Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Mama mkwe wako mtu mzuli sana.Mzee kachanganya na watu wa Burundi.
Jamaa yangu mmoja alipenda na bint wa Burundi.wakaenda kwao kutoa mkaja mwisho wafunge ndoa.Mwisho nilimuona rafiki akilejea peke yake.
Mama wa yule wa bint aliomba radhi lakini mshikaji aliwapotezea wote...
 
Pole best. Mke anakupenda Kwa dhati nadhani mpende pia. Wazazi wake fanya kuwasamehe lakini usiende tena kigoma. Mwisho funga ndoa harali ikibidi bila hata wazazi wake kuwepo ili likitokea la kutokea uwe on safe place
Hili ndio wazo,kwakuwa unesha tangulia kitu funga ndoa ya kawaida serekali maisha yaendelee, kuna makosa hata wewe umeyafanya huwezi mpata mtoto wa watu mimba then ukamchukuwa kirahi hivyo hata mimi ningekuchenchia aisee
 
Madhira gani jamaa kasababisha? Basi wamuoe wao wenyewe. Umasikini ndio huchagiza watu kuwa na roho mbaya kama huyo baba mkwe wa jamaa. Million 4 hata kwa mtutu siwezi kutoa ili nioe tena kibaya zaidi ili nioe muha
 
Watu wanaolewa kwa mahari ya kitanda na godoro mjini hapa,WENGINE mahari NI elfu 50.Kijijini ukatoe mahari ambayo ukienda chanika unapata Banda la kuishi😭😭😭😭😭
 
ushakanyaga kwenye territory za mzee, ukiishia njiani hatakuacha salama...huyo mzee anachokitafuta ni heshima na kuna kitu kinampa jeuri. Kubali kuingia garama utume mtu mzee kutoka kwenu akayaongee.

Hata hivyo umekosea, ingetakiwa waende wazee wako kwanza ndo ufuate wewe. Au kwa sababu za kiuchumi na kuokoa garama ungeambatana na baba yako au mzee kutoka kwenu.
 
Kuna siri kubwa sana imejificha wahenga waliposema ukitaka kuoa familia /ukoo fulani chunguza kwanza baadhi ya tabia,mila na desturi za watu husika.

Suala la kuunganisha familia linahitaji ukomavu na kujiridhisha kwa mambo mengi sana.

Naamini kuna baadhi ya tabia za kwao ungezijua kabla hata hujafanya maamuzi ya kuzaa naye.

Mwisho wa siku unafikiri sasa mtoto akue ufanye maamuzi mengine ambayo yanaweza kuja kukugharimu zaidi.
 
Kwa kifupi hawa wakwe walikuwa wamekukataa, walijua kuwa wewe siyo binadamu wa kawaida. Hata angekuwa mtu mwingine tofauti na hao, naye pia vile vile angekukataa
Waha wana maadili sana ukiwaendea vingine wanakushangaa
Sasa walitegemea mimi nisafiri kutoka Dar mpaka huko kwao kuhudhuria msiba tu
 
Kwanza huyo mzee kukwambia muende wote na mkeo ni kua ile "nimekubali kwa mbinde" na huko ulikomuacha na mama mkwe itakua kapewa vipande vyake....usimuache mke anaekupenda kwa sababu ya dingi yake mnoko..huyo dingi yake ni watu wenye hasira za karibu na watu wa hivo huwa wanapoa haraka...relax..enjoy with your family..time heals
 
Kwenye hiyo familia hakuna shida hata baba mkwe hana shida ,

Umempa mimba binti hilo ni kosa , kimila na kisheri , sasa huyo mzee amekupiga fain, kwnza ulitakiwa uwende kuomba msamaha kwa uwaribu ulioufanya baada ya hili kuisha ndio sasa uzungumzie kuhusu ndoa. Umesema yule mazee alikuwa anazungumzia kuhusu cm zako , na pesa uliokuwa unamtumia bint, jalibu kuongea na bint , bint aongee na mama, mama aongee na baba hapo panaweza patikana suluhu
 
Uchafuzi upi huo?,kwani alimbaka mzazi mjinga ndio ataona usemalo wewe...mzazi muerevu ataona jambo jema binti yake analipiwa mahari,
Je angezalishwa tu huyo mkwe angempata wapi
 
Kwa hiyo kwa mtazamo wako sisi kutoka Dar mpaka Kigoma kwenda kuyajenga tulikuwa wapumbavu?
Ilikuwa busara kuona dhamira yetu na kuwa muungwana, ila kwa réaction aliyoonyesha atabaki n'a mtoto wake tu, siwezi kuwa n'a baba mkwe wa aina yake
Kuzaliwa familia maskini ni bahati mbaya...ila kuoa kwenye familia masikini ni kujiongezea matatizo
 
Watu wanaenda ukweni mtoto anaumri wa chekechea na maisha yanasonga,siku hizi binti anapanga mahari yake..then wazazi wanaridhia,5m unanunua shamba au kiwanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…