyo.
Siku moja kuna dada alikuwa ananipenda sana.akaniambia nimsindikize sehemu anapeleka mzigo kwa kaka yake nikakubali sijui na yeye masikini hajui kitu ila nilikuwa najua anakaa maeneo yale. Binti na yeye ana ufunguo wa pale kila akifungua mlango umefungwa kwa ndani ikabidi agonge akafungua mwanamke wakasalimia tumekaribishwa mke kaja ghafla bila taarifa ahsante Mungu naangalia ukutani picha ya jamaa anamvisha.pete mkewe huyo niliyemuona[emoji3][emoji3] nilitulia kimya tukaacha mzigo tukaondoka njia nzima best anamsifia wifi yake, siku hiyo jioni hakuja. Siku ya pili kaja nikamsikiliza.sera.zake alipomaliza nikamwambia Jana saa tano nilikuja kwako na fulani bahati nzuri nikamkuta mkeo akanyamaza kimya, nikamwambia naomba iwe mwanzo na mwisho nikamwita huyo mwenyeji nikamwambia unaona malezi ninayolelewa naomba wewe na huyo boss wako msiniharibie maisha, mengine atakueleza huyo, nikatoka siku ya pili yule dada anamwombea msamaha boss wake nilichosema nitawashitaki kwa baba wakaona ohoo hapa tutakula "shaba" [emoji3][emoji3] hawakurudi tena. Kosa lako ulimuamini huyo laghai hukufanya uchunguzi na huenda ulijitoa mapema
Pole sana achana naye anza upya bahati nzuri una mtoto atakuliwaza.
 
Pole, Jiangalie wewe binafsi na mwanao. Kwasasa fanya mambo haya :
Jipende mwenyewe
Usimfuatilie
Onyesha kutokujali
 
Hisia kuziweka pembeni haiwezekani, sema azibadili hisia mbaya kuwa nzuri, kama anasema mwanaume ni malaya aanze kuifanya positive kwamba pengine amezidiwa maarifa na wajanja wa nje, au kwamba alipata tamaa tu ya mara moja, yaani kwa kifupi amuwazie mumewe in positive way mpaka brain ikariri hivyo uone mabadiliko atakayopata.


Mchawi wa kila jambo duniani ni emotions tu.
 
Mwanaume akitaka kukulaghai ana njia nyingi sana, ni bahati yako tu ila haimaanishi umemfanyia uchunguzi ukagundua, ni bahati imekutokea tu, ila Mwanamke kwa manaume hana ubavu. Tumejaaliwa zaidi ya njia 100 za kutapeli, wanawake mkubali tu nynyi ni viumbe dhaifu kwa mwanaume linapokuja swala la utapeli. Kusudi la dunia kila mwanaume atapeli mke au wake zake siku zipite afe maisha yaendelee
 
Mnaweza kuamini nimefunga harusi naye kanisani na kunihakikishia hajaoa kumbe ni mume wa mtu!

Ninaomba msaada wa kisheria wa kuachana naye
Katika kitu sikubali kwenye haya maisha nI unyonge, nakubaliana na wewe kwenye hili pambania haki yako ya talaka, huyo muhuni ameshakifanya mjinga kwa kipindi kirefu
 
Lakini mlalamikaji ni konki hasa kwenye siasa, hasa za CCM:

 
Kutapeliwa kimapenzi Hilo lipo Sana. Mimi me ila wakati namtafuta huyu mkewangu alikuwa wife material kwelikweli, heshima kama zote, yaani mvaa nguo za vitenge tu, tena mtu wa aibu aibu hata kuniangalia usoni alikuwa anaoma aibu. Basi mi kimono nikasema huyu ndio make sasa nimeokota dodo kwe mnazi hasa ukizingatia Mimi ni mpole Sana sio mtu wa starehe. Bwana bwana si nikaona sasa baada ya kuzaa mtoto 1 hakuna rangi niliacha kuniona, anakujibu kwa jeuri na dharau huku ananikodolea macho aibu Hana tena ndio hapo nikagundua nimeshataoeliwa kimapenzi. So inawezekana wewe ndio umebadilika Sana Una dharau
 
Sepa tu mdogo wangu kama huwezi kuvumilia. Mnapoambiwa ndoa ni utapeli muwe mnaelewa. Olewa/Oa at your own risk.
 
Na kwa mwanamke huwezi kuwa mjumbe wa CCM usiliwe uroda, kumbe tatizo limeanzia hapa. Jamaa aendelee na michepuko ya nje tu maisha yaendelee
 
Na kwa mwanamke huwezi kuwa mjumbe wa CCM usiliwe uroda, kumbe tatizo limeanzia hapa. Jamaa aendelee na michepuko ya nje tu maisha yaendelee
I don't believe binti kama alivyojiita, na mkristo kweli, awe na experiences hizo mpaka awe mjumbe wa vikao vya Dodoma vya CCM! Naona kama scam. Ni mwandishi mzuri sana na mzoefu wa hali ya juu.
 
Ulimfumania kitandani na huyo mama!?. Kama hujamfumania kwanini huhisi huzuni kwa yeye kukaa na mama watoto wake. Nafikiri unajipa presha zisizo na msingi, unawaza vitu ambavyo huna ushahidi navyo huko ni kujitesa wewe mwenyewe.

Kosa la yeye ni kutokukuambia kama aliwahi kuwa na watoto na mke. Na kama ukiendelea kuongea nae zaidi Ndo atazidi safari za kwa huyo mama.

Jambo nililojifunza kwa Hawa wanaume , ukigundua anachepuka na ukamwambia wengi wao kama alikuwa anafanya Siri basi sasa ataanza kudhihirisha kwakua Hana Cha kupoteza. Suluhu Huwa ni kukaa kimya au kuchukua maamuzi magumu bila kulalamika, hata ukilalamika huwa hawabadiliki ndo dharau na kebehi huzidi akijua huwezi kumfanya lolote.
 
Ungesikiliza ushauri wa KATAA NDOA usingeandika gazeti lote hili!
 
Jitahidi kujipa furaha.
Tafuta mtaji ujishughulishe.
 
Ungesikiliza ushauri wa KATAA NDOA usingeandika gazeti lote hili!
Tatizo watu wanaishi katika life circle kama ya Panzi. Yai, Lava, Pupa, Panzi kamili.

Wameshajiwekea kichwani nimalize chuo, nipate kazi, nioe/kuolewa, ninunue gari, nipate watoto, nifungue fremu, nijenge, nisomeshe, nisubiri kustaafu na kufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…