Nimeunga mita mpya ya maji lakini inaonesha nimetumia unit 2

madunda boy

Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
25
Reaction score
12
Jana nimefunga mita ya maji yaani maunganisho mapya kwa mara ya kwanza. Cha ajabu na cha kushangaza mita inaonesha nimetumia unit mbili.

Sasa nikamuuliza fundi kuwa hizo unit 2 zimetokea wapi wakati mita ni mpya..Akanijibu kuwa hizo unit 2 ni yale maji yaliyokuwa yanamwagika wakati wanatest bomba, nika choka.

Kama unit moja ni sawa na lita 1000 ambazo ni sawa na debe 20.

Kwa maana hiyo ndani ya daki kama 20 tu maji yametumika lita 2000.

Kuna shida kwenye hizi mita Nawasilisha hoja
 
Kama haukuripoti utazilipa, wanachofanya wanachukua mita wanaitumia kujaza matenki kwa aliyekatiwa maji kisha wanapata chao na wanakuja kukufungia wewe na deni juu.
 
Maji kutiririka dakika 20 mfululizo ni mengi sana kusema kweli japo haiwezi kufika unit 2 ila moja itapitiliza.
 
Nadhani unakumbuka tulifundishwa zile hesabu za kwenda na moja kichwani,Basi hapo ndipo Muda wake.
 
Yani hapo huna jinsi utalipa tuu na ukigoma wanakukatia huduma
 
Kama haukuripoti utazilipa, wanachofanya wanachukua mita wanaitumia kujaza matenki kwa aliyekatiwa maji kisha wanapata chao na wanakuja kukufungia wewe na deni juu.
Hii umetolea wapi? Yaani mtu akitaka kuiba maji kwanza afungue bomba halafu afunge mita ndo aibe maji?
Kwa nini asiibe tu pale baada ya kufungua bomba na maji yanamwagika aanze kufunga mita ya nn tena!?
 
Mita zao nahisi hazipo sawa, sidhani Kama nikweli Unit moja sawa na ndoo hamsini Kama wanavyosema!
 
Hii umetolea wapi? Yaani mtu akitaka kuiba maji kwanza afungue bomba halafu afunge mita ndo aibe maji?
Kwa nini asiibe tu pale baada ya kufungua bomba na maji yanamwagika aanze kufunga mita ya nn tena!?
Fundi wa shirika anajua waliokatiwa maji, anakuja na mita anaifunga anakujazia maji kisha anarudisha mita yako na wewe unampa chake anaondoka, kwa mafundi kila kitu dili.
Mita mpya hizo uniti mbili zimeigiaje wakati kujaza uniti moja inaweza kuwa saa moja, hao mafundi walimwaga maji kwa saa mbili! Haiwezekani, na ni wapi walikomwaga maji hayo.
 
Duh lita 1000 kwenu mnatumia 1hr kujaza mbona mnamaji yenye kaso ndogo sana au ni mimi ndio sijaelewa ulichoandika?
 
Alafu unit 2 ndio mpka muanzishe uzi mnalalamika kama deni litakuja 1m duh na hapo demu akikuomba 10k unaitoa kama zuzu vile
 
Inawezekana umekosea kusoma, wewe umesoma lita za ujazo ndio unahisi ni mita za ujazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…