Wachawi huwaroga wapumbavu wanaokubali kurogwa.Huu ushauri utamletea jamaa matatizo, uwajui waha vizuri hasa hao wa huko vijijini haswa ni wachawi mno
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wachawi huwaroga wapumbavu wanaokubali kurogwa.Huu ushauri utamletea jamaa matatizo, uwajui waha vizuri hasa hao wa huko vijijini haswa ni wachawi mno
Mama mkwe wako mtu mzuli sana.Mzee kachanganya na watu wa Burundi.Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!
Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!
Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!
Akiwa kwao mawasiliano yetu yalikuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswa mpaka dk. ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume.
Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea na maisha ya sogea tuishi.
Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka.
Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpenzi wangu.
Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nimeambatana na brother wangu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.
Brother akaniuliza, "Hivi dogo hukuona wanawake mikoa yote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu. Tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za Kiha ili mambo yasiwe magumu.
Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi, hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe, nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.
Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!
Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!
Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba na mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu, mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani.
Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k.
Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema "Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"
"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, sitaki mjadala!"
Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sana, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri."
Tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!
Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani Tsh. 500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k, sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!
Muda huo wote nina hasira vibaya mno, ila najitahidi kuificha japo mpenzi wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia. Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "Mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu," tukawaambia sawa.
Muda wa kutoka nikakuta mpenzi wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapaswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari. Akagoma, akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki kijijini tena. Nikamwambia hapana, unapaswa kubaki mpaka tumalizane na mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu, machozi yanamtoka tu!
Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "Kama mnaondoka wote nendeni tu!" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu), akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.
Basi kishingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira. Akamuita mtoto wake, akamwambia "Mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, na mimi mama naomba atusamehe tu."
Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mno, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini. Tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpenzi wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba sitokaa nirudi Kigoma, wala sitokaa nipeleke hiyo mahari waliyosema.
Nasubiri mwanangu akuekue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena.
Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyways.
Hili ndio wazo,kwakuwa unesha tangulia kitu funga ndoa ya kawaida serekali maisha yaendelee, kuna makosa hata wewe umeyafanya huwezi mpata mtoto wa watu mimba then ukamchukuwa kirahi hivyo hata mimi ningekuchenchia aiseePole best. Mke anakupenda Kwa dhati nadhani mpende pia. Wazazi wake fanya kuwasamehe lakini usiende tena kigoma. Mwisho funga ndoa harali ikibidi bila hata wazazi wake kuwepo ili likitokea la kutokea uwe on safe place
hapa ndipo huu msemo unapopata tumizi lake haswaaPole sana mkuu hata wapumbavu huzeeka, amemgeuza binti yake mtaji.
Madhira gani jamaa kasababisha? Basi wamuoe wao wenyewe. Umasikini ndio huchagiza watu kuwa na roho mbaya kama huyo baba mkwe wa jamaa. Million 4 hata kwa mtutu siwezi kutoa ili nioe tena kibaya zaidi ili nioe muhaDogo lazima ukubali kuwa una matatizo. Ulifanya ujinga, umemtia binti wa watu ukaendelea kumficha kwako badala ya kujisalimisha mapema.
Badala ya kwenda mikono nyuma, kwa adabu, unyenyekevu na kuomba radhi, unajifanya kijogoo na mwenye pesa!. Milioni 4 unaiona pesa nyingi bila kuhesabu madhira uliyosababisha kwa wazazi wa huyo binti. Ulitakiwa kuwa na hekima kubwa kwa kutanguliza wajumbe kuyamaliza ndipo ukaribishwe kwa heshima kama mwana aliyekosea na kujirudi.
Kwa ujinga wako unawaza umbali, mahari na faini uliyojipangia mwenyewe, unajiaibisha. Jipange, tuma wazazi wako au wajomba/shangai ili wayaweke sawa na yataisha kilaini badala ya kuchukua mtu barabarani ati kuchukua nafasi ya wazazi. Ingekuwa wewe ungempokea mtu ambaye hata sio ndugu yako kuchukua nafasi ya wazazi? Kaka yako ni mtoto kama wewe kwa wakwe zako, kiri kukosea na utengeneze upate mke.
Vv
Milioni5??? Kwa hapo aisee hawanipati hata wamuue albinoSasa hi ndo maana halisi ya ule msemo wa " Kupigwa kitu kizito kichwani".
Baba mkwe alitisha Sana kwa kweli dah 🤔
Watu wanaolewa kwa mahari ya kitanda na godoro mjini hapa,WENGINE mahari NI elfu 50.Kijijini ukatoe mahari ambayo ukienda chanika unapata Banda la kuishi😭😭😭😭😭Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!
Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!
Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!
Akiwa kwao mawasiliano yetu yalikuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswa mpaka dk. ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume.
Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea na maisha ya sogea tuishi.
Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka.
Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpenzi wangu.
Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nimeambatana na brother wangu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.
Brother akaniuliza, "Hivi dogo hukuona wanawake mikoa yote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu. Tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za Kiha ili mambo yasiwe magumu.
Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi, hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe, nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.
Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!
Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!
Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba na mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu, mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani.
Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k.
Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema "Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"
"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, sitaki mjadala!"
Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sana, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri."
Tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!
Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani Tsh. 500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k, sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!
Muda huo wote nina hasira vibaya mno, ila najitahidi kuificha japo mpenzi wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia. Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "Mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu," tukawaambia sawa.
Muda wa kutoka nikakuta mpenzi wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapaswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari. Akagoma, akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki kijijini tena. Nikamwambia hapana, unapaswa kubaki mpaka tumalizane na mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu, machozi yanamtoka tu!
Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "Kama mnaondoka wote nendeni tu!" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu), akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.
Basi kishingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira. Akamuita mtoto wake, akamwambia "Mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, na mimi mama naomba atusamehe tu."
Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mno, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini. Tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpenzi wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba sitokaa nirudi Kigoma, wala sitokaa nipeleke hiyo mahari waliyosema.
Nasubiri mwanangu akuekue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena.
Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyways.
Na kama si Buhigwe pale basi katanga hukoHIYO NI BUHIGWE MOJA
Sasa walitegemea mimi nisafiri kutoka Dar mpaka huko kwao kuhudhuria msiba tuKwa kifupi hawa wakwe walikuwa wamekukataa, walijua kuwa wewe siyo binadamu wa kawaida. Hata angekuwa mtu mwingine tofauti na hao, naye pia vile vile angekukataa
Waha wana maadili sana ukiwaendea vingine wanakushangaa
Dah, we jamaa ni mmbeaPole Sana, Kijiji Gani Hicho
Uchafuzi upi huo?,kwani alimbaka mzazi mjinga ndio ataona usemalo wewe...mzazi muerevu ataona jambo jema binti yake analipiwa mahari,Hilo la kuua mtoto si kweli.Mambo huwa complicated unapozaa kabla ya kutimiza taratibu.Punguza hasira.Naturally wababa huwa overprotective kwa Binti zao. Jipe muda, baadaye utagundua huyo Mzee ni mtu poa kuliko unavyodhani. Utaratibu mzuri wa kuoa huku ni kwamba Binti stoke mbichi Nyumbani. Wee umefanya uchafuzi halafu unataka fair? Kila kabila na taratibu zake. Jipe muda utagundua. Mwenyezi Mungu awajalie Kila lililo la heri kwenye familia Yako changa.
Kuzaliwa familia maskini ni bahati mbaya...ila kuoa kwenye familia masikini ni kujiongezea matatizoKwa hiyo kwa mtazamo wako sisi kutoka Dar mpaka Kigoma kwenda kuyajenga tulikuwa wapumbavu?
Ilikuwa busara kuona dhamira yetu na kuwa muungwana, ila kwa réaction aliyoonyesha atabaki n'a mtoto wake tu, siwezi kuwa n'a baba mkwe wa aina yake
Kabisa ila kuoa familia yenye njaa ni kujiongezea mzigo...pili familia zenye msimamo hawaoini mbali,dar to kigoma sio chini ya km 1400Mapenzi ni ya wawili.....over!!
Watu wanaenda ukweni mtoto anaumri wa chekechea na maisha yanasonga,siku hizi binti anapanga mahari yake..then wazazi wanaridhia,5m unanunua shamba au kiwanjaSasa mkuu ulitakiwa familia ya mwanamke ikujue kabla ya mimba au mtoto kuzaliwa, sasa wewe unaishi na mtoto wa mtu kabla ya kumpa ujauzito mpaka anajifungua upo kimya na mpaka anaenda kwao anakaa miezi mingi kazi yako ni kupiga simu na kumtumia pesa we unavyoona ulikuwa sahihi?, je mimba ingetoka mpaka leo ungekuwa unaishi naye bila kujulikana kwao, wewe ulienda kuweni kwaajili ya mtoto bila kuwepo na mtoto safari ya Kigoma hakuna .