Nimewashangaa sana Lissu na Heche baada ya kusikiliza mjadala wa Royal Tour kwenye Club House ya Maria Sarungi


Hivi billion 9 kwa dakika 56 na billion 9 kuwaempower vijana kipi Cha Msingi?
 
Nanukuu;
"Akatema pumba siyo za Nchi hii!"
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwenye club house wanapaswa kualika watalamu wawili wa jambo husika Lisu na Heche hawajui kiwanda cha utalii hata kwa asilimia 2
 
Hivi billion 9 kwa dakika 56 na billion 9 kuwaempower vijana kipi Cha Msingi?
Yote muhimu

Ila ss ndio waliopo in power washaamua

Mkifika na nyie mtaamua

By default mtaanza na Katiba mpya😅🤣
Sio hao vijana tena
 
A combination of both methods itumike

Wabongo wanaenda china kwa sababu za kibiashara sio kiutalii

WaTZ wengi naona utalii is just not in us hata kama tuna uwezo..
Sasa utategemeaje wajue mambo ya Seychelles na Maldives?
Kuna soko kubwa la Wamarekani weusi na ndugu zetu waliohamia Marekani na Ulaya lakini hatuwaoni. Tunawakazania tu wazee wakizungu wakati vijana wengi sasa hivi ndio wanasafiri.

Amandla...
 
Nanukuu tu
"Heche Hana tofauti na Mdude na hajui chochote zaidi ya kukaza fuvu kubishana na kupinga. Heche, Mdude, Lema wore akili ZINAFANANA."

Baba mtumishi Pep hii imekaaje mkuu?
 
Hivi billion 9 kwa dakika 56 na billion 9 kuwaempower vijana kipi Cha M

Naunga mkno kuwe na sera ya kuwezesha vijana tena wapewe hata zaidi ya bilioni 20 ila siungi mkono hoja kuipinga ku deploy 9 billion kwenye kutangaza utalii wa TAIFA. Kwasasa kwenye utalii tunawekeza kama 3billion kwa mwaka and our yield is USD2.5Billion kwa mwaka. Avator yako ni Economist sijui ni jina tu au ni mchumi kweli kama mimi
 
Wako sahihi!, kwani tungewawezesha vijana wetu wakajiajiri kama alivyopendekeza Heche mbona tungekuwa mbali sana,
Angalia umeme unavyosuasua wakati nishati hii imewaajiri vijana wengi, tunaweka siasa kwenye mambo ya msingi sana!
 
Mbona hawajaitangaza Burigi? Unatangazaje kitu kilichokwisha jitangaza?.
 
Sisi tunasema wapi?

Halafu huu muda unatumia kubweka bweka mitandaoni, ungeutumia kujifungua kuandika ili siku nyingine usiandike STIRLING
Halafu uwe na nidhamu ,wow ndio wanabweka watu wanaongea na kutoa mitazamo yao au kuandika.
 
Sasa utategemeaje wajue mambo ya Seychelles na Maldives?
Kuna soko kubwa la Wamarekani weusi na ndugu zetu waliohamia Marekani na Ulaya lakini hatuwaoni. Tunawakazania tu wazee wakizungu wakati vijana wengi sasa hivi ndio wanasafiri.

Amandla...
Royal Tour si inawafikia watu wa aina zote amaa?
 
Royal Tour si inawafikia watu wa aina zote amaa?
Mke mwenzake Meghan wewe! Watu wa aina gani wanaangalia PBS? Kule kila kundi na Channel zake. Watu wa Trump utawakuta Fox, wa Biden utawakuta MSNBC na CNN. PBS inayorusha Royal Tour nayo ina watu wake.

Amandla...
 

Kwenye club house wanapaswa kualika watalamu wawili wa jambo husika Lisu na Heche hawajui kiwanda cha utalii hata kwa asilimia 2
Wale wakialika wataalamu labda wawe upande wao
 
Mkuu,heshima kwako.
Kwenye suala LA watalii wanajua wenyewe msimu na muda wa kuja na wapi pa kuja. Istoshe watalii wengi hutokea ulaya so it is irrelevant kufanya uzinduzi marekani wakati target kubwa iko ulaya.
Pia usidhani hao tembo na faru wako huku tu....wako na kwingine kule. Kikubwa we don't need to make noise for them to come.....anyway tujipe muda.
 
Lissu aliulizwa swali huko clubhouse aeleze kwa nini Tanzania ni masikini na ifanye nini ili iweze kuendelea akajibu hivi:
Sikiliza hiyo audio
 

Attachments

Royal Tour was a bad idea.

Nguvu, muda na fedha zilizotumika haviendani na impact yake kwenye soko.

Pale ni hasara tupu.
 
Ukianza na Sarungi yule anajiita mwanaharakati lakini naona yupo kwenye kupinga kila kitu cha serikali kwake hakuna jema inafaa ajitambulishe tu ni mwana Chadema.
Ukija kwa viongozi wa Chadema nilitegemea wakati huu ambao kuna mfumuko wa vitu kupanda bei wao ndo wawe mstari wa mbele kufanya mikutano na kutoa analysis ya nini kifanyike kama kuna vipengele vyovyote vifanyiwe kazi watoe ushauri lakini wengi wao utawakuta Club house ,Kufanya mkutano kwenye redio na TV ni tofauti na kuwa Keyboard warrior wa Twitter .
Wana mkakati wa Chadema wanawaangusha sana namiss sana zile old days za kina Zitto,Mnyika akina Slaa walikua vichwa kweli sijui nini kimewapata?
 
US has influence jmn
Ulaya tungeenda nchi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…