Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Vitu vidogo Sana hivyo sema u bado mdogo
Mahari hata iwe milioni 100 Huwa hakuna anaemaliza mahari,hizo ni figure tu.
We zaa tu,ishaisha hio
 
Pole best. Mke anakupenda Kwa dhati nadhani mpende pia. Wazazi wake fanya kuwasamehe lakini usiende tena kigoma. Mwisho funga ndoa harali ikibidi bila hata wazazi wake kuwepo ili likitokea la kutokea uwe on safe place

Engineer, afunge ndoa bila ridhaa ya wazazi kwa tamaduni zetu? Hiyo ni a time bomb! Balaa kubwa!
 
Kujitia umwamba kwa vitu vya namna hii haifai n'a ni tabia mbaya kabisa, sasa akibaki na mtoto wake atamuoa yeye???
Mlikutana/walikutana chuo ,kutoka kigoma nani alifanikisha mtia mimba au mzazi ,kama ndivyo ilipwe

Swala la kumtukana mkwe ,haisaidii ukigoma ,nakushauri kakomboe mtoto fasta
 
Nimetafakari sanaaa, nampenda sana mama wa mtoto wangu lakini sina namna zaidi ya kumuacha aendeee kuepusha Shari za baadaye!
Kosa kubwa Sana endapo atafanya hvo au kama ameshafanya. Ikumbukwe mama mkwe alimuelewa mwamba kasoro bamkwe.

Laana ya Baba hua haifanyi kazi coz wakat mungine pombe ndio hua zinaongea
 
Mkuu kabla hujaachana na huyo dada hemu nitumie namba yake pm na jina lako ili nijitambulishe kama shemeji yake [emoji4]
 
Mkuu kataa kabisa unyonge wa kipumbavu. Na usijaribu kabisa kutoa million 4 kuhamisha mtu kuja kwako. Bora uwekeze milioni tatu halafu hiyo moja utafute pisi nyingine uoe. Kama huyo mzee anaendeleza itikadi za kipumbavu basi mwambie amuoe yeye huyo binti yake. Kutishiwa kurogwa sio rahisi, ni ngumu sababu wataloga baba wa mjukuu wao. Do you think what next mtoto anakua halafu aambiwe baba alirogwa na babu? Kama huyo mzee hatabadilika basi atamnyima haki mtoto wake wa kike ambae kiuhalisia anakupenda sana tu.
Ushaambiwa hao watu hawana huruma na huyo mjukuu wao.
Jamaa akizingua wanamdedisha ili binti yao aolewe.

Sasa we endelea kumpa ushujaa uchwara.
Jamaa ni mbinafsi.
 
We fala Nini unaoa mama yake au baba yake,nyie ndo mnatualibia watoto mnawazalisha na kuwaacha buladifakini Sasa ukitaka tukutoe kafara mrudishie mtoto wetu Kijijini uone.utakufa mchana kweupe

Komaa na Binti muoe Wewe Cha kufanya mpige mimba nyingine wakifka watoto watatu tu wazazi wataookea hata Laki moja.
 
Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!

Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!

Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!

Akiwa kwao mawasiliano yetu yalikuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswa mpaka dk. ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume.

Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea na maisha ya sogea tuishi.

Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka.

Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpenzi wangu.

Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nimeambatana na brother wangu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.

Brother akaniuliza, "Hivi dogo hukuona wanawake mikoa yote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu. Tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za Kiha ili mambo yasiwe magumu.

Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi, hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe, nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.

Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!

Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!

Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba na mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu, mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani.

Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k.

Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema "Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"

"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, sitaki mjadala!"

Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sana, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri."

Tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!

Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani Tsh. 500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k, sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!

Muda huo wote nina hasira vibaya mno, ila najitahidi kuificha japo mpenzi wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia. Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "Mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu," tukawaambia sawa.

Muda wa kutoka nikakuta mpenzi wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapaswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari. Akagoma, akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki kijijini tena. Nikamwambia hapana, unapaswa kubaki mpaka tumalizane na mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu, machozi yanamtoka tu!

Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "Kama mnaondoka wote nendeni tu!" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu), akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.

Basi kishingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira. Akamuita mtoto wake, akamwambia "Mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, na mimi mama naomba atusamehe tu."

Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mno, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini. Tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpenzi wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba sitokaa nirudi Kigoma, wala sitokaa nipeleke hiyo mahari waliyosema.

Nasubiri mwanangu akuekue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena.

Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyways.

dah!

Pole sana Mkuu!
 
Ushaambiwa hao watu hawana huruma na huyo mjukuu wao.
Jamaa akizingua wanamdedisha ili binti yao aolewe.

Sasa we endelea kumpa ushujaa uchwara.
Jamaa ni mbinafsi.
Hivi vitisho vya kipuuzi sana, sasa wamuue mtoto kwa sababu ya wao kutaka pesa nyingi?
Kwani kuoana ni miradi mpaka ihusishe mauaji?
Kama ndivyo walivyo inaniongezea sababu ya kuwakataa tena na kutojenga undugu na watu wa aina hii!
 
Huo sio Uanaume Kiongozi huwezi kumhukumu mpenz wako kwa tabia za Baba ake..Be a gentleman
Nakuelewa sana, lakini ndoa ni zaidi ya mke na mume! Ukiwa na wakwe wenye hulka za kishari shari utajikuta umejitwisha gunia la misumari
 
We fala Nini unaoa mama yake au baba yake,nyie ndo mnatualibia watoto mnawazalisha na kuwaacha buladifakini Sasa ukitaka tukutoe kafara mrudishie mtoto wetu Kijijini uone.utakufa mchana kweupe

Komaa na Binti muoe Wewe Cha kufanya mpige mimba nyingine wakifka watoto watatu tu wazazi wataookea hata Laki moja.
Vitisho vya kuua na kujivunia uchawi ni ujinga uliopitiliza, mkiua nyie mnaishi milele? Au pumzi yangu mnapeea nyie?

Acheni tabia za kishenzi bhana, yaani mnaanzisha ugomvi makusudi ili mupate mwanya wa kuroga? Haya rogeni sasa nipo hapa!
 
Kwa upande wangu mimi naona wewe ndio tatizo huwez kwenda kwenye mkoa mwingine bila kuja taratibu zao hasa kama waha kwa ufahamu wangu mimi na hili ni kabila langu wewe kwenda ukwen kijipatanishia mahari ya mkeo ni kosa na dharau kwa ile kwamba unaona wote ni watoto na sidhani kama kuna mkoa wenye mahari ndogo kama kigoma vijijini walikutajia mahari ili ushindwe uende ukae ujitafakari ka una wazazi uwashirikishe wewe ulivyo mpuuz na huyo mshenga wenu akajifanya anayaweza ili apate chochote tu kigoma hayo mambo ya mkaja wa mama hayana nguvu sana hata 30k wanachukua afu kwa taratibu za kiha mzazi anaozesha binti kwa mzazi mwenzie yaan ingekua ndio wameenda wazazi wa kiume wa upande wako baba zako wakubwa kwa wadogo au mababu hata kaka zako wakubwa na baadhi ya viongozi wa iman yako ya dini kwa upande wako na uko unakoenda kuoa huko ukwen kwako ndio wangewaandaa afu na uyo mshenga hakua sawa hawezi kukuambia kwamba ukimuacho mtoto atakufa anakujengea nini akilini mwako kwa unaenda kuoa familia ya wachawi wakat uyo mwanamke wako hujawahi kuyaona umuamini mshenga kwa maneno yake wakat umekaa na binti yao muda kama ni washirikina ungeaanza kuona kwa binti yao
Ndugu umri wako ila kwa jambo kubwa kama hilo la kutaka achana na fikra za ujana na huu mji wetu wa dar fanya maamuzi ya kiutu uzima hata kama wewe unapesa huwezi kujiozesha wape pesa wazazi wako waende wakatoe mahari we baki dar utapewa taarifa wakisha kamilisha kama ukiwa na baada ya muda kama miezi kadhaa nenda kaombe msamaha kwa baba mkwe wako ulimuabisha sana kwenye jamii yake hata huo mkaja wa lak 5 walikutajia ili ushindwe ujiongeze ili mlivyokua wote mapumba mkasema huku ni mbali acha tukomae liishe hatuwez kurudi kumbe ndo mnaharibu kabisaa hakuna mshenga aliewahi kupatanisha mali kama watoto mmeridhiana ikashindikana we bint kaishakuambia milioni na ndo kawambia wazazi wake waje wakuambie m5 tena kigoma vijijini mkashindwa kushtuka kwamba kuna kitu tumekosea
 
Aiseew wachangiaji ni wengi na comments zao interesting,ila kwa upande wangu mie nisingeacha mke kisa baba yake kazingua abadan asilan.
 
Back
Top Bottom