Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na mimi narudia kukuambia jipe Muda.Nimejivunia kipi hasa hapo zaidi ya kumtukuza Mungu kuwa ni mwema kuniepusha na huo upuuzi?
Rudia kusoma nilichoandika.
Picha inaonesha kuwa mirungi na kisamvu ni mapacha sasa kisamvu iitwe Kisamvu doto na mirungi iitwe Mirungi kulwa ili mirungi ihalalishwe kama kisamvu, mimi naiona iko poa tu.Hii kitu kwa sisi wakaayi ni culture View attachment 2087989
Sent from my SM-G960U1 using JamiiForums mobile app
Uraibu wako ni upi....?Mirungi huaribu sana nguvu za uume, wakati mwingine ktk hii dunia si kila kitu ni cha faida na chakuigwa.
Ona sasa Mke mwema kabisa anakosa Mume sahihi na kuachwa njia panda.
Mungu ni mwema sana kuniepusha na ulevi wowote wa sigara, bangi, kokein, shisha, pombe, pornography na uzinzi wa Wanawake na hata hii mitandao ya kijamii.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] veveSema veve ukiizoea ina addiction aseee ukifika ule mda wake unapata arosto mbaya mbovu.
Mkuu nyie ni Warangi? Maana hao watu wanapenda sana kuchanja veve/miraa/mirungi/gomba.
Hilo la mirungi ni kweli mkuu,,Mara kwa mara nimekuwa nikipenda kuweka visa vinavyogusa maisha yangu hata marafiki na ndugu zangu ili mpate kitu cha kujifunza hapa
Mdogo wangu wa kiume ana mwanamke ambae alimuowa mwaka 2017, ni binti mstaharabu sana mwenye heshima sana maana hata nyumbani ukweni anapendwa sana na wazee na dada zangu pia,
Hatari sanaGomba aka miraa
Warangi
Wadigo
Wapare
Makabila haya yamekuwa wahanga wakubwa wa miraa
Yupi huyoHilo la mirungi ni kweli mkuu,,
Walaji wengi wa mirungi ndoa zinawashinda.
Kama yule jamaa vuvuzela,
Ndoa ya 6 sasa,,
Shida mirungi
Yaan hapo uyo shemejiyo ukimwomba tyu lazima akupe, wanawake wanapenda wasuluhishaji mkuu!Mara kwa mara nimekuwa nikipenda kuweka visa vinavyogusa maisha yangu hata marafiki na ndugu zangu ili mpate kitu cha kujifunza hapa
Mdogo wangu wa kiume ana mwanamke ambae alimuowa mwaka 2017, ni binti mstaharabu sana mwenye heshima sana maana hata nyumbani ukweni anapendwa sana na wazee na dada zangu pia,
Hujaelezea umesuluhishajeMara kwa mara nimekuwa nikipenda kuweka visa vinavyogusa maisha yangu hata marafiki na ndugu zangu ili mpate kitu cha kujifunza hapa
Mdogo wangu wa kiume ana mwanamke ambae alimuowa mwaka 2017, ni binti mstaharabu sana mwenye heshima sana maana hata nyumbani ukweni anapendwa sana na wazee na dada zangu pia,
Sipendagi kuruhusu akili yangu itawaliwe sana na uraibu wa kitu kimoja tu maana nafahamu madhara yake ni mazito sana.Uraibu wako ni upi....?
Apo kwa wanawake Sasa....
Soma hadi mwisho wazazi wa mke wamekataa kusuluhisha wameondoka ba binti yaoHujaelezea umesuluhishaje
Utachelewa sana kubadilisha tabia ikiwa kila tatizo lako unatafuta wa kumtupia lawama.Simuwazii mwanamke mabaya ila sitaki nihitimishe kuwa huo ndo ukweli 100% nikilinganisha na maelezo ya mdogo wako.
Kaa na dogo mzungumze kiume, usikute hata chanzo cha mirungi ni mwanamke. Usimchukulie poa mwanamke linapokuja suala la kuwa innocent, wana uwezo mkubwa sana wa kuaminika na kuonekana hawana makosa.
Kitendo cha kuwa na ujasiri wa kusema kuwa haniridhishi na mdogo wako kusema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akitaka waachane usihitimishe kuwa dogo ndo tatizo 100%, kama sio kweli kwa 100% mtampoteza mdogo wenu na mawazo.
Mwanamke akipiga yowe ukawa wa kwanza kufika ukamkuta kadondosha chungu huku kajilowesha maji kipande cha nguo yake kikiwa pembeni kabla hujamwinua au kumsaidia na kumuuliza ni nn shida, hakikisha kuna mtu mwingine kafika au mazingira ni salama maana wanaokuja nyuma wanaweza hata wasimuulize shida ni nn wakakuua wewe.
Wanaume bana mnapenda kufichiwa kila kitu chenu cha aibu....ingekuwa ndo mwanamke hapo mngesema chepuka au mwache huyo hakufai.mwanamke nae ni ki roporopo
asa ni kwa nn alisema hayo yote kwenye kikao?
si angesubiri tu amwambie baba mkwe mwenyewe au hata wewe
Hakuna anayetupiwa lawama hapo. Ila mtoto wa kiume anatakiwa pia kulindwa.Utachelewa sana kubadilisha tabia ikiwa kila tatizo lako unatafuta wa kumtupia lawama.
Naomba namba ya shemejiMara kwa mara nimekuwa nikipenda kuweka visa vinavyogusa maisha yangu hata marafiki na ndugu zangu ili mpate kitu cha kujifunza hapa
Mdogo wangu wa kiume ana mwanamke ambae alimuowa mwaka 2017, ni binti mstaharabu sana mwenye heshima sana maana hata nyumbani ukweni anapendwa sana na wazee na dada zangu pia,
Sasa kuazia mwaka 2020 tukawa tunaskia visa vya chini chini tu kuwa mdogo wangu amekuwa akimnyanyasa sana huyo binti na unyanyasaji alio kuwa nao ulikuwa ni wivu kupitiliza na kufanya binti kuwa kama mfungwa maana alikuwa hataki afanye kazi yoyote wala kutoka nyumbani akiamini akitoka ataenda kupitiwa na wanaume wengine
Wiki iliyopita ulitokea ugomvi mkubwa dogo alimpiga yule binti nusu amuuwe ikabidi familia upande wa mwanume na kwao upande wa mwanamke tufunge safari kuja Dar kujua tatizo ni nini na kusuluhisha pia, hivyo tulivyofika kikawekwa kikako kikubwa ili lijulikane jambo lililopelekea Bro kufanya kitendo kibaya kama kile ambacho si jadi yetu.
Dogo alipopewa nafasi aeleze nini shida, akasema kuwa mwanamke wake, kwa muda wa mwezi sasa amekuwa akitaka watengane kwa amani ili migogoro na wivu uliopotiliza isiendelee na kila mtu awe na amani na maisha yaendelee, akasema kuwa kitendo hicho kilimfanya amuhisi mkewe kuwa tayari ana mwanaume mwingine hivyo alikuwa anatafuta sababu tu watengane na akiangalia kasha mgharamia vitu vingi hivyo akajikuta mkono umeteleza akamshushia kipigo lakini anajutia
Ikabidi tuje na kwa upande wa Binti tumskilize na yeye atoe maelezo yake tujue mwenye tatizo ni nani, hapa ndipo tulipoaibika maana mambo aliyoyaongea binti tulijikuta sisi kama upande wa mwanaume tunaaibika mbele ya ndugu wa mwanamke
Binti uvumilivu ukamshinda ikabidi afunguke yote, akasema kuanzia wameanza kuishi wote mwanaume alijiingiza kwenye matumizi ya mirungi sijui wanaita gomba kupitiliza, asasema akirudi kazini kazi yake ikawa ni kukaa nnje anasaga mirungi hadi sa tano au sita za usiku kila siku akawa anashindilia mirungi tu na Sigara, ndani anakuja kulala saa sita or saba usiku
Binti akasema kuwa aliendelea kumvumilia tu na kila alipomshauri aache kutumia hivyo vitu akawa anaambulia maneno makali
Akasema kuwa ikafika kipindi akawa amebadilika kabisa yani hata kitandani uwezo wa kufanya mapenzi hadi kumridhisha ukawa umepotea kabisa yaani akifika chumbani ni kulala tu hamu ya mapenzi na nguvu ya kufanya mapenzi ikapotea kabisa hvyo kilichofuatia yakawa ni maisha ya wivu tu sababu alikuwa hamridhishi kitandani.
Baada ya kusikiliza pande zote mbili ikaonekana Mwanaume ndio ana matatizo tena sio madogo ni makubwa, Upande wa Binti ukagoma kusulihisha wakasema wanaondoka na mtoto wao wanaogopa atakuja kukatwa na mapanga aje auliwe huko mbeleni na wameondoka nae kweli.
Mzee kwa Hasira akamwambia Bwanamdogo kuwa amepoteza mwanamke mzuri kwa ajili ya uzembe wake, akamwambia kuwa yule mwanamke alivumilia sana pasipo kutafuta mapenzi nnje akiamimi atabadilika lakini Dogo hakubadilika.
Akamwambia kuwa akipata mwanamke mwingine kichaa kwa tabia zile atamletea mwanamme mwingine chumbani kwake pale pale atamsaidia kazi vizuri.
Wakuu tumeaibika sana hapa tupo kwenye basi na wazee tunarudi mkoa kwa aibu kali sana , tumeaibika sana, mzee wetu amekasirika sana anasema ni heri Bwanamdogo angemueleza tu ukweli kwenye Simu asingekanyaga ardhi ya Dar kufuata aibu kama ile