Hajatoa sababu za match fixing! ameandika kwa mihemko, atulie na aeleze sababu zake za msingi!
Nikukumbushe tu, wengi walidhani refarii amekataa goli kwa sababu zake binafsi, VAR ingekuwepo ingekusaidieni sana! lines Man alinyoosha bendera muda mrefu sana kabla ya goli kuingia, bahati mbaya refa hakuona.
Pia, wachezaji wa Singida F. Gate walishindwa ku contain haisra zao mbele ya Refa, hii ilipelekea kucheza kwa hasira huku wakimfokea refa mara kwa mara, rejea video za Kakolanya.
Kiujimla, refa alijitahidi sana kuwa fair, na kuepusha mikanganyiko hasa katika maeneo ya hatari, rejea mpira uliyo mgonga mkononi Gadiel Michael akiwa ndani ya box, action ya wachezaji wa simba baada ya refa kukataa haikuwa ya maudhi kwa refa.
Mpira ulikuwa fair, ila saikolojia ya wachezaji wa SFG haikuwa sawa, na waliamini wameonewa, zaidi walitafuta dro ili waingie kwenye matuta, naamini walidharau uwepo wa Ally pale golini, huku histori ya simba kwa sasa katika upigaji penati ukiwa sio bora.
Je, kabla ya goli kuingia, kulikuwa na off side au haikuwepo?