Kama mnavyojua ndugu zangu sisi ni wanyong mpaka pale sisiemu itakapotoka madarakani.
Hivyo maisha yetu ni ya kuunga unga na kusaidian ili siku zisonge.
Na mtu pekee wa kukuinua ni mwanafamilia mwenzako Dada au Kaka. Mimi nilimaliza masomo baada ya kuhangaikiwa sana na Dada yangu na Kaka Yangu waliokuwa wanafanya kazi za Ndani. Hatimaye nikayakwaa majiwe kadhaa ya Elimu.
Baada ya kuyakwaa majiwe ikabidi na mimi nianze sasa kuinua waliobaki nyuma. Ila sasa maji yamezidi Unga. Nahitaji msada. Hivi kwa Tanzania hii unaweza kusomesha watu watano kwa mpigo vyuoni?
Basi tukasonga mbele kama familia hatimaye tukainuka......sasa watu kadhaa wana vipato vizuri tu. Alhamdullilah.
Tuna kesi tatu kwa pamoja.
1. Dogo yuko chuo anasoma
2. Nyumba imejwngwa bado finishing
3. Kaka anafunga ndoa.
Mimi kwenye kikao cha wanafamilia nimewambia hizi fedha badala ya kuchangia harusi tuchange kwa ajili ya Dogo masomoni na Tumalizie nyumba ya familia( Family house kwa maana ya family house).
Wamefura.
Hii imenishangaza ni sawa na washkaji zangu unakuta anachangia harudi laki tatu huku Mama yake kijijini anaumwa anamtumia elfu 20.
Wafrika tubadilike. Maendeleo ni sisi wenyewe.
Mkuu,
Nilichogundua katika maisha haya ni kwamba, akili nyingi ni mzigo pia.
Yani unaweza kuwa na akili zaidi ya wenzako halafu hiyo akili ikawa mzigo, wenzako hawakuelewi, na wakija kukuelewa unayosema leo, inawachukua miaka 20.
Michango ya harusi za kifahari kushinda uwezo wa kawaida wa watu ni shobo tu za kijamii za kutaka kujionesha kuwa "na sisi tumo". Lakini hazina tija.
Mimi nilikataa ujinga huu. Ila familia zinakuwa na changamoto sana.
Kuna wakati aunt mmoja alikuwa anaozesha mtoto wake. Anti mtu fulani wa kupenda harusi za fahari sana, alikuwa anataka kukodisha ukumbi wa Mlimani City, enzi hizo ndiyo unaanzishwa tu.
Mimi mchango nililipa, ila aunt akaja kwangu anasema anataka kukopa a few thousand US dollars kukamilisha harusi, atanilipa. Mimi nikajua hapa nikitoa imeenda hii. Ila kwa heshima nikampa, alisema anataka kuwa mtu wa kwanza kanisani kwetu kufanya harusi hapo Mlimani City, apparently that was so important for her status.
Nikasema huyu aunt wangu, kanipitisha machaka mengi sana wakati naanza maisha, najua hii hela hawezi kunilipa, lakini si kitu, ngoja nione.
Nikampa zile hela, I think it was about $3,000. Hapo nishachangachanga sana na kununua nunua sana nguo za New York kutuma kwenye harusi.
Kama nilivyotabiri, harusi ikaisha na habari ikaishia hapohapo.
Ila haikuwa issue sana kwangu kwa sababu nilijua tangu awali kwamba hii hairudi. Na yule cousin aliyekuwa anaoa ni mtu wangu sana. Nikaona hii shughuli ya nyumbani siipigii hesabu.
Ningetegemea pesa irudi ingekuwa tabu.
Mara nyingine hawa watu unamalizana nao kulinda mahusiano tu, halafu unafanya mambo mengine kivyako.