Nimetukaniwa Mzazi wangu kwa SMS, Naombeni Muongozo!

John L. Mihambo

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
526
Reaction score
177
Wakuu habari!

Nimetukaniwa Mzazi wangu, matusi ya nguoni, kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu! Aliyenitukana tupo naye mbali kijiografia. Yeye yupo mji mwingine mbali na mimi, wakati mimi nipo mkoa mwingine lakini pia kijijini kabisa!

Kwa heshima ya Mzazi wangu, naweza kutumia njia gani, yaani nianzie wapi kulingana na hii sheria mpya ya matumizi ya mitandao (Cyber Crime)?

Ahsanteni, mbarikiwe sana!
 
Haaa.. Hii sheria mpya haijakulenga mtu kama wewe Mkuu japo inaonekana hivyo.. So kokote utakapoenda utapoteza muda wako bure unless kama una le grand god father.. Msg kama hiyo angetumiwa kiongozi ndo sheria mpya inge-apply faster yaani...
 
Anyway ninavyojua mtu mpaka amporomoshee mtu mwingine matusi ya nguoni huyo anayetukanwa anakuwa kafanya jambo fulani baya mno.Pamoja na kuwa hutaki kusema kwa nini kakuporomoshea matusi mazito siri unaijua wewe.

Cybercrime kazi yake si kulinda akina chokochoko. Kama umemuanza lazima akumalize kwa kukuporomoshea matusi ya nguoni.Tena shukuru wewe labda si mtu wa Pwani, ungekuwa mtu wa Pwani ingekodiwa ngoma yenye waporomosha matusi maarufu waje wakuporomoshee matusi live na wala sio kwenye simu.
 
Hahaha, mkuu kwahiyo nimuache tu jamaa aendelee kutamba? Hii si mara yake ya kwanza ujue!
 
Kumbe mtu anaweza akafanya apendalo tu kupitia simu? Duh!
 
Hahaha, mkuu kwahiyo nimuache tu jamaa aendelee kutamba? Hii si mara yake ya kwanza ujue!

Kuna mambo matatu unaweza kufanya hapa.. Kutenga kiasi kadhaa na kwenda Polisi ambao wao kwa kuwezeshwa wataweza kumfikia huyo jamaa ambae lazima sasa ataogopa baada ya kuona Polisi wamehusishwa..

Au unaweza kuchukua matters in ur own hands.. tafuta watu wachache wakamfunze adabu kwa adabu kwa kipigo maana ni mshenzi..

Au unyamaze kimya na kuendelea kum-ignore..
 
Wakuu habari!

Nimetukaniwa Mzazi wangu, matusi ya nguoni, kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu! Aliyenitukana tupo naye mbali kijiografia. Yeye yupo mji mwingine mbali na mimi, wakati mimi nipo mkoa mwingine lakini pia kijijini kabisa!

Kwa heshima ya Mzazi wangu, naweza kutumia njia gani, yaani nianzie wapi kulingana na hii sheria mpya ya matumizi ya mitandao (Cyber Crime)?

Ahsanteni, mbarikiwe sana!

Yani from nowhere akaanza tu mitusi?? Lazima kuna tatizo kati yenu. Na huenda wewe ndio chanzo cha tatizo. Funguka usaidiwe..
 
Mtu hawezi kukutusi tu bila sababu.

kweli kabisa.....na ndo maana na mimi namwambia kuwa "The wearer of the shoe is the one who knows exactly where and how the shoe do pinches....."
 
Sidhani kama sheria mpya ya matumizi ya mitandao ya kijamii inahusikana hili suala lako na pia haijaanza kutumika...

Kama una ushahidi wa maandishi unaweza ukafungua kesi ya madai na ushahidi wako ukatumika mahakamani kama ukithibitika ni wa kweli...

Kwa kawaida huwa ni kedi ya madai na sio jinai...
 
Wakuu habari!

Nimetukaniwa Mzazi wangu, matusi ya nguoni, kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu! Aliyenitukana tupo naye mbali kijiografia. Yeye yupo mji mwingine mbali na mimi, wakati mimi nipo mkoa mwingine lakini pia kijijini kabisa!

Kwa heshima ya Mzazi wangu, naweza kutumia njia gani, yaani nianzie wapi kulingana na hii sheria mpya ya matumizi ya mitandao (Cyber Crime)?

Ahsanteni, mbarikiwe sana!
Chama gani wewe kwanza kabla hatujaanza kukusaidia
 
Nenda na hiyo massage TCRA makao makuu ....

Wewe umenena mkuu, kuna watu wanatoa ushauri mwepesi sana! Yaani mtu awe anakutumia ujumbe wa matusi ya nguoni, tena akimtukana Mzazi wako kila wakati halafu ukae kimya tu?

Siku watoto wkizisoma hizo msgs itakuaje? Well, nipe muongozo kwa mtu niliyeko porini kwasasa, TCRA hawana huduma kwa mtandao?
 
Back
Top Bottom