Nimetengeneza 15,632,000/= kwenye betting ndani ya miezi minne

, Sema ina changamoto zifuatazo.
1) Low yield or High capital required.
Hapa unaona kua return per day ni approximately 5%. Kwamba ukiweka stake ya laki 1 utapata tuseme 5,000/= faida. Ili upate zaidi inabid uwe na mtaji mkubwa. 1mil stake utapata faida 50,000/=

2) Transaction Cost. Sijajua ku deposit hela kwenye kampuni yako utatumia njia gani isiyo na makato. Ki bongo bongo (default) sio makato kivile. Hapa pia namaanisha tuseme umecheza kampuni 3 tofauti na ulioshinda ni kampuni "B". Sasa ukitaka kubet tena kesho yake na stake kubwa unataka uiweke kampuni "A" itabidi uhamishe hamishe hapo.

3) Kodi. Kama yield ni ndogo basi pale inapokua taxed ndio inazidi kupungua zaidi. Makampuni ya nje hayana kodi, lakini wengi tumezoea kubeti kwenye haya yaliyoko hapa nchini. Na yenye kodi yaweza kua na odds ndogo.

4) Kupata Maximum odds. Ile website uliyoweka inatoa suggestions ya kampuni za nje, je odds zilizoonyeshwa pale zaweza kupatikana kwenye local companies na zika maximize profit?

5) Kubadilika kwa odds. Kuna makampuni yamekaa kitapeli. Odds unayoiona pale eti ukiwekea bet ndo wanakuambia imebadilika.

All in all ni strategy nzuri kwa wenye mtaji, coz at any point you must win
 
Mkuu nashukuru tangu nianze kufuata maelekezo yako mwelekeo nauona. Ubarikiwe sana.
 
Yap Odds Kubadilika ndio issue kubwa kuliko zote;

Pili kuna kitu kinaitwa maximum payout kwenye single bet (hapo hata wenye mtaji mkubwa kuna limit, pia betting firms nyingine zinaweka odds kubwa ili kubalance vitabu (hedge) kwahio huenda ukaweka dau kubwa ukaambiwa labda robo ndio inaweza kuwa processes

Tatu credit cards kutoa na kuweka ni gharama (processing fees); ingawa hapa unaweza kutumia kitu kinaitwa E-Wallet.... kupunguza processing deposit fees...unaweza kutumia Skrill au Neteller yaani unaweza kuhamisha funds from kampuni A mpaka B mpaka C kwa urahisi bila kuwa na funds kwenye kila Kampuni...

All in all nothing is without risks and disadvantages hii nilitoa tu kama mfano baada ya Wall street kusema hakuna kitu kama hicho na kutangaza Dau la 100K nikionyesha something ambayo sijaona mpaka sasa.... well..., that's life.....
 
Practically,

Wewe ushawahi kujaribu hii kitu?
 
Practically,

Wewe ushawahi kujaribu hii kitu?
No I don't really gamble ila ni mdau wa kutafuta loopholes na opportunities thats my hobbie ...; I don't do it cause I think its not emotionally worth it.....

Ila Arbs zipo na kama nilivyosema loopholes zinaweza kupatikana kwenye mchanganyiko wa Over / Under Goals au Asian Handicaps
 
No goal labda kama anacheza in play betting dakika ya 80 huko, no goal kuanzia game inaanza?

kaka anaweza akacheza first half au moja kwa moja ila anachezaga live betting na anacheza ikifika dakika ya 30 anaturbo kama mambo yanaenda poa, wewe mdau wa meridian unajua turbo ni nini
 
Kuna jambo hujui. Ukibet 500,000 ktika bet bet zako ukabahatisha ukapata 2m ukawa na m2.5, ukiendelea kubet na 500,000 hata ikiliwa hujapoteza bado. utahesabika umepoteza pale ambapo 500,000 italiwa na 2m uliyotengeneza ikaliwa halafu ukalazimika kuchukua pesa mfukoni na kucheza. Kama una bahati na ni mchambuzi mzuri unaweza kubet na hela ya mwenye kampuni maisha yako yote ya betting. Hapa namaanisha m2 uliyoshinda unatoa laki tano yako nyingine yote inayobaki unacheza nayo, ikipotea huwezi sema nimeliwa maana haikua yako bali uliishinda.
 
Unaweza bet single bet si lazima mkeka. mm sibet sana ila nipo na watu wanabet mkuu. mtu anabet single match tu na anaweka ela kweli. akipata anabet na pesa aliyoshinda sasa hapo anapotezaje? Kwenye kubet naona kuna hadi corner zitakuwa ngapi, nani atapewa kadi, magoli yatakuwa chini ya matatu au la, red cards etc. sasa kuna watu wanazijua timu na wanawajua wachezaji wanahisi kabisa mechi ya leo ilivyo na presha huyu beki lazima apate njano anabet. Sasa hesabu za magazijuto huyo ukimweleza hawezi kukuelewa
 
kwahio hiyo 2.5m ikiliwa unaacha au unajikopesha tena laki 5, au tusema umepata good trend ikafika milioni 100 baada ya miaka mitano baadae ukapata bad patch ikaliwa mpaka kubaki milioni moja ingawa moneywise bado upo juu hio time wastage ya kuzalisha 1m kwa miaka mitano ingawa sio financially waste what about opportunity cost na time wastage ?

As said before in the end the house always win.., kama bado upo juu fahamu kwamba soon or later the shit will hit the fan...
 
Sasa boss kama ameanza na laki tano halafu ikapanda hadi 50m halafu ikashuka mpaka 15m hata hadi 400k au 200k akaacha anakuwa amepotezaje? Akibakiwa na 200k si atakuwa amepoteza 300k kwa cash flow ya almost 50m? hiyo cash flow inayompitia si inamaana? Si faida kwake? Watu wanatamani wapate angalau mzunguko wa fedha hata kama si zao ziwe zinawapitia tu wacheze nazo kidogo ziondoke wewe unasema ni wastage of time? Kuna vimatumizi vidogo vidogo vingapi unasolve kwa hiyo pesa kupita kwenye mzunguko wako wa fedha? Wewe hujawahi kukopa pesa ili ukalipe pesa halafu ulipolipa ukakopa tena ili urudishe pesa mambo yaende? Kuna wakati mtu unahitaji hata hiyo cash flow tu ikupitie hata kama ni ya interest ila huioni, sembuse huyu aliyeshinda?
 
Na wanaotengeneza odds wanajua mpira sio kidogo na wanafanya research za maana na ukiona odds zina value mara nyingi punters (wanaobet ni wengi kuliko uhalisia) kwahio na kama unapata hizi value bets mara nyingi unayekula pesa yake sio bookies ni punters wenzako walioliwa; na hata ujue mpira vipi kuna unknowns zinaweza kutokea, nikupe mfano ukirusha shilingi mara kumi kuna uwezekano wa asilimia 50 kichwa kitatokea mara tano.., sasa kwenye odds badala ya kupewa 50% unapewa kama 40 % Kichwa na 40% Tails.., hapo kuna 20 percent ambayo haipo kwenye mchanganuo.., ndio maana nikasema in the long run na utaalamu wote utashindwa sababu wote mnajua game, na bahati mbaya hutokea anachokushinda mwenzako ni anakupa a RAW DEAL...., unless kama unabet kama leisure au mara chache siku ukiona value Bet labda mpinzani wa Brazil kapewa odds nyingi kutokana na jina la Brazil na punters wengi watabet Brazil sababu ya jina hence kuna value ambayo ipo hapo, hata hivyo huwezi kufanya week in week out....
 
kama amebet akapata faida halafu hiyo faida akaitumia kubet akawa anapoteza na kupata hana alichopoteza. Cash Flow ni muhimu sana, na kama anaweza kutumia ela ya kampuni kutengeneza cash flow hapotezi chochote. Hii kitu nafikiri unatakiwa usiwe mlevi tu kwamba wewe unatoa pesa mfukoni tuuuu unajikopesha unabet. Kama haikufai unaacha. Kama kilimo tu kuna watu wameima sana matikiti mara mvua izidi, mara wadudu na akivuna soko linakuwa chini sasa huyu akiendelea ni mlevi wa kilimo cha matikiti na ulevi haufai kwenye bet au popote pale
 
Hapo Issue ipo kwenye Alafu Akaacha..., wangapi wanaacha ? kumbuka gambling is addictive..,

Cashlow nzuri ila ukishapata mpaka 50M unakuwa na kitu kinaitwa over-confidence ambayo bookies wanapenda sana hii ukishajiona una uwezo huo ikipungua na kubaki ndogo huchelewi kujikopesha 10M mara tatu ili urudi kwenye 50M na if things go wrong huchelewi kujikuta upo minus 30M.., ndio maana haya mambo kuna mpaka rehab na watu ndoa zimekwisha wengine kula ada ya watoto ni kawaida as well as mpaka kuuza nyumba.... Heri addiction kwenye Pombe kuliko Gambling
 
Odds za kilimo kama soko lipo na mtu kafanya due dilligence na anauwezo wa kumwagilizia ni fair kuliko odds zozote kwenye gambling hii ni leisure mkuu unless kama una illegal advantage (match fixing etc) ambayo hio sio bet tena bali ni sure thing na ni illegal and its not easy.....
 
Unajua tunapishana wapi mkuu? hapo kwenye long run. Hii si compitition kati ya anayebet na kampuni. ni compitition ya watu wa aina tatu. Mwenye kampuni, Mshindi na anayewachangia hawa wawili. Sasa ukiingia ukiona wewe unawachangia wenzako ukaendelea kukaa huo ni uzwazwa wako.
 
Upo sawa ni ulevi mbaya sana. Lakini kama ulivyo ulevi mwingine wowote ule personality ya mtu inahusika.
 
Simpi sapoti mtu ambaye anatake risk halafu anapoteza na bado anaendelea kutake aina hiyo hiyo ya risk regardless ya odds zipo fair au la. Huwezi badilisha matokeo kwa kutumia njia zile zile zilizokufelisha. Take risk mara moja au mbili haijakulipa amia kwenye aina nyingine ya risk. Haijalishi ni bet, Kilimo au nini. Sema ubaya wa betting ni kwamba hakuna production. Taifa likiwa la vijana wanaofanya bet tu litapotea. Ila kusema bet kwa mtu binafsi haiwezi mpa chochote si kweli maana watu wapo wameonekana wameshinda na wanaendesha maisha shukran kwa bets.
 
Nina uhakika kwa sasa East Africa na nchi nyingi za Africa serikali inaigiza pesa nyingi sana kutoka kwenye betting; hivi unajua kuna 20% tax ya kila anayeshinda inaenda serikalini... ? Issue mimi ipo pale pale kwa muda mrefu hakuna strategy itakayokutoa kama full time business (unless unapata pesa nje ya betting kwa kuuza vitu vinavyotokana na betting) ndio maana ma so called Gurus wengi wanauza gambling systems na Vitabu badala ya wao ku-gamble peke yake..., kama watu wanafanya kama bahati nasibu n,k. ni sawa hata Bingo na Lottery kila siku watu wanabahatisha mamilioni ya pesa na wanashinda kuna Mkenya alishenda Sportpesa ila uwezekano wa kushinda ni mdogo sio kitu cha kutegemea, na bahati nzuri uambatana na mbaya sasa on average kama kuna siku nzuri na siku mbaya ila kwenye uzuri unapata nusu kikombe na ubaya unawapa kikombe kimejaa utaona kwamba kuna uwezekano mkubwa siku ya mwisho pipa litakuwa tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…