Nimeumia sana na sijafurahishwa na ushindi wa Tundu Lissu

Nimeumia sana na sijafurahishwa na ushindi wa Tundu Lissu

Ndugu zangu Watanzania,

Uchaguzi wa CHADEMA umemalizika Rasmi kwa Tundu Lissu Kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Sanjali na John Heche Kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wake.

Ushindi huo umeniumiza,kunisikitisha ,kunihuzunisha na kunisononesha sana. Ni ushindi ambao unaiweka CHADEMA katika hatari ya kusambaratika,ni ushindi ambao utapelekea kupoteza wanachama wengi kutokana na misuguano ya ndani kwa ndani. Ni ushindi ambao haukustahili kuelekea Mikononi Mwa watu kariba ya lissu na Heche.

Hao watu wana midomo michafu sana,ni wabaguzi sana na wenye mioyo iliyo jaa sumu ya chuki kubwa sana vifuani pao. Mimi binafsi namchukia sana Lissu siyo kwa sababu yupo CHADEMA nami nipo CCM. namchukia Lissu kwa sababu ya mdomo wake Mchafu na wa Uropokaji.

Mdomo wa Lissu mara nyingi umetumika kuchochea sana na kupandikiza chuki ,uhasama na ubaguzi hapa Nchini.Ameutumia Mdomo wake bila Breki kumtukana na kumbagua Rais wetu. Kiasili mimi sipendi mtu mbaguzi na mwenye chuki kama aliyonayo lissu kifuani pake.

Sijawahi kufurahishwa wala kupenda namna lissu alivyokuwa akimdhalilisha Rais wetu majukwaani kwa sababu ya Uzanzibari wake na uwanamke wake. Kwa sababu mimi naamini uongozi au kiongozi bora na mzuri siyo suala la jinsia bali ni uwezo wa mtu binafsi na kipawa na Karama aliyo jaaliwa na Mungu kiuongozi.

Lakini sote ni mashahidi wa namna lissu ambavyo alikuwa akimbagua Rais wetu kwa kusema huyu ni Mzanzibari na hana uchungu Taifa hili na kauli nyingine mbalimbali za kutweza utu wa Rais wetu. Sasa mtu wa aina hii na mwenye mawazo ya kibaguzi hataishia kumbagua Rais wetu tu ambaye anajua fika ni Mtanzania na mwenye haki zote za kitanzania.

Mdomo wa Lissu unanifanya nimchukue kwa sababu najua atafanya kazi ya kueneza chuki ,ubaguzi,fitina ,marumbano yasiyo na tija pamoja na kuhatarisha usalama wa Taifa letu. Kwa sababu yeye ni mtu ambaye akili yake anaijua Mwenyewe na inavyomuongoza.

Lakini mimi niseme tu kuwa ni aidha akubali njia ya maridhiano ambayo Mheshimiwa Mbowe alikuwa ameiongoza. Kwa sababu siasa za jino kwa jino hataziweza na itakuwa ni ngumu sana kuziendesha hapa Nchini. Ni siasa ambazo zimeumiza wengi,kuwaacha wengi na vilema,kuwafanya wengi kupoteza maisha,masomo,ajira ,kupoteza marafiki na hata wengine kupoteza kabisa muelekeo mpaka leo hii hususani kundi la vijana.

Hivyo asifikirie kuwa siasa za muundo huo na zenye misimamo mikali zitafanikiwa hapa Nchini. Hakuna anayeweza kuandamana mbele ya polisi ambao wamepiga marufuku jambo fulani kufanyika. na wala hakuna atakayekuwa tayari kuhatarisha usalama wake na Maisha yake barabarani. katika hilo namuhakikishia kuwa hatafanikiwa hata kidogo.

Isitoshe watanzania wa sasa wanatambua ya kuwa wapinzani wa Tanzania wanaongozwa na matumbo yao tu yaani uchumia tumbo tu. Kwa sasa upinzani hauaminiki hata kidogo kwa wananchi maana wanajua ni vigeugeu tu. kwa hiyo Lissu akitaka aendeshe siasa za kibabe basi ataishia kuumia tu. kwa sababu vyombo vyetu vya ulinzi hususani jeshi la polisi halitakuwa tayari kuona chama au mtu fulani anataka kuleta na kuchochea uasi hapa Nchini.

CHADEMA wamepoteza chaguo sahihi na kuchagua mtu asiye stahili kuiongoza CHADEMA. Najua mnafuraha ya muda mfupi kwa baadhi yenu. Ila mtalia sana na kumkumbuka mbowe Mwamba na Jabali la siasa za upinzani hapa Nchini. Muda ni Mwalimu mzuri sana.Ngoja tuupe muda nafasi ili uwapeni majibu . Siku yaja ambapo mtalia na kububujikwa na machozi ya huzuni na kumkumbuka sana Mheshimiwa Mbowe.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Poleni sana Wana CCM kwa msiba uliowapata
 
Wewe kidampa kweli hujitambui ukishapewa mada hujifikirishi unatupa gazeti humu.

Lissu anambaguaje Samia ambaye kweli ni mzanzibari mwenye kitambulisho cha mzanzibari mkaazi hapo pichani ambacho wewe na Lissu hamna hicho kitambulisho sababu sio wazanzibari?

Kisha wewe unaumia nini watu wakiondoka Chadema au ikisambaratika wakati wewe sio mwanachama au mfuasi wa Chadema bali ni kidampa huko Lumumba?

Jipange upya na CCM mfanye uchaguzi kura zipigwe live na watu wahesabu mbele ya camera sio yenu hiyo Samia anajichapishia fomu moja na kujiteua kuwa mgombea urais na nyie mnainamisha vichwa chini na kusema zidumu fikra za mwenyekiti.

Lissu na wewe hamuwezi kupata hata hatua mbili za ardhi Zanzibar ila Samia anapata mahekari Tanganyika na Zanzibar sasa hapo kabaguliwa nani?
images - 2025-01-22T172535.978.jpeg
 
Hata mimi kiongozi, mbowe alikuwa anatosha kabisa .. kwani siasa zetu zinahitaji mpinzani dizaini ya Mbowe .. 4R
 
CHama kinaenda kufa , kuendesha chama kinahitaji fedha.

Mbowe kashaachana nacho anaenda kusimamai biashara zake.

Mbowe alikuwa anawawezesha baadhi ya makada kufanya siasa ila mnyaturu hawezi ,wengi watakimbia.
Haahaa binafsi nilikuwa naomba Sana mbowe ashindwe huu uchaguzi, chama kuendeshwa na mtu mmoja kipesa sio sawa.Leo chadema imekombola
 
chrome_screenshot_22 Dec 2024 12_26_57 GMT+03_00.png

Wewe kidampa risiti zako zipo kuhusu Mbowe huyu huyu unayejidai umeumizwa kuondolewa kwake ni mwaka jana tu uliandika hafai kuendelea kuwa mwenyekiti ulivyokuwa kidampa msahaulifu ukadhani wote humu wasahaulifu kama wewe.
 
CHama kinaenda kufa , kuendesha chama kinahitaji fedha.

Mbowe kashaachana nacho anaenda kusimamai biashara zake.

Mbowe alikuwa anawawezesha baadhi ya makada kufanya siasa ila mnyaturu hawezi ,wengi watakimbia.
HIko ndio mmebaki nacho? Ruzuku huwa zinakwenda wapi?
 
Wajumbe wa mkutano mkuu wa CHADEMA hawana tofauti na wayahudi walioona ni bora mhalifu Baraba aachiwe ili Messiah Yesu asulubiwe. Watajutia mno.
ni dhihaka kwa Mungu kumfananisha mwanasiasa na Yesu, Yesu kristo alijitoa sadaka voluntary , wanasiasa wa bongo hakuna hata mmoja amedhubutu kuweka uhai wake on the line. Have some respect
 
Back
Top Bottom