PreGE2025 Nimeumia sana chama kuvunjika na kuparaganyika siku 70+ za uongozi mpya!

PreGE2025 Nimeumia sana chama kuvunjika na kuparaganyika siku 70+ za uongozi mpya!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwani mlivyosema no reform no election mlitania? Maana kama mlimaanisha je kuna mabadiliko gani ya sheria yaliyofanyika Ili twende kwenye uchaguzi?
Now mwenyekiti wa chama yupo ndani kwa kesi, je Mbowe alivyokamtwa watu mbona walipiga kelele?, mbona hatumsikii Leo akiongea chochote?
Uamuzi aliufanya yeye mbona hajatoka hadharani kusema nilimaanisha hiki. Na ni mjumbe wa Kamati kuu kwa nini asihoji kwenye kikao? Naamini Bado ana wajumbe wa kutosha kulazimisha kikao kiitishwe. Je, ameitisha kikao?
Muacheni Mbowe apumzike. Mgombea mwenza wa Lissu anakimudu vizuri tu chama chake. Watawafikisha tu katika nchi ya ahadi.
Wengi wa waliopiga kelele Mbowe alipokamatwa ndio hao wamejitoa kwenye chama.
Unataka Mbowe alazimishe kikao halafu mseme ni king'ang'anizi?
Achaneni nae. Hii ni Chadema ya Lissu sio ya Mbowe.

Amandla...
 
Mtoa mada hili si geni,hata Paulo kabla ya kuongoka na kuwa mfuasi wa Yesu alikuwa Farisayo kindakindaki!
 
umenena vyema, ni bora wakatimize ndoto zao, kwenye majukwaa mengine. tatizo hata baada ya lissu kuwa mwenyekiti still yet, timu mbowe ni kama walipooza. ni kama walishikiwa akili zao na wasitake mabadiliko.

halafu kumtuhumu lissu, ya kwamba ni mwanaharakati na sio kiongozi ni kukosa upendo. ni chuki pia. na hivyo huwezi kamwe ukawa upande wake.

kama unakumbuka ujio wa lowasa CDM, ambapo uliacha makovu kwa wafia chama mithili ya Dr slaa, suala la agenda la No reforms no election, haliwezi likawa mzigo kwako, labda kama wengi wenu mlitegemea udalali wa kisiasa ilihali mkisahau kuna damu , za wapigania vyama zinawalilia kwa tamaa zenu....kuna watu wamekufa kwa ajili ya chama wakifufuka na kuwakuta mnataka kutumia njia zile ili kujinasua watalia sana.
 
Inabidi G55 waungane na Covid19 kuunda chama kipya cha kuikabili CHADEMA. Au waongee na Hashim Rungwe awauzie chama chake ili wasipoteze muda kwenye usajili huku CHADEMA ikichanja mbuga. G55 na Covid19 wakiungana wataleta upinzani mkali kwa Lissu na genge lake. Pia G55 na Covid19 ni rahisi kuelewana kwa sababu vigogo wa G55 wakiwemo Salum na Kigaila wana wake/mahawara kwenye Covid19. Sisi wanaCCM tunawasihi sana G55 na kina Lissu wasiache kupasuana kadiri iwezekanavyo. Ikibidi piganeni kabisa.
Una Kifua?
 
Ni video ya dakika moja na sekunde 45

Pia usisite kusoma 👎🤗

Nimeumia sana, imenichukua masaa kadhaa kusema chochote baada ya uamuzi huu mgumu wa waliokuwa viongozi wakuu wa Chama changu Chadema Naibu Katibu Mkuu Bara Mh Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mh Salumu Mwalimu na Waliokuwa wajumbe wa Sekretaieti yote ya Chama kujivua uanachama wa Chadema.

Nimeumia kwasababu tatizo hili uongozi mpya umeshindwa kulitibu tangu uchaguzi ulipomalizika, Tulishauri uongozi mpya uwaunganishe wanachama waliogawanyika baada ya Uchaguzi, Lakini walioshinda wakakomaza mafuvu na kutupuuza, wakatuita tuna madonda ya uchaguzi hayajapona kisha tukaitwa wasaliti na mwisho tukaitwa maccm. Haya ndio yametufikisha hapa.

Katika siasa lolote linatokea, huu ndio utofauti wa siasa na harakati, Mwanasiasa anafikiria kushika madaraka ili afanye mageuzi ya sheria na mifumo mbali mbalimbali ya kijamii. Wakati huo Mwanaharakati anafikiria kuhimiza mageuzi ya sheria na mifumo mbalimbali ya kijamii, Yaani mwanaharakati hafikirii kuitoa ccm madarakani bali kuishinikiza ccm ifanye mageuzi ya sheria na mifumo ya kijamii tu, Kwamba ccm ikitekeleza madai hayo, basi mwanasiasa huyo anaweza kuhamia tu katika madai mengine mfano haki ya wanafunzi wa kike kupewa taulo za kike, Haki ya wanaume kupata unyumba kwa wake zao, nk. Hii ndio tofauti kuu.

Ninawapongeza viongozi hawa kwa uamuzi wao ili wakatimize ndoto zao katika majukwaa mengine kwakuwa jukwa lako walilolijenga kwa maisha yao likawa jukwaa pendwa kwa umma limeharibiwa na wanaona linaenda shimoni. Vyama vya siasa ni vyama vya hiyari, ukiona hapa wenzio hawakutaki basi unatafuta jukwaa lingine.

Niwatakie mapambano mema huko waendako, Mimi nitapambana ndani ya Chadema ili kujaribu kukirejesha chama kwenye misngi yake na kuhakikisha chama kinafuata katiba na miongozo yake, Na kurejesha umoja na mshikamano uliojengwa kwa miaka mingi.

Nimeumia sana chama changu kuvunjika na kuparaganyika siku 70+ tu za uongozi mpya!😭😭😭😭

WE SHALL WIN!

Na Yericko Nyerere

View attachment 3327116

Hata kina Tlaatlaah mmeumia nao.
 
Shut Up! Mamluki wee

Kila nilipotaka kungatuka,wapambe, washauri na watu wangu wa karibu, waliniambia,hapana Mwalimu watu wengi bado wanakuhitaji.
Kumbe baadae nikagundua wao ndio walikuwa wananihitaji,ili kujiakikishia kesho yao.
 
Yericco Nyerere ungetuambia kwanza ni wapi Chadema ilipotoka kwenye misingi yake alikadhalika ni wapi ambapo katiba ya chama haijafutwa tofauti na hapo utakua unaimba kidalipoo.
Nyie si ndio mliasisi "hakuna kuama chama"?
Naomba utuhainishie hayo maeneo mawili ili tukuelewe.
Kwani environment za mwenyekiti Mbowe Chadema haikuwahi kuondokewa na wanachama na viongozi waansamizi, kwani chama kiliparaganyika?
 
hawa washenzi wangekuwa madarakani tungeshudia umwagaji damu wa hovyo sana, na hii nchi ingeparanganyika zaidi ya somalia
 
Back
Top Bottom