Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Hapa issue sio kiasi cha hela, hata kama baba kaagiza milioni kumi, hayo ni mambo ambayo huzungumzwa na kuwekana sawa, ila mwanzo dogo alipaswa kurekebisha kosa alilolifanya.
Sasa anataka kutelekeza familia, mama na mwanaye kisa babake binti alimfokea kwa alichokifanya? Huyu dogo awajibike, hata kama hatoitoa hiyo mahari haipaswi atelekeze familia, ahusishe wazee wa kwao wamsaidie kurekebisha.
Sasa kama huyo mzee atakaza unadhani nini kinaenda kutokea? Ni kutelekeza tu. Siwezi toa hata mil.2 mimi
 
Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!

Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!

Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!

Akiwa kwao mawasiliano yetu yalikuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswa mpaka dk. ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume.

Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea na maisha ya sogea tuishi.

Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka.

Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpenzi wangu.

Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nimeambatana na brother wangu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.

Brother akaniuliza, "Hivi dogo hukuona wanawake mikoa yote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu. Tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za Kiha ili mambo yasiwe magumu.

Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi, hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe, nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.

Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!

Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!

Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba na mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu, mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani.

Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k.

Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema "Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"

"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, sitaki mjadala!"

Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sana, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri."

Tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!

Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani Tsh. 500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k, sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!

Muda huo wote nina hasira vibaya mno, ila najitahidi kuificha japo mpenzi wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia. Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "Mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu," tukawaambia sawa.

Muda wa kutoka nikakuta mpenzi wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapaswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari. Akagoma, akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki kijijini tena. Nikamwambia hapana, unapaswa kubaki mpaka tumalizane na mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu, machozi yanamtoka tu!

Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "Kama mnaondoka wote nendeni tu!" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu), akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.

Basi kishingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira. Akamuita mtoto wake, akamwambia "Mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, na mimi mama naomba atusamehe tu."

Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mno, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini. Tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpenzi wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba sitokaa nirudi Kigoma, wala sitokaa nipeleke hiyo mahari waliyosema.

Nasubiri mwanangu akuekue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena.

Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyways.
Wapumbafu Sana ,pole sna
 
Na huu ndiyo mtihani sasa, nawezaje kuwa na mke ambaye sina mahusiano mazuri na familia yake, tena baba kabisa!
Na ukilikibali hilo utanyqnyasika mno! Kuna siku watakwambia mtoto wao asipike,asifue asizae, na mengine mengi au ukipata dharura ndoa itavunjwa utake usitake .
Binafsi ningekuwa mimi ,uchumba ndo ungeishia hapo!
Andaa taratibu za malezi ya mwanao tu mkuu mpe bint uhuru mapema.
Kumbuka baba mkwe hakuridhia bint yake aende mjini sasa ikitokea ishu yoyote kwa huyo bint Mzee hata kuelewa.
 
Pole, kuna mkinga mmoja alitufanyiaga kama hivi watu tumetoka dar alafu mtu analeta za kuleta.
 
Tulienda na gari tukaiacha mjini, kutoka mjini kwenda huko Kijijini tulikodi boda boda kwani njia ni mbaya mno!
Mkuu hao huwa hawana utu wala huruma my kaka alisamehe kila kitu.
Huwa na misimamo na hawabadiliki .
Bint anajielewa lakini hawezi kmbadili baba , UKISTULIWA , ..STUKA!
 
Haya yako malaini kabisa,mie nitakuja kuleta kisa changu humu nita kutag utaona yako cha mtoto kabisa.
 
Halafu wazee huwa ni mikwala,angekuwa Mama yake ndio AME act vingenevyo hapo kazi angekuwa nayo.
Mama wa Mabinti ndio huwa nuksi sana,wanaua ndio nyingi sana.
 
Ulifanya kosa la kwanza, kabla hujarekebisha hilo ulafanya la pili, kabla nalo hujarekebisha ukaenda kufanya la tatu.

Ulipaswa utume kwanza wazee wakazungumze na kuomba radhi then ndio waseme nia ya wewe kutaka kumuoa binti yao.

Mzee hakukosea, huna adabu na una dharau.
 
Mkuu hakuna namna hapo. Sasa ni aidha umuache mke ili mtoto ateseke kuwafurahisha wazazi na kufurahisha nafsi yako lakini pia kunuumiza mkeo au ishi na mke ili uwaumize wazazi wake.

Mwisho na Kwa umuhimu kupanga ni kuchagua. Hapa tutakushauri mengi Ila siku yakikupata ya kukupata hutotuona kwenye shida yako mkuu
Well said
 
Ulifanya kosa la kwanza, kabla hujarekebisha hilo ulafanya la pili, kabla nalo hujarekebisha ukaenda kufanya la tatu.

Ulipaswa utume kwanza wazee wakazungumze na kuomba radhi then ndio waseme nia ya wewe kutaka kumuoa binti yao.

Mzee hakukosea, huna adabu na una dharau.
Wewe utakuwa muha. Hivi milioni nne unaijua? Hao inaonyesha wana maisha magumu kwahiyo wanataka kutumia huo mwanya kupunguzia ufukara walionao. Hilo kosa haliwezi kuwa na adhabu ya hivyo
 
Wewe utakuwa muha. Hivi milioni nne unaijua? Hao inaonyesha wana maisha magumu kwahiyo wanataka kutumia huo mwanya kupunguzia ufukara walionao. Hilo kosa haliwezi kuwa na adhabu ya hivyo
Tumia akili japo kidogo tu ile ya kuvukia barabara. Hapo shida wala sio pesa.

Anyway, ukikua utaelewa.
 
Tumia akili japo kidogo tu ile ya kuvukia barabara. Hapo shida wala sio pesa.

Anyway, ukikua utaelewa.
Wewe MUHA waambie waha wenzako wapunguze upumbavu. Mnanuka shida mnatafuta magepu kiboya.
 
Back
Top Bottom