Ligi ya kujilinganisha simu na iPhone sijui itaisha lini?
Sio Samsung, Tecno, Bb, Tesla, Nothing phone, Oppo, Huawei n.k. wote hao hakuna wa kujilinganisha na android mwenzake ni iPhone tu.
Hizi kampuni naamini wateja ndo wana ligi ila zenyewe nikupambana kimya kimya tu mali yake iwe bora na kuuzika zaidi ila sio ijitetee kuwa mali yake ni nzuri kuliko mali ya mwingine
Kila simu ina mazuri yake na mapungufu yake hakuna iliyokamika kwa % zote na haitotokea tukubaliane tu kama binadam aso hili ana lile, na kwenye simu mwendo ni huo huo tu.
Na matumizi nayo yametofautiana photographer hapo atakuelewa ila ukija kwa bora mawasiliano hana habari na picha nzuri!