Economist amezungumzia watalii, sio wananchi wote. Wananchi wengi wa Marekani hawana habari na nchi yeyote iliyokuwa nje ya mipaka yao isipokuwa zile ambazo wana uhusiano nazo au ziko karibu nao. Ndio maana wengi wenye asili ya ulaya wanapendelea kwenda Ulaya, weusi wanaenda Caribbean na walio kwenye mipaka ya kusini Mexico. Hawa hata uwaambie vipi hawatakuja Tanzania. Watalii anaozungumzia Economist ni wale ambao wanapendelea kutembelea nchi geni. Hawa ni wadadisi. Hawa wanafanya utafiti kabla ya kuchagua wapi kwa kwenda. Wanaangalia website za tour companies. Wanauliza wenzao kuhusu experiences zao. Vijana wanaangalia blogs za vijana wenzao ambao wanasafiri au waliowahi kuishi nje ya nchi. Ni wachache sana watafanya uamuzi kwa sababu wamemuona Rais wa Tanzania PBS na sasa wanajua Kilimanjaro iko Tanzania. Hivi unaamini mtalii mwenye nia ya kupanda mlima Kilimanjaro atakuwa hajui kuwa uko Tanzania?
Seychelles, Mauritius, Maldives na Botswana zina booming tourism industry. Na wamefanikiwa kwa kutumia private sector na sio serikali. Sisi hatuzijui nchi hizi kwa sababu dhana ya utalii ni ngeni kwetu. Watanzania wengi wanaenda China, lakini sidhani kama hata wanajua kuna Great Wall kule.
Serikali inatakiwa kuweka mazingira mazuri ya private sekta kushamiri, wao wataleta watalii!
Amandla...