PreGE2025 Nimeumia sana chama kuvunjika na kuparaganyika siku 70+ za uongozi mpya!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwa kuwa wewe pia ulikuwa miongoni mwa hao wafuasi wa G55 (Chawa wa Mbowe), embu tuambie hapa nawe utaamua kufuata mkondo kama nyumbu kujitoa Chadema au umeamua kubakia Chadema kibishi huku ukingoja kuchinjiwa baharini maana hauna faida yoyote?
 
gentleman,
hizo ni miongoni mwa athari na hasara za kuongoza harakati za kibinafsi chini ya mwamvuli wa siasa bila kua na maono ya mbali na tathimini ya kina dhidi ya madhara, faida na hasara za agenda zisizo na tija kama vile no reform no elections, huku ukitegemea public sympathy na mitandao ya kijamii tofauti kabisa na mahitaji ya field kule ground kwa wananchi
 
Maji na mafuta havikai pamoja
 
Yericko wewe umeacha nini huko CHADEMA kwanini unang'ang'ania kama kweli chama kimeparanganyika jinsi ulivyosema?
 
Hawa viongozi walishindwa kuunga mkono uongozi mpya wakata kukigawa chama , uchaguzi ukiisha na makundi pia yanaisha , usisubiri uje kuponywa majeraha, hawa jamaa walijua Mbowe atashinda wakajiandaa kumfukuza Lissu , Lissu ameshinda wameona watakufa njaa sababu Mbowe alizoea kuwapa viposho posho vya mfukoni na kupiga madili flani
Hawa jamaa walikua na kinyongo na walijiandaa kutofanya kazi na Lissu, wangap hawakubaliani na uongozi mpya na wamebaki , hawa wana maslahi yao binafsi
 
Hao jamaa ni attention seeker waondoke tu CHADEMA wala hatutaki kuwaona, wapo pale tu kimaslahi, sasa Mbowe baada ya kupigwa chini wameona hawana chao tena, busara ilikuwa wakubaliane na Uongozi mpya au waondoke.

Wao wameamua kusepa. Its Ok
 
Chama kinaongozwa kiharakati
 
Huko ndiko kujitakasa kwenyewe
Wafia chama wa kweli ndiyo wataonekana
Biblia inasema mwenye kuvumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa
 
Inabidi G55 waungane na Covid19 kuunda chama kipya cha kuikabili CHADEMA. Au waongee na Hashim Rungwe awauzie chama chake ili wasipoteze muda kwenye usajili huku CHADEMA ikichanja mbuga. G55 na Covid19 wakiungana wataleta upinzani mkali kwa Lissu na genge lake. Pia G55 na Covid19 ni rahisi kuelewana kwa sababu vigogo wa G55 wakiwemo Salum na Kigaila wana wake/mahawara kwenye Covid19. Sisi wanaCCM tunawasihi sana G55 na kina Lissu wasiache kupasuana kadiri iwezekanavyo. Ikibidi piganeni kabisa.
 
Chama kiko imara saaΓ na sana trust me
 
Wakwende zao. Walijifanya jeuri kutaka kuivuruga chama! Wajinga sana. Chadema ni taasisi imara na itaendelea kuwepo sana tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…