Nimetembea mikoa mingi Tanzania nimegundua kuwa Dodoma kuna nyoka wengi hatari kuliko mikoa yote Tanzania

Nachingwea ndio Wakoloni kipindi cha Ptoject ya Kilimo cha Karanga waliachia au tuseme kufuga nyoka na kuwaachia Mashambani ili wawale Panya...kwaiyo Nyoka Nachingwea ni wengi
Hiyo issue ndio imechangia pakubwa Wilaya za Mpwapwa/Kongwa na Urambo kuwa na majoka mengi baada ya project ya karanga kuanzishwa na kutumia nyoka Kama Kinga dhidi ya panya waharibifu kwa zao la karanga

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Natamani nijue nyoka wenyewe na tiba zake maana soon nitakuwa mtu wa msituni
Nyoka wapo wa aina nyingi sana na sio rahisi kuwaona wote kwani nyoka ni werevu na wanajua kujificha sana. Tiba za sumu za nyoka zipo Hospitali na hutegemea ni aina gani ya nyoka aliyekung'ata. Nyoka wote duniani unaweza kuwaweka katika mafungu manne(4) kwa mujibu wa sumu zao:
1. Nyoka wenye sumu inayoshambulia mishipa ya fahamu i.e.Neurotoxic venom
2. Nyoka wenye sumu inayoshambulia misuli ya mwili i.e. myotoxine venom
3. Nyoka wenye sumu inayoshambulia damu i.e.Haemotoxic venom.
4. Nyoka wasio na sumu kabisa i.e. Non poisonous (toxic) snakes.
Sumu ya nyoka hukaa(huhifadhiwa) kichwani pake ndani ya vijimfuko vidogo na hutoka kupitia meno yake mawili marefu upande wa juu-mbele wa mdomo wake. Hii ina maana sehemu ya mwili wa nyoka iliyobaki ukiondoa kichwa sio sumu na yaweza kuliwa bila shida i.e.ni chakula. Vp broo, ungependa ujaribu ck moja? Mie nilishakula cobra na ninadunda hadi leo sikudhurika hata kidogo.
Ni kweli kuna tiba za asili/mitishamba lakini ck hizi udanganyifu/uongo/utapeli umekuwa ni mwingi mno kiasi kwamba you don't have to risk your life
 
Chunya ,nilikutana na koboko,atakua alinichukilia poa tu akunikimbiza maana nisengemshinda,ila mwenda niliokimbia ,ile spidi nikagundua binadamu tuna uwezo wa kupaa ila tunajiendekeza tu.
Aisee mazingira niliyopo na hii comment yako nimejikuta nageuka kituko mbele za watu nimecheka sana 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Umetafuta sababu za kutaka kurudi Dar baada ya magufuli kuwakurupusha Dar umekosa ,sasa umekuja na gia ya nyoka wengi,endelea tu kula nyama mnadani mkuu,hapo ndio umefika subiri mpaka ukistaafu ndio utaondoka...
 
Huenda kutokana na uwepo Wao mkubwa huko na Kuwadhuru Watu wa huko umepelekea wengi Wao ( Watu kutoka Mkoa wa Dodoma ) kuwa uwezo mdogo wa Kufikiri nikimaanisha Akili tofauti na Makabila mengine mengi nchini Tanzania yenye Akili sana kama ya Wazanaki ( Mara ) na Wayao ( Mtwara ) ambako ndiko Chimbuko Tukuka la GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE Mimi.
 
Wamakonde wamegoma kula nyoka
 
Nataka nizijue tiba asili kulingana na aina na nyoka husika
Mkuu; kwanza kabisa NUKUONYE(WARNING) kila kabila au kila utakopoenda au kufika, utakuta wapo watu wanaodai wanajua au kuwajua "wazee" wanaofahamu Tiba za Nyoka esp. wale wanaopatikana eneo hilo. Majina ya nyoka waliopo i.e. wale nyoka wanao wafahamu watakutajia kwa kilugha chao. Miti itumikayo kama tiba kwa sumu ya nyoka watakutajia kwa kilugha chao. Ili uweze kwenda kui-identify hiyo miti ni lazima ufuatane na huyo "mtaalam" kwani miti inafanana.
Ukizingatia kwamba ww ni " Binadamu-Mpiganaji" leo uko hapo, kesho uko kule n.k. Sio miti yote hususan ile "miti-dawa" hupatikana kila mahali. Kwa mantiki hiyo utauchosha sana ubongo wako.
Kama ni kutaja au kujua aina ya "miti dawa" itumikayo kama matibabu kwa mtu aliyeng'atwa na nyoka waweza kuipata kwenye Google hata picha za miti hiyo.
Lakini bila kuiona Physically ni vigumu sana kusema umeijua kwa uhakika.
 
Ngoja niangalie kama ubongo wangu utakubali huu ukweli na kusitisha maharakati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…