Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kikubwa zaidi, ichukulie umri umefika wa kuoa, mke mtarajiwa anasema nami natamani kuja kwenu kwa wazazi wako, kwa mtazamo wako unafikiri nitampeleka wapi akidai twende kwa baba mzawa! Just help,
Hapa ndipo umuhimu wa mke mmoja, mtoto mmoja unapokuja.
Hakuna chance ya watoto kugombea mali.
hehehe kumbe upo blaza?
Hivi mwanaume mwenye umri wa kuoa anaweza kugombea mali za baba yake? sijui kwa nini huwa mali hazinipi mawazo kabisa aisee.
HAKI HAMNA HAPO NDUGU, zaidi atajipotezea muda tu.
Kumbuka kuacha mwenyewe utajijengea heshima zaidi kuliko kupigana vita ambayo huwezi shinda.
Hana haki ya kudai lolote hapo, anahitaji kudra tu wamsaidie ila HAKI HANA.
Hivyo suala la kwenda nae kisheria hapati kitu.Huu ndio ukweli japo mchungu.
So muhimu kwake kama anahitaji undugu ajenge undugu vinginevyo hana lake hapo.
kufahamiana kwao na mama ni kwamba kulikuwa kuna kaka wa kwanza alikufa mbaye alikuwa mkubwa kwangu ndiyo huyo wao ndio wanadai kuwa angekuwa yule wa kwanza wangekubaliana nae ila sio mimi,tatizo ndio hlo.
tpaul usemayo ni kweli...lkn kama ndugu washamsusa itachukua muda na resource kupata haki yake...kama anaweza kuishi kwa nini atumie nguvu kutambuliwa kama mwanafamilia...kwa nini asitafute tu ya kwake...
utachukua muda na pesa nyingi kugombea urithi, utajihatarisha bure. wewe uko chuo mbona umeshasimama! Tafuta maisha, amini nakwambia hao ndugu wanaotegemea pango la nyumba zilizojengwa miaka hiyo watakuja kwako kutaka msaada. PIGA KAZI.
Hakuna sheria kama hiyo...weka ushahidiia hiyo unayoisema...Kuwa Baba akizaa nje mtoto wa nje ana haki ya kudai mali za ndoa za baba yake...HAKUNA SHERIA HIYO...HANA HAKI HIYO.kwani hujui SHERIA inasema nini kuhusu urithi? je, unafahamu kwamba ipo sheria inayohusu mambo ya urithi inayomlinda apate haki yake?
mkuu Zamaulid, hapa suala sio kutambuliwa. ndugu wamtambue wasimtambue, ni haki yake kupata urithi kwa kuwa ni mtoto halali wa marehemu baba yake. hata akina mama wanaozaa nje ya ndoa huwabambika waume zao watoto waliozalishwa na michepuko lakini huja kuumbuliwa na kipimo cha DNA....hiki ni kipimo mojawapo ambacho jamaa anaweza kukitumia kama last alternative (ikiwa hana documents zozote) ili apate haki yake. lakini nakumbuka mkuu Lukas4 anasema kwamba anazo picha alizowahi kupiga na babaye na pia anacho cheti cha kuzaliwa. na sio kwamba ndugu wote hawamtambui ila baadhi yao wenye roho mbaya kama kauzu ndio wanamkataa. anaweza kuwatumia hao ndugu wanaomkubali kama mashahidi+docmuments+photos, etc kupata haki yake ya urithi. kwanini ateseke kujitafutia karo wakati baba yake ameacha mali lukuki? sio haki hata kidogo.
vithibitisho vipo kama picha za utotoni ambazo nilipiga naye, furthermore baada ya kumaliza kidato cha nne baba yangu alikuja kunichukua na kunipeleka kwake kwa mama mkubwa na kumtambulisha pamoja pamoja na watoto zake. Pingamizi kubwa ni kwa baba mdogo na shangazi zangu, inafika mwaafaka ninakosa hadi amani kwamba mimi ninani kakika jamii!
Dogo naomba ukubali hii, babako alidhamiria kuinvest kwako through EDUCATION.
Kutokuwepo Kwa wasia kuhusu mgao wako inathibitisha kuwa mpk hapo diploma ulipo ndio URITHI wako, kuanzia hapo kwenda juu ni msuli wako!
Hata huo mgao wa Mali unaotaka, unaweza kupewa kiasi tu, kuendeleza no juu yako! Na pia dogo umebahatika wee ni wa kiume, huo pia ni mtaji, JIKUBALI
Dogo naomba ukubali hii, babako alidhamiria kuinvest kwako through EDUCATION.
Kutokuwepo Kwa wasia kuhusu mgao wako inathibitisha kuwa mpk hapo diploma ulipo ndio URITHI wako, kuanzia hapo kwenda juu ni msuli wako!
Hata huo mgao wa Mali unaotaka, unaweza kupewa kiasi tu, kuendeleza no juu yako! Na pia dogo umebahatika wee ni wa kiume, huo pia ni mtaji, JIKUBALI