Nimevumilia nimeshindwa, amerudi amelewa na hana nguo hata moja

Nimevumilia nimeshindwa, amerudi amelewa na hana nguo hata moja

Salaam,

Jamani nasumbuliwa na shemeji yenu ndoa hii ina tabu sana nimevumilia mpaka nimeona leo niwashikishe mke huyu anavuta ugoro, pariki, mlevi wa pombe na kikojozi choo kipo ndani yeye anatumia ndoo na siku nyingine anajisaidia bila kujua kwa ulevi.

Nilijaribu kuwaita ndugu na jamaa kuomba msamaha na kusema harudii, siku nyingine akitoka amevaa chupi harudi nayo mi navumilia mpaka niliamua kuwacha mlango wazi ili asinisumbue kugonga.

Sasa kali ni jana amerudi amelala ukumbini nguo hata moja hana na ananuka choo mpaka muda huu naona watoto pia hawajatoka vyumbani kwa kuogopa fedhea nahisi walitoka wakamuona mama yao, hii ni safari namrudisha Makete nimechoka wadau.

Uvumilivu umenishinda

Mjadala ww ndio utakuwa na matatizo sio Shemeji yetu
 
Back
Top Bottom