Nimevuruga kikao cha watu, hakuna ndoa tena

Nimevuruga kikao cha watu, hakuna ndoa tena

Jokajeusi

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2018
Posts
6,323
Reaction score
10,813
Wakuu kwema!

Jana jumamosi nilikuwepo kwenye Kikao kilichofanyika Tegeta Tangibovu.

Kikao kilimhusu mtoto wa Baba Mkubwa, ambaye kiumri anamiaka 29 nikiwa nimemzidi miaka Kama sita hivi.

Mtoto wa Baba mkubwa ambaye jina lake linaanzia na herufi J, miezi minne iliyopita yaani mwezi wa tatu, alitoa Posa Kwa binti mmoja mwenye asili ya Dodoma.
Baada ya kutoa mahari, ndoa ilipangwa ifungwe mwezi wa Tisa tarehe 27.

Michango ilichangwa, wanandugu na watu wa karibu tuliambiwa tuchangie 100,000 Kwa single na 150,000 Kwa double.
Michango ilianza Rasmi mwezi wa sita. Na 70% wamechanga .

Mwezi Saba Mwanzoni J alinipigia simu akitaka tuonane.
Tukapanga siku tukaonana pale Ubungo Plaza,
Akanieleza jinsi alivyochanganywa na mchumba wake baada ya kuzifumania SMS za hovyo za mapenzi kwenye simu ya mchumba wake.
Kwa mujibu WA maelezo yake ni kuwa Mchumba wake anamegwa na huyo msela ambaye ni mwajiriwa katika Benk Maarufu hapa Nchini.

Nikamuuliza, alivyoongea na mchumba wake ikawaje,
Akanijibu kuwa Mchumba wake alikuwa mkali Kama mbogo.

Nilikamuuliza swali la lazima ambalo wengi wanaoniombaga ushauri huwa nawauliza.
"ulimkuta Bikra huyo mchumba wako?"
Akanijibu hapana.

Nikamwambia Piga chini wala usijishauri na wala usisubiri nikushauri zaidi.

Fukuza, mwambie umeghairi kumuoa.
Akaniambia, lakini bado anampenda, nikamwambia Kama unampenda ulichoniitia ni kitu gani Kama sio upumbavu wake.

Nikamtolea mifano ya ndugu niliowashauri wakavunja Uchumba usio na mbele Wala nyuma na sasa wanafurahia maisha Kama jokajeusi.

Akanambia atafikiria. Nikamwambia asiniite tena mpaka atakapokuwa amempiga chini. Tukapotezana Kwa wiki mbili hivi.
Mwanzo mwa wiki iliyopita mambo yalikuwa mabaya Sana.

Mwanamke anamuomba msamaha, vikao vimekuwa vingi sasa dogo anazidiwa ushawishi na pande zote mbili. Wote wanamshauri amuoe.
J aliwaambia Baba Mkubwa hataki kumuoa mchumba wake na hakuwaambia ukweli wote, isipokuwa alitoa sababu za kawaida.

Sasa ijumaa Dogo akanambia ananiomba kwenye kikao cha jumamosi ambayo ni Jana.
Ili nimuunge Mkono kwenye msimamo wake.

Jana kwenye kikao,
Nimechafua upepo, nimeeleza kila kitu,

Nikamuuliza mchumba wake J,
"Unafikiri ni Kwa nini unastahili kuolewa na J na sio mwanamke mwingine?"
Akanijibu Kwa sababu anampenda na anatabia njema.

Nikamuuliza,
"Ni kipi unamaanisha ukisema unatabia njema?"
Akajibu kuwa atamheshimu na kumsikiliza.

Nikamuuliza,
"Kwa mfano J akasema anatafuta mwanamke mwenye bikra Kama ishara ya tabia njema Kwa mwanamke, je utakuwa nayo hiyo bikra?"

Hapo nikamuona Shemeji yangu akijaa upepo, amepaniki, kikao kikaingiliwa na wakubwa upande huu na upande huu wakilipinga swali langu kumstahi binti wa watu.

Mwisho nikasema,
Binti huyu atamsumbua kijana wetu. Hajaolewa, mchakato wa Harusi yake na ndugu yetu unaendelea yeye analala na wanaume wengine.

Kama ningekuwa ni amri yangu, basi hapa hakuna Harusi,
Baada ya hapo James akaniunga Mkono tukatoka tukiacha wametahamaki huku Mchumba wake J akitufuata nyuma akimlilia James.

Bikra Matters
 
Wakuu kwema!

Jana jumamosi nilikuwepo kwenye Kikao kilichofanyika Tegeta Tangibovu.

Kikao kilimhusu mtoto wa Baba Mkubwa, ambaye kiumri anamiaka 29 nikiwa nimemzidi miaka Kama sita hivi.

Mtoto wa Baba mkubwa ambaye jina lake linaanzia na herufi J, miezi minne iliyopita yaani mwezi wa tatu, alitoa Posa Kwa binti mmoja mwenye asili ya Dodoma.
Umeanza na jina linaanziwa name J baadae umenogewa kutuambia ni James

Ila hata ukiachana na mambo ya Bikra. Hakuna ndoa hapo......mapema sana kakunjua makucha tayari huyo mgogo/mrangi
 
Wakuu kwema!

Jana jumamosi nilikuwepo kwenye Kikao kilichofanyika Tegeta Tangibovu.

Kikao kilimhusu mtoto wa Baba Mkubwa, ambaye kiumri anamiaka 29 nikiwa nimemzidi miaka Kama sita hivi.

Ushauri mzuri sana huu japo kwa upande wa mwanamke unaumiza, ila atajifunza na atatulia kwenye ndoa yake hata akija Kuwa na mwanaume mwingine huko mbeleni hata kama afanye kosa kama hili kamwe
 
Wataoana. Trust me. Na wewe utakuwa adui yao namba moja. Usipende kujihusisha na mambo ya watu wawili hadharani hasa wenye akili za kitoto kama huyo mdogo wako


Sijawazuia kuoana.

Uzoefu wangu unaonyesha wengi walioomba ushauri kwangu waliwaacha wenza wao moja Kwa moja na sasa wameoa wake wema sio vichomi
 
Naona jokajeusi anataka 100,000 yake ya mchango irudi tu. [emoji1787][emoji1787] lakini ukweli usemwe akiliwa wakati wa uchumba mbususu ujuwe akiwa kwenye ndoa mbususu itachakazwa.


Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]


Mnirudishie pesa yangu niagize Chanjo Mimi ya Uingereza
 
Back
Top Bottom