Nimeuliza ChatGPT kati ya uslam na ukristo ikaleta majibu haya

Hapa umefanya selection ya Aya zinazotimiza lengo lako na ukifanya hivi lazima upotoshe hebu isikilize Surah nzima ya Al ahkaf upate ujumbe uliokusudiwa kwenye quotation yako ya mwisho
 
M M
 

Attachments

Kasome hesabu 31 uniambie upendo upi ulioandikwa kwenye biblia kuua watoto wakiume na kuoa watoto bikra
 
Vingi saana mfano kufa kwa ajili ya dhambi zenu, Yesu Mungu, kufa kwa yesu ni mengi saana
 
Vingi saana mfano kufa kwa ajili ya dhambi zenu, Yesu Mungu, kufa kwa yesu ni mengi saana

Kuhusu Yesu kufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu.

Nakujibu.
Ni somo refu ila nitafupisha.

Ukisoma torat ya Musa . (Torati na Mambo ya malawi).
Utaona Jinsi Mungu alivyomuelekeza Musa kuwaambia wana wa Israel kumtolea bwana Dhabihu na Sadaka ya kunchinja mnyama na kunyunyuzia damu madhabahuni.

Na Mara zote wana wa israel walipokuwa wakikosea .bas ile damu ya mnyama ndio inakuwa upatanisho baina yao na Mungu.

Mambo ya malawi 6:6
"Kisha ataleta sadaka yake ya hatia kwa Bwana, ni kondoo mume wa katika kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, na kumpa kuhani"

Mambo ya malawi 6:25
"Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya hiyo sadaka ya dhambi ni hii; mahali hapo pachinjwapo sadaka ya kuteketezwa ndipo itakapochinjwa sadaka ya dhambi, mbele za Bwana; ni takatifu sana."

Na hii
Waebrania 9:22
"Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo."

Kwahiyo dhambi ilikuwa haisamehewi bila damu ya mnyama. Mwanakondoo.

Swali utajiuliza .
Sasa kwanini Wakristo wanaamini Kupitia Damu ya Yesu kuna ondoleo la dhambi na sio ya mnyama?.

Tuanzie hapa
Yesu yeye mwenyewe alisema wakat anakula chakula cha mwisho na wanafunz wake, (aliwapa Divai- Wakristo tunaita meza ya bwana)
"Luka 22:20
[20]Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu."

Matendk ya mitume 26:28
"kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi."

Pia
Yohana 1:29-34
29 Kesho yake Yohana alimwona Yesu akimjia akasema, “Tazameni! Huyu ndiye Mwana-Kondoo wa Mungu anayeondoa dhambi ya ulimwengu!

30 Huyu ndiye niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi kwa maana alikuwapo kabla sijazaliwa.’ 31 Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakini nimekuja nikibatiza kwa maji kusudi apate kufahamika kwa watu wa Israeli.”

Waebrania 9:14
"basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa. Itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai"

Hitimisho:-

Ni Yesu mwenyewe ndio alisema Damu yake ni ondoleo la dhambi.
Na wanafunzi wake wakafundisha hivyo kama ambavyo Yesu alivyowaagiza.
 
Nimetumia neno "huwezi kuhangaika na hizi mambo"
Nikiwa na maana kwamba jitambue kisha fuata kile unachoamini.
Ukiamini chako inatosha,habari za kuanza kulinganisha ni dalili ya kutojiamini kwenye unachoamini.
Baki huko unakoamini na waachie wao wanakomini kufuatilia ya wengine ni dalili ya kupagawa na uoga.
BAKI NA SHUGHULIKA NA NJIA YAKO ULIYOICHAGUA WACHANA NA YA JIRANI
 
Ukitaka Ujue kuwa dini ni Ujinga na ni kichaa
Jiulize swali endapo Ingekuwa umezaliwa china au Tibet Ungelikuwa muumini wa hiyo Dini uliyo nayo !?


In short watu wengi wapo katika dini walizo nazo Kwa kurithishwa desturi ya Imani hizo kutoka Kwa wazazi wao au walezi Au Wana jamii wanao mzunguka , so it means kama ingekuwa umezaliwa china now ungekuwa na Imani tofauti na hiyo Uliyonayo Kwa kuwa china Ina watu wengi sana wasio amini katika Imani hizi za Muslim and Cristian Tibet ndio kabisaaa Hawana mpango na hizo Imani

Hapo ndio utajua kuwa dini ni mchongo ,
 
Je sheria ya kupigwa mawe haikuwa ya Mungu.
 
Dini ni imani ambayo inapatikana kwa Elimu kama Elimu zingine ndiyo maana wakatumwa Manabii
 
Sasa wewe wakati yesu anakufa msalabani wewe ulikuwa na dhambi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…