Nimeuziwa mbwa maeneo ya Victoria, nilipomfikisha nyumbani mume wangu akasema eti sio mbwa ni fisi

Nimeuziwa mbwa maeneo ya Victoria, nilipomfikisha nyumbani mume wangu akasema eti sio mbwa ni fisi

Jemima Mrembo

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
2,864
Reaction score
8,328
images (23).jpeg
Jana jioni nilipokuwa nikitoka kazini, nikafika Victoria, nikakuta kuna jamaa ana mbwa watatu, wawili wakubwa na puppy mmoja.

Nikavutiwa na puppy nikaenda naye nyumbani. Mume wangu alirudi akiwa amechoka na amepiga mambo yake, lakini nilimjulisha kuwa nimenunua mbwa.

Asubuhi ya leo akaenda kumwangalia, nilikuwa nimemuweka garage sababu bado hatujapata kibanda chake. Nikashangaa mtu ananiita kwa hasira ananizodoa kuwa sina akili kabisa, nimeletaje fisi nyumbani?

Kwa kweli mimi wakati namnunua nilifurahia umbo lake alivyonona, sikujua fisi kuwa wako kama mbwa. Lakini pia nadhani nilirogwa.
 
Back
Top Bottom