Jemima Mrembo
JF-Expert Member
- Jul 19, 2021
- 2,864
- 8,328
Nikavutiwa na puppy nikaenda naye nyumbani. Mume wangu alirudi akiwa amechoka na amepiga mambo yake, lakini nilimjulisha kuwa nimenunua mbwa.
Asubuhi ya leo akaenda kumwangalia, nilikuwa nimemuweka garage sababu bado hatujapata kibanda chake. Nikashangaa mtu ananiita kwa hasira ananizodoa kuwa sina akili kabisa, nimeletaje fisi nyumbani?
Kwa kweli mimi wakati namnunua nilifurahia umbo lake alivyonona, sikujua fisi kuwa wako kama mbwa. Lakini pia nadhani nilirogwa.