Nimetembea mikoa mingi Tanzania nimegundua kuwa Dodoma kuna nyoka wengi hatari kuliko mikoa yote Tanzania

Nimetembea mikoa mingi Tanzania nimegundua kuwa Dodoma kuna nyoka wengi hatari kuliko mikoa yote Tanzania

Dodoma kuna ukoma
Dodoma kuna nusu jangwa
Dodoma kuna gereza la kunyongea
Dodoma ndio makao makuu ya wehu
Dodoma ndio kuna upofu usababishwao Na trachoma
Dodoma kuna Hali mbaya sana ya hewa
Dodoma no makao makuu ya majoka
Hebu ona hii:
Dodoma ni mahali penye fursa nyingi za kiuchumi e.g. Maeneo makubwa ya kilimo/mifugo/samaki, madini na uwekezaji mwingine.
Dodoma ardhi yake na hali ya hewa vinaruhusu watu kutoingia gharama kubwa kuanzisha makazi ya kudumu
Dodoma maeneo yote yanafikika kirahisi na ni tambarare hakuna milima mingi
Dodoma maji ya chini ya ardhi yapo juu tofauti na maeneo mengine ambayo ili uweze kuyavuna maji hayo unakwenda kina (vertical depth) mita 120+
Dodoma ni rahisi zaidi kupata malighafi za ujenzi e.g. mchanga, kokoto, kifusi au tofali za kuchoma
Dodoma ina nguvu-kazi kubwa (untapped cheap labour) ambayo haijatumika kikamilifu
Dodoma inafikika haraka kwa baraba(Magari na Treni ya kisasa),Anga(Ndege)
Dodoma inazo huduma muhimu za kijamii Hospitali kubwa, Vyuo vya elimu ya juu, Mawasiliano kwa simu na mitandao mingine yote, vituo au huduma za Usalama wa raia(Polisi, JWTZ, Zima moto, n.k.)
Dodoma huduma za kiroho zipo zinapatikana kwa kwa wingi -Nyumba za Ibada (Misikiti, Makanisa, Mahekalu n.k.)
Dodoma ndo makao makuu Rasmi ya Serikali Tz.
 
Habari za mida hii ndugu wananchi, kifupi mimi siyo mtaalamu wa wanyama ila ni mpenzi na mfuatiliaji wa masuala ya wanyama na makala zao kupitia TV na mitandao.

Nimetembea mikoa karibu yote Tanzania ila nimegundua kuwa dodoma ndo mkoa wenye NYOKA wengi hatari kuliko mikoa yote Tanzania. Pia nimekutana na watu wengine ambao pia wanadai dodoma hakufai, kisa wingi wa NYOKA.

Hii ni orodha ya nyoka ''HATARI" niliowaona kwa macho yangu katika ardhi ya Dodoma.

Koboko (black mamba)
Swila wa msituni (forest cobra)
Nyoka kijiti (twig snake)
Boomslang
Kifutu (puff adder)
Kifutu magamba (saw scalled viper)
Swila mweusi (spitting cobra)

THIBITISHENI AU BATILISHENI HILI KUHUSU DODOMA.
Chai
 
Na dar kuna chawa wengi
 
Still laana IPO.
 
La hasha. Hilo la uwepo wa nyoka wengi ni kweli. Proof: Baadhi ya nyoka walikuwa Imported kutoka Malawi (esp.Puff adder) kipindi cha The Great Groundnut Project na project ilipofeli hao nyoka hawakuondolewa waliachwa na kuzagaa hovyo na hivyo walizaliana na tangu kipindi hicho hadi sasa wamesambaa sana. Wahusika hawakufanya EIA (Environmental Impact Assessment) kabla ya kuanzisha Mradi huo. Wao waliona tu manufaa ya karanga na kuagiza nyoka ili kudhibiti wanyama(Panya) waharibifu.
 
Habari za mida hii ndugu wananchi, kifupi mimi siyo mtaalamu wa wanyama ila ni mpenzi na mfuatiliaji wa masuala ya wanyama na makala zao kupitia TV na mitandao.

Nimetembea mikoa karibu yote Tanzania ila nimegundua kuwa dodoma ndo mkoa wenye NYOKA wengi hatari kuliko mikoa yote Tanzania. Pia nimekutana na watu wengine ambao pia wanadai dodoma hakufai, kisa wingi wa NYOKA.

Hii ni orodha ya nyoka ''HATARI" niliowaona kwa macho yangu katika ardhi ya Dodoma.

Koboko (black mamba)
Swila wa msituni (forest cobra)
Nyoka kijiti (twig snake)
Boomslang
Kifutu (puff adder)
Kifutu magamba (saw scalled viper)
Swila mweusi (spitting cobra)

THIBITISHENI AU BATILISHENI HILI KUHUSU DODOMA.
Hauhitaji kuwa na nyoka wengi, you only need to have black mamba, naona unajaribu kuupoka ufalme wa Tabora kwenye hilo
 
Tatizo hutaki kuambiwa kweli, nitajie mkoa gani wenye laana kama ilizonazo Dodoma?
Mkuu, Sina Orodha lakini na ww ukubali kwamba Dodoma haijalaaniwa kwani kuna maeneo mengine hali sio nzuri e.g. maeneo yenye Matukio mengi ya watu kujinyonga, Watu kukumbwa na mafuriko, Matetemeko ya ardhi, kupigwa radi, milipuko ya moto kichaa, yapo pia maeneo yenye kiwango cha juu zaidi cha kesi za ugonjwa wa malaria, maeneo yenye visa vingi vya ukorofi e.g. ujambazi, wizi wa kutumia nguvu e.g. panya rodi, Utapeli; yapo maeneo au Mikoa inayovuma zaidi kwa visa vya madawa ya kulevya, ushoga, njaa(Uhaba wa chakula), magonjwa yasiyoambukiza e.g. pressure na kisukari n.k. Hayo yote ni majanga.
Kwa hoja zako za Dodoma, e.g Hospitali ya wehu hilo ni maamuzi tu kwani hospitali hiyo yaweza kuhamishwa au ikaanzishwa nyingine mkoa mwingine. Hapo utasema laana imekuwa duplicated? au imehamishwa?
Kwamba Dom ndipo penye gereza la kunyongea watu. Hiyo ni infrastructure tu yaweza kufungwa na ikaanzishwa nyingine mahali pengine. Ina mana laana itakuwa imefungwa kwa Dom na Kuhamishiwa mahali pengine? Zinagtia Laana haihamishiki- iko pale pale.
Kwamba Dom kuna Ukoma. Ukoma ni ugonjwa wa zamani na kwa Taarifa yako Siku hizi UKOMA (leprosy)UNATIBIKA. Ni tofauti na Laana ambayo kwa hali ya kawaida huwa haina tiba.
Kuhusu ugonjwa wa Upofu mto(Trachoma); Ugonjwa huo unatibika kabisa na kuna chanjo yake. Ni ww tu kuwa makini na kuzingatia maelekezo ya Wataalam.
Kwa habari ya Hali mbaya ya hewa, huo huwa ni mtazamo wa mtu binafsi kwani huko nako Dom si kuna watu wanaishi? Hilo ni suala la wewe kuyamanipulate mazingira yako ili yaendane na jinsi ww unataka kuishi. e.g. Kilimo cha umwagiliaji, upandaji wa miti na mazao yanayostahimili ukame au mazao yanayo stahimili mvua kidogo/mifugo inayovunwa ndoni ya muda mfupi/mapema n.k.
 
Mkuu, Sina Orodha lakini na ww ukubali kwamba Dodoma haijalaaniwa kwani kuna maeneo mengine hali sio nzuri e.g. maeneo yenye Matukio mengi ya watu kujinyonga, Watu kukumbwa na mafuriko, Matetemeko ya ardhi, kupigwa radi, milipuko ya moto kichaa, yapo pia maeneo yenye kiwango cha juu zaidi cha kesi za ugonjwa wa malaria, maeneo yenye visa vingi vya ukorofi e.g. ujambazi, wizi wa kutumia nguvu e.g. panya rodi, Utapeli; yapo maeneo au Mikoa inayovuma zaidi kwa visa vya madawa ya kulevya, ushoga, njaa(Uhaba wa chakula), magonjwa yasiyoambukiza e.g. pressure na kisukari n.k. Hayo yote ni majanga.
Kwa hoja zako za Dodoma, e.g Hospitali ya wehu hilo ni maamuzi tu kwani hospitali hiyo yaweza kuhamishwa au ikaanzishwa nyingine mkoa mwingi.Hapo utasema laana imekuwa duplicated?
Kwamba Dom ndipo penye gereza la kunyongea. Hiyo ni infrastructure tu yaweza kufungwa na ikaanzishwa nyingine mahali pengine. Ina mana laana itakuwa imefungwa kwa dom na Kuhamishiwa mahali pengine? Zinagtia Laana haihamishiki- iko pale pale.
Kwamba Dom kuna Ukoma. Ukoma ni ugonjwa wa zamani na kwa Taarifa yako UKOMA (leprosy)UNATIBIKA. Ni tofauti na Laana huwa haina tiba.
Kuhusu ugonjwa wa Upofu mto; Ugonjwa huo unatibika kabisa na kuna chanjo yake. Ni ww tu kuwa makini na kuzingatia maelekezo ya Wataalam.
Kwa habari ya Hali mbaya ya hewa huo huwa ni mtazamo wa mtu binafsi kwani huko nako Dom si kuna watu wanaishi? Hilo ni suala la wewe kuyamanipulate mazingira yako ili yaendane na jinsi ww unataka kuishi. e.g. Kilimo cha umwagiliaji, upandaji wa miti na mazao yanayostahimili ukame.n.k.
Identify ya Dodoma ni kuwa omba omba.
Ukiwa omba omba utaambiwa wewe ni Mgogo (mtu wa Dodoma).
Dodoma Kuna umasikini wa kutupwa.
Kuna baa la njaa.
Hakuna mvua .
Yaani Dodoma kwakweli sijui watu Huwa wanaishia vip Dodoma.
Serikali isingeweka Bunge.
Wizara zote, Ikulu na vyuo mbalimbali pangekuwaje kama ilivo Mwanza, Mbeya , Iringa , Manyara .
Dodoma laana ipo kubwa tu
 
Hapana sio laana - labda tuziite ni changamoto au hizo ni Kero kwa sababu zote zilizotajwa hapo juu zinaweza kutatuliwa au kupata ufumbuzi wake. Ni suala la muda tu.
Inakuwaje tunasema eti Dodoma hakuna mvua? Tunastawishaje zile zabibu? Mazao kama ufuta, uwele , alizeti n.k. mbona yanasitawi. Me naona tatizo lipo kwenye akili zetu kwamba mvua ni ile ya Kiwango cha juu hadi wastani e.g.Dodoma ina wastani wa milimita 610 au inchi 24 za mvua kwa mwaka, nyingi zaidi hutokea wakati wa msimu wa mvua kati ya Desemba na Aprili.
Chanzo: nimenukuu kutoka mamlaka TMA 2023.)
Umaskini umeenea nchi nzima. Umaskini (Poverty) ni National Agenda. Ni suala mtambuka. Mikoa tunazidiana viwango tu.
Hoja ya kwamba watu wanaishi vp Dodoma, inakubidi ufanye research utagundua mengi.Kwani wamekataliwa kuhama? Mbona wanaingia wahamiaji tena kwa wingi? Usiangalie kipimo kimoja tu cha uwepo wa wingi wa fedha ktk mzunguko. Angalia na mengine.
Unasemaje kwamba Dodoma kuna baa la njaa ilhali Miji mikubwa e.g. Dar. wanapokea mazao kutoka Dodoma? Shida ni pale mtu anafikiri chakula ni Ugali wa mahindi dona au sembe au wali na kusahau kwamba hata mtama na uwele, maboga, matikiti maji, mihogo na viazi, mbaazi na ufuta pia ni chakula. Wanyama kama ng'ombe, mbuzi na kondoo na kuku wa kienyeji wanastawi - hiyo njaa inapita wapi? Watu wanakimbilia Dom kupata zabibu halafu wanasema kuna njaa :KEKBye: Zipo mboga zilizokaushwa na zinasafirishwa nje ya mkoa kwenda kwa wenye njaa. Hebu jaribu just for fun utembelee sehemu inaitwa Kiboriani kule Mpwapwa. Hata ndizi na miwa vinasitawi; nyie mnatakaje? Angalieni msije kuwa mnamKufuru Mungu.
 
Hali ya hewa na viumbe wengine waliopo eneo husika ni factor kubwa Sana kustawisha nyoka. Mikoa inatofautiana Hali ya hewa
Na hApa tunazungumzia nyoka hatari,sio tu nyoka kwa ujumla.
Kama ni kuzungumzia nyoka wakali labda yaweza kuwa kweli,

Lakini kama ni wingi wa nyoka nadhani nachingwea inaongoza jaribu kufika huko ujionee,

Kule miaka ya nyuma kidogo paliletwa mladi wa nyoka kutoka nje ili waje kupambana na panya ile mijoka ikala panya ikanenepeana na kuzaliana kwa wingi mleta mladi alipotaka kuwaondoa alishindwa na kuwaacha,

Sasa walishazaliana na kusambaa Lindi yote na kuingia maeneo ya Mtwara hususani Masasi, Newala na Tandahimba.

Hivyo kwa wingi wa nyoka nachingwea yaweza shikilia nafasi
 
Huko ni jangwani kumbuka...hivyo wadudu wa hatari jangwani ndio nyumbani kwao
Mkuu; tofautisha kati ya semiarid land na desert. Dodoma inakuitwa semi arid au arid land na sio Jangwa (Desert). Dodoma uoto wa asili umeenea kila mahali nyasi, miti(Cassia spp) na mibuyu. Jangwani ni mchanga mtupu hakuna kinachoota. Hakuna mvua inayoweza kustawisha chochote- inanyesha kidogo sana na kwa mtawanyiko mbovu - walau mara moja kwa mwaka na kwa muda mfupi (siku chache) au hakuna kabisa au ni baada ya miaka kadhaa.
Nanukuu: "Mvua. Majangwa hupata takriban milimita 250 (inchi 10) za mvua kwa mwaka —kiwango cha chini zaidi cha mvua kati ya viumbe vyote).
Ukigoogle utapata hiyo.
 
Habari za mida hii ndugu wananchi, kifupi mimi siyo mtaalamu wa wanyama ila ni mpenzi na mfuatiliaji wa masuala ya wanyama na makala zao kupitia TV na mitandao.

Nimetembea mikoa karibu yote Tanzania ila nimegundua kuwa dodoma ndo mkoa wenye NYOKA wengi hatari kuliko mikoa yote Tanzania. Pia nimekutana na watu wengine ambao pia wanadai dodoma hakufai, kisa wingi wa NYOKA.

Hii ni orodha ya nyoka ''HATARI" niliowaona kwa macho yangu katika ardhi ya Dodoma.

Koboko (black mamba)
Swila wa msituni (forest cobra)
Nyoka kijiti (twig snake)
Boomslang
Kifutu (puff adder)
Kifutu magamba (saw scalled viper)
Swila mweusi (spitting cobra)

THIBITISHENI AU BATILISHENI HILI KUHUSU DODOMA.
Ni kweli Dodoma kuna nyoka hatari ila sidhani kama wanaizidi Tabora haswa Kigwa. Tabora kuna nyoka utafikiri ndiyo chimbuko lao liko kule
 
Habari za mida hii ndugu wananchi, kifupi mimi siyo mtaalamu wa wanyama ila ni mpenzi na mfuatiliaji wa masuala ya wanyama na makala zao kupitia TV na mitandao.

Nimetembea mikoa karibu yote Tanzania ila nimegundua kuwa dodoma ndo mkoa wenye NYOKA wengi hatari kuliko mikoa yote Tanzania. Pia nimekutana na watu wengine ambao pia wanadai dodoma hakufai, kisa wingi wa NYOKA.

Hii ni orodha ya nyoka ''HATARI" niliowaona kwa macho yangu katika ardhi ya Dodoma.

Koboko (black mamba)
Swila wa msituni (forest cobra)
Nyoka kijiti (twig snake)
Boomslang
Kifutu (puff adder)
Kifutu magamba (saw scalled viper)
Swila mweusi (spitting cobra)

THIBITISHENI AU BATILISHENI HILI KUHUSU DODOMA.
Chunya kuna koboko wa kutusha
 
Back
Top Bottom