Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Uislam ni dini safi kabisa linapokuja swala la ndoa, mahari simple kabisa, sio huku watu wanafanya kuuza watoto wao ili kujipatia kipato kikubwa!
Sidhani kama hiyo ndiyo maana halisi ya mahari!
 
Wewe ni mjinga, mtu kukuletea zawadi ni kudanganywa [emoji706] au mtaonekana mnadhiki..?

Kuna watu waliacha kuoa kisa hayo mamilioni waliaga wakenda mazima
Sijajua wewe kabila gani yani umuharibi maisha binti yangu uishi naye kama mke bila baraka ya wazazi kisha umzalishe aje nyumbani kwangu kila uje na zawadi za danganya toto.
 
Ww itakua hujasoma bandiko la mleta mada vizuri na kulielewa.
Shida sio hela aliyotajiwa, shida ni pale baba mkwe wa mchongo alivyoleta ubabe na vitisho. Sasa kuepusha yote hayo akae na mwanae na mjuu awalee.

Mbona watu wa namna hii wamekomeshwa na wengi. Binti zao wamepigwa mimba na jamaa haonekani maisha yote. Kitu gani kizuri kama jamaa kujitokeza tena kiungwana na yuko tayar kwa mahali. Kama ni hela angeiomba kistaarab. Angepokea zilizopo na wakapeana muda wa kuzilipa ili kulinda undugu na mahusiano.
 
Ulifanya Makosa kwenda Kwa kumsikiliza hiyo Mchumba wako. Hivi vibinti vya siku hizi havijui mambo ya Mila. Alisema milioni 1 ili uende.

Kama alikudhalilisha Sana na kukutokea maneno ya shombo. Piga Chini.
Sio lazima uwe na Binti Yao
 
Ndio usha yakanyaga sasa
 
Na wewe umekazania wazanzibari wazanzibari, kwa hiyo Zanzibar hakuna single mothers?

Na huko ukumbuke asilimia kubwa ya wakaazi wake ni waislamu, ambao mahari kwao sio kikwazo kufunga ndoa, that is why ni rahisi watu kuingia ndoani n'a kutoka pia!

Kama mtu anaweza kuoa kwa mahari ya sh. laki mbili na baada ya mwezi akamuacha mke na kuoa mwingine, unaringanishaje na hizi za kwetu?

Umesema kila jamii ina utaratibu wake, kwa hiyo unapokazania yanayotokea Zanzibar, jua kabisa nako kuna madhaifu yake!
 
Ilikuwa wilaya gani na kijiji gani.Nimeumia sana? Kuna jambo nataka kusaidia hapa
 

huwezi elewa uzito wa kiatu cha mtu kama hujakivaa... yule ni mzazi probably ana hasira after all jamaa kaonyesha busara piaa ila bado mtoa mada kilio chake ni mahali ukiachana na kukasirika kwa baba mkwe wake nadhan hata wewe hujamwelewa mtoa mada[emoji28][emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…