kamwendo
JF-Expert Member
- Apr 19, 2012
- 900
- 1,923
Umenikumbusha mbali Mkuu,Simuwazii mwanamke mabaya ila sitaki nihitimishe kuwa huo ndo ukweli 100% nikilinganisha na maelezo ya mdogo wako.
Kaa na dogo mzungumze kiume, usikute hata chanzo cha mirungi ni mwanamke. Usimchukulie poa mwanamke linapokuja suala la kuwa innocent, wana uwezo mkubwa sana wa kuaminika na kuonekana hawana makosa.
Kitendo cha kuwa na ujasiri wa kusema kuwa haniridhishi na mdogo wako kusema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akitaka waachane usihitimishe kuwa dogo ndo tatizo 100%, kama sio kweli kwa 100% mtampoteza mdogo wenu na mawazo.
Mwanamke akipiga yowe ukawa wa kwanza kufika ukamkuta kadondosha chungu huku kajilowesha maji kipande cha nguo yake kikiwa pembeni kabla hujamwinua au kumsaidia na kumuuliza ni nn shida, hakikisha kuna mtu mwingine kafika au mazingira ni salama maana wanaokuja nyuma wanaweza hata wasimuulize shida ni nn wakakuua wewe.
Rafiki yangu iliwahi kumtokea hii kitu mpaka Leo ni mlemavu wa mguu
Ilitokea Laela B, Sumbawanga uko mkoa wa Rukwa. Jamaa alikuwa na mahusiano na bint badae wakaja kuachana kumbe bint hakupendezwa na jinsi alivyoachwa. Zikapita wiki hatimaye miezi 3 tangu waachane siku hiyo rafiki yangu Hana hili Wala lile akapigiwa simu na bint kuwa anamuhitaji sehemu Ana shida ya dharula .
Jamaa tulikuwa nae tunaangalia Mpira akatuaga akaenda Kijiji Cha pili alipo demu kufika uko kamkuta bint njian anamuuliza alichomuitia ni kipi bint anajiuma Uma Mara ghafla bint anaanza kulia kama utani tu kaangua bonge la kilio akajiangusha chini jamaa haelewi anaanza kum,bembeleza kuhamaki watu washaanza kukaaa bint anadai kabakwa daah
Jamaa angu alipigwa Sana bahati kuitwa mjumbe ndo kuwahoji Hadi polisi bint kapimwa zahanati hamna kitu ikabidi kesi imalizwe kifamilia aisee.
Wanawake sio watu wa kuwaamini .