Nimevumilia sana ila leo imebidi niulize, hivi mtu anakupaje msaada wa Trilioni 1.5 wakati nchini kwake kuna watu wanalala nje na kufa njaa?

Nimevumilia sana ila leo imebidi niulize, hivi mtu anakupaje msaada wa Trilioni 1.5 wakati nchini kwake kuna watu wanalala nje na kufa njaa?

Misaada yote huwa ina masharti yake.
Unakuta zaidi ya nusu ya pesa ya msaada inarudi ilipotoka

Maana ukipewa pesa utalazimishwaa kinunua bidhaa zote kutoka kwa aliyetoa. Wakandarasi wa miradi lazima watoke kwao. Mwisho wa siku unakuja kulipa deni na riba juu.

Mfano unakumbuka mradi wa SGR, exim bank walikataa kutoa mkopo baada ya wakandarasi kutoka china kipigwa chini

Hakina kitu cha bure. Wale wanafanya kutengeneza ajira za watu wao kupitia misaada/mikopo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee, ni kama msaada wa Tazara flyover toka Japan na SUMITOMO ya Japan ikala tenda, pesa yote ikarudi kwao..
 
Nimekuwa najiuliza sana hili swali bila majibu ya uhakika, hivi haya mataifa yanayojiita donor countries, huwa wanatupa hii misaada kwa misingi na madhumuni yapi hasa?

Na kwanini wanapotupa misaada huwa tunasainishana mikataba ya msaada? hivi huo ni msaada au tunawauzia kitu hadi tusainishane? Whats happening?
Tanzania ilitoa msaada wa chakula kwa nchi fulani hapa afrika ilihali nchini kwake kuna watanzania hawana chakula!! Je huo msaada ulikua wa maana gani wakati wananchi wake hawana chakula?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania ilitoa msaada wa chakula kwa nchi fulani hapa afrika ilihali nchini kwake kuna watanzania hawana chakula!! Je huo msaada ulikua wa maana gani wakati wananchi wake hawana chakula?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo pesa yote inarudi kupitia cargo zao wanazopitishia bandari ya Dar es salaam, ile ilikuwa kama hongo tu waendelee kututajirisha kwa kupitishia mizigi Dar..
 
Unaweza kumlisha mchepuko chips kuku huku wanao na mkeo wanalala njaa/kula ugali chumvi..kuna kitu utakuwa umekilenga kwa mchepuko na sio kwamba unampa fervor pekee[emoji125][emoji125]

Sent using Jamii Forums mobile app
Misaada ni kama chambo. Utavutwa na hiyo misaada lakini baadae utaliwa kwa njia moja au nyingine. Alituasa Mwalimu "mikopo na misaada inahatarisha Uhuru wetu, utashindwa kutoa maoni yako kwa kuogopa kunyimwa hiyo misaada na mikopo."
 
Unapewa hela ya kuinua sekta ya elimu, kwa mfano, hivyo lazima mkubaliane huo msaada utakuwa na manufaa gani kwenye elimu na jinsi utakavyowafikia walengwa.
Tatizo ni walipa kodi wa nchi inayokupa msaada. Huwa hawataki pesa ziende kwa taifa linalokinzana na sera zao.
 
Unakuja kulia njaa uwalishe wanao, nakupa halafu nakukuta uko na totoz bar huku ukiagiza kama mlivyo
Huko nyumbani bado shida ni ile ile
Unafikiri nitajisikiaje mtoaji?

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Hawakusaidii. Kwanza wanaangalia fursa zao kwako halafu wanakuja kwa gea ya kukusaidia ili kufungua zile fursa.
 
Kwahiyo sisi Tz ni kama mchepuko anaelishwa burger na pizza huku nyumbani kwao wanashindia ugali tembele, ila baadae mchepuko kuna cha moto anakipata.., sivyo?

Wakati wa kudaiwa, hata mtoto mdogo wa kike anapewa MME.

Je, ndiyo huo utaratibu Watanzania tumeukubali au tunalazimishwa kukubali?
 
Misaada ni ya kimkakati.
Mfano misaada sekta ya afya.Fikiria nchi mna uhusiano,mmewekeza miradi yenu huko,mna watu wenu wanasafiri kwenda huko,vipi ukitokea mliupuko wa magonjwa kama Ebola?

Unadhani misaada ijapo unapewa wewe haina msaada kwa watu katika mapana yake?

Mfano unapewa msaada wa kuimarisha nishati mfano Umeme wa sola au hata wa kawaida.Unadhani hawajui athari za matumizi ya kuni na mkaa kwa misitu na vyanzo vya maji?

Mwisho nashauri muwe mnafikiria kabla ya kutuhumu wanaowapa misaada,kwani hujawahi kutoa msaada kwa mtu baki ingawa kwenye ukoo wenu kuna mtu ana hali mbaya hujawahi kumsaidia?

Hawa watu hata nyoka akiugua au mnyama anatibiwa na kurudishwa porini.Sasa kama mnyama anatibiwa kwa nini wasitoe msaada kwa binadamu wenzao wanaohitaji?

Hata hapa kwetu kuna mtu analisha mbwa kwa bajeti ya shilingi laki 6 kwa mwezi wakati kuna mtu ana mshahara wa laki 3 na anatunza familia ya watu wanne.

Kazi ya kichwa ni kufikiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom