Nimetuma fedha kwenda benki ya Tanzania na zimepotea!


Doh!

Afadhali umejijua wewe ndio moja wa mabenker tunao kutana nao humo kwenye macounter ya bank zetu?

Na lazima ulifeli ndio ukaishia bank maana wengi tu walipata 4 na 0 wamerudi kuanzia certificate za banking huko IFM

Mleta mada alinielewa na like akanigongea

Tumekuelewa umesikika uko kwa banking industry
 
Mwanangu ulisema ungetuma pesa ya kutosha kumbe ndo hii 150,000 za kitanzania? Au unanitania tu ila km kweli basi sipokei....
Ni mimi baba yako natumia jf pia.
 
Pole
sana. Jaribu kuulizia intermediary bank yao ni ipi? Yawezekana ni
Commerzbank ambao ndio nimesikia wameripoti tatizo ktk kufanya transfer
hivyo benki zetu zinazopitisha hela huko zimekwamishwa kwa namna moja au
nyingine. Kama sio hiyo basi endelea kufuatilia kwenye benki yako hadi
kieleweke.
 
Wakuu ahsanteni sana kwa mawazo na michango yenu mizuri ambayo imejaa nia njema tu na uwazi.

Ni hivi juzi tu nilitaarifiwa na benki yangu kwamba ile paundi 60 imerudi na haikuweza kumfikia mtumiwa, kwahio nimepata pesa yangu.

Kama nilivyosema hapo awali kwamba mimi nilikuwa nafanya majaribio kuona kama nnaweza kufanya bank transfer kwenda kwenye akaunti ya mtu yoyote pale Tanzania na ndio maana nilitumia hivyo vijisenti hiyo paundi 60.

Sasa hili suala ni muhimu sana kwa kila mtoa mada kwa sabau wengi wetu tumezoea kutumia Western Union na hatufahamu kama tunaweza siku moja kujaribu kutuma pesa kwenda kwenye benki moja kwa moja.

Western Union kwa sasa barani Ulaya wanatumia njia hii kwani mtumaji huitaji kujiunga na mtandao huo na kufanya transfer mtandaoni bila matatizo.

Sasa kwa mfano nikitaka kutuma fedha kwenda kwenye benki yoyote nyumbani tanzania iwe NMB, NBC au Stanbic si itabidi nijaze details zote husika kuanzia na anuani ya benki na anuani ya mtumiwaji,akaunti ya mtumiwaji, BIC au IBAN na SWIFT CODE.

Au tuchukulie natuma fedha kwenda benki ya AZANIA BIC yao itakuwa ni ADBCTZT1 na SWIFT CODE - AZANTZTZ je kuna masuala mengine tena yanahusika katika kumfikishia mtumiwaji pesa hata kama benki ya ughaibuni imefanya kila jitihada kutuma pesa hii?

Ila naungana kabisa na wachangiaji wengi kwamba iwe ni vijisenti tu pesa kamili iliyoshiba inabidi kutumia WESTERN UNION.
 

Mkuu watake radhi mabanker! Kama kuna teller mmoja alikuzingua usifanye ujumla wa sekta nzima. Sekta ya benki ni sekta pekee Tanzania ambayo maofisa waandamizi wote lazima wawe na viwango vinavyokubalika na msimamizi wa masuala ya fedha kwa maana Benki Kuu (BOT).
 

hahaaaaa. . . Watu mwepesi sana. kugongewa like kuna uhusiano upi na tunachozungumza? mbona hata kwangu zimegongwa nyingi tu (hata mtoa huu uzi kanigongea - lakini hii si hoja)

kwamba wewe umeandika JF doesn't make me niwe unavotaka/unavohisi.
 
Aisee, hii sio sawa ndugu. Kwasasa wire transfer ni changamoto sana, pesa inaweza kukufikia hadi baada ya miezi 3
 

Nina swali bro, mfano umetuma usd 410 , then badala ya kufika milioni inafika laki 9, hayo makato yakoje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…