Nimetukaniwa Mzazi wangu kwa SMS, Naombeni Muongozo!

Nimetukaniwa Mzazi wangu kwa SMS, Naombeni Muongozo!

Matusi si ruksa ila maelezo yako naona hayajajitosheleza - mtu akutukane wewe na mzazi wako kila mara bila sababu????????!!!!!!!

Kwa tafsiri yako kama kuna sababu ama maelezo yasiyojitosheleza, mtu akikutukana kila mara hakuna tatizo! Aisee!
 
Kutoka huko atokako awatukana wazazi wako, hapana;
Ungesema zaidi kidogo.
 
Wakuu habari!

Nimetukaniwa Mzazi wangu, matusi ya nguoni, kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu! Aliyenitukana tupo naye mbali kijiografia. Yeye yupo mji mwingine mbali na mimi, wakati mimi nipo mkoa mwingine lakini pia kijijini kabisa!

Kwa heshima ya Mzazi wangu, naweza kutumia njia gani, yaani nianzie wapi kulingana na hii sheria mpya ya matumizi ya mitandao (Cyber Crime)?

Ahsanteni, mbarikiwe sana!

tafuta kituo cha polisi kilicho karibu nawe, au hata kilichokaribu naye, kafungue kesi mkuu. kuwa makini tu, kama una matatizo naye ujue utamfanya na yeye afungue kesi dhidi yako. kaeni mmalize mambo yenu, mambo mengine madogomadogo kusimamishana mahakamani ni kujipotezea muda na pesa tu!
 
Back
Top Bottom