Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Akiona mahindi meno yote nje
Binadamu ni wabishii sanaa siku hiziHivyo vimiaka vyako 27 ndo unataka madogo wakuogope?
Mbona blazaako Mshana Jr na kaumri kake ka miaka 35 analelewa na majimama ya miaka 50+
Acha uchoyo mpare wahed. Toa namba hiyo kijana apate kiburudisho
Enyi watoto wadogo, wakiume, wavulana nani amewaloga?
Mmekuwaje mbona hamna hofu ya kuogopa wakinamama wakubwa waliowazidi umri mara 20000?
Mnapata wapi ujasiri huo?
story iko vile:
Jana nilipita kwenye bucha la nyama ambako huwa ninapenda kununulia hapo kwa kuwa wana nyama ya kutoka wilaya ya Ukerewe. Kwa ufupi nyama inayotokana na ng'ombe wa Ukerewe ni nzuri kwa kuwa ng'ombe wa Ukerewe wanalishwa tu maeneo jirani na nyumbani, hawajachoka na pia nyama ya Ukerewe ina ladha nzuri na ni laini. (sio tangazo za biashara mjue)
Baada ya kununua nyama, wakati nafungua mkoba kutoa hela, hako kavula kakawa kananiangalia sana, na mie nikakazia macho. Kakawa kanaonesha ishara ya kuomba namba za simu (yaani kakawa kanaweka mkono wake kwenye sikio kama vile kanapokea simu). Nilikaelewa nikakausha tu. Nikamlipa mwarabu hela yake.
Nilivyotoka hapo kuelekea kwenye usafiri, ghafla nikaona dogo yuko nyuma yangu. Mazungumzo yakaanza:
Dogo: Mama shikamoo.
Mie: Marahaba.
Dodo: huku akiwa anatoa tabasamu kama la panya, samahani mama naweza kupata namba yako ya simu.
Mie: Kwa ajili ya matumizi yepi?
Dogo: Ili niwe nakupigia kukupa taarifa za nyama inapoingia toka Ukerewe.
Mie: Mbona ratiba naijua tu, kwani ni lini niliikuja hapo nikakosa nyama?
Dogo: hahahaha, basi tuyaache hayo ya nyama, nataka tu nipate namba zako tuwe tunachat, kwa ufupi nimependa uwe mtu wangu!
Mie: Mxeeeewuu (nikaondoka zangu nikakaacha kamesimama hapo)
Mkuu huwa nakuheshimu Sana hapa jukwaaniNa kwako pia bibi. Naomba namba yako PM tafazali. Nataka nikuwozap
Hatar fayaaa mzeeKila huyu mdada akimuona tuu dogo, atakumbuka kuwa huyu anataka kunivua pichu!!, na kadri dogo atakavyo zidi kuwa jasiri kumfuata, atamvua tuu.
Mmhhhhh!Ni mtoto mdogo sana, namzaa mara elfu 10.
Ukimsumbua sana atakuendea kwa mganga, ndo hapo utakapoona kupatwa kwa nyota mkuu, act brave.Mola aniepushe na hilo balaa.
Mshana atakuloga shauri yakooHivyo vimiaka vyako 27 ndo unataka madogo wakuogope?
Mbona blazaako Mshana Jr na kaumri kake ka miaka 35 analelewa na majimama ya miaka 50+
Acha uchoyo mpare wahed. Toa namba hiyo kijana apate kiburudisho
Hapana huyo dogo ni kidukulilooooNasikitika kukuambia huyo dogo ni rikiboy.
Hivi vitoto vya siku hizi vimeshindikana kwakweli, havina adabu kabisa.
Nani kakupeni ruhusa kuweka hapa namba ya trumphahahahaha, +254 0978 987 234
Kilo ya nyama ikishafika elfu 17 utamkumbuka dogo. Mambo yako ya dharau dharau!!Enyi watoto wadogo, wakiume, wavulana nani amewaloga?