Nimetembea na mchumba wa Marehemu binamu yangu

Mnafanya mambo marahisi… siku hizi jamii imeelimika huoni itakuwa ni hatari
Basi mkuu achana nae, Mungu hapendi wewe kumla mchumba wa marehemu binamu, tafuta mwingine...naona kichwa yako nzito nzito tu.
 
Kabla ya yote nini kilimuua binamu yako? Ukishajua hakuna dhambi kumrithi huyo bibie
 
binadamu nyama ya hamu,kama unaoa embu oa usituchoshe huko
 
Hapo laana ipo kwasababu ya uzinzi na si sababu zingine.
Huyo binamu ameshakufa, hata hivyo hawajafunga ndoa.
Hata kama wangefunga ndoa na mmoja kufa hapo hakuna kifungo tena.
Vijana acheni uzinzi, mnalaani maisha yenu wenyewe
 
Yeah,kwakuwa ni marehemu inaweza sound vibaya,wakafikiria labda ulikuwa unamzunguka marehemu.
Inaweza kuleta minong'ono au lawama pia.
Busara ni kuachana naye tu
Lakini hakuna laana yoyote ni vile jamii itakuchukulia hasa ndugu zake na marehemu.
 
Hiyo mbona hakuna kipingamizi kabisa, watu wanaoa binamu zao sembuse huyo mchumba wa binamu tena binamu mwenyewe ameshatangulia mbele ya haki. Chukua ngoma hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…